Inakuaje mtumishi wa Serikali unajiona kama Mungu mtu? Hampewi training huko namna ya kuzungumza na wateja??

Ushauri wangu ni kwamba serikali ya CCM iache kuchezea fedha za umma kwa kufisadi na matumizi ya kipumbavu kama vile kuwalipa wake za marais badala yake hizo fedha ziende kuhudumia wananchi maskini. Wewe unashauri nini mkuu?
 
Kuna mtu aliwahi sema "Najua Kuna siku mtanikumbuka. Na mtanikumbuka kwa mema Wala si kwa mabaya"
 
Kwahiyo nilivyo kuambia upange foleni nilikosea?

Pia kukuambia nenda direct nilikosea?
Umeamua uje usema hapa wakuu mtu alikuwa anazunguka ana elezea anarudi kulekule ndio maana nikamwambia aende direct kwenye point
Sasa mbona baada ya yeye kwenye point analalamuka wewe ukarudia tena kumuuliza yale yale aliyokuwa anajaribu kukueleza hapo shida itakuwa ipo kwako ulikosea kukurupuka ungemsikiliza kwanza pengine alikuwa na hoja
 
Mimi nipo kwenye jokes mkuu
 
Ushauri wangu ni kwamba serikali ya CCM iache kuchezea fedha za umma kwa kufisadi na matumizi ya kipumbavu kama vile kuwalipa wake za marais badala yake hizo fedha ziende kuhudumia wananchi maskini. Wewe unashauri nini mkuu?
Ndio kuna wajinga wanauliza mboni kule sinza fremu ina shati 2 na suruali 3 tu sijui kufanyaje hawajui kuna watu wanapewa tu hela za ubwete
 
Mkuu uli fail pakubwa mtu kama huyo unamchana hapo hapo tena kwa msisitizo ajue yuko hapo kutoa huduma na ajue analipwa kwa kazi anayofanya kama hataki kazi akakae nyumbani kwake kuna watanzania wengi wenye uhitaji wa kazi na wanaweza kuhudumu vizuri sana.

unaruhusu vipi mtu mjinga kama huyo akuletee upuuzi. Afu unaogopa nini kumtaja hapa taasisi na sehemu anayofanya kazi ikiwezekana na majina yake, ukikutana na mtu wa sampuli iyo mnyooshe kwa lugha ngumu next time ajue wajibu wake sehemu ya kazi.
 
Nahisi katika mtaala mpya limekosekana somo la customer service, kwa ujumla ofisi nyingi za umma baadhi ya watumishi wanakosa hii kitu ya kiungwana. Pengine teknolijia ikisambaa tutamaliza kadhia nyingi online ili tusikutane na Hawa wananzengo.
 
kwa hio akihesabu na kudeposit hela unaona hapo hapo mkuu....Ila salio linapungua ukiondoka
 
kwa hio akihesabu na kudeposit hela unaona hapo hapo mkuu....Ila salio linapungua ukiondoka
Hapana sio hivyo mkuu. Nilitoka nyumbani nikiwa ninehesabu pesa zangu vizuri zimetimia nilipompa cashier akajifanya anahesabu kwa mikono kabla ya kuhesabu kwa mashine. Alipozihesabu kwa kutumia mashine ikapungua note moja ya 10000 kumbe aliidondosha chini kwa makusudi ili baadaye nikiondoka aichukue ale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…