Inakuaje mtumishi wa Serikali unajiona kama Mungu mtu? Hampewi training huko namna ya kuzungumza na wateja??

Inakuaje mtumishi wa Serikali unajiona kama Mungu mtu? Hampewi training huko namna ya kuzungumza na wateja??

mbona majority tumesoma primary to tertiary level public institutions kwa mafanikio makubwa, huduma nyingi za kijamii over 90% tunazipata kwa public facilities, changamoto zilizopo hata ungeishi first world countries kuna malalamiko mengi (people want more quality service), ingawa kwa wenzetu issues zinakuwa ni za kisera zaidi, unasema huku kwetu (shule, hospitali, barabara, majengo, nk. Ni upuuzi mtupu!) , hapo ushauriwako ni upi? ziwe privatized to serve the few privileged?
Ushauri wangu ni kwamba serikali ya CCM iache kuchezea fedha za umma kwa kufisadi na matumizi ya kipumbavu kama vile kuwalipa wake za marais badala yake hizo fedha ziende kuhudumia wananchi maskini. Wewe unashauri nini mkuu?
 
Heshima kwenu Wakuu,

Nimekwazika sana, mara ya 2 mtu unaenda kitengo flani kutaka huduma na maelekezo vizuri namna ya kufanikisha jambo lakini majibu unayopewa ni ya mkato na dharau imetamalaki.. yani sijawahi onyeshwa nyodo za hivi ata na mwanamke tokea nizaliwe.

Huyo jamaa siku ya kwanza naenda ofisini nikakuta foleni, ilikua unasikia mwezako anavojibiwa na sio mimi pekee wote ata wa mbele yangu mwendo ni ule ule majibu yake short yasiyojitosheleza.

Imefika zamu yangu, namsalimia Habari ya kazi bro, kanyanyua kichwa na kujibu 'ehee??' Basi nikaanza kujieleza shida yangu napokwama napohitaji msaada, aisee jamaaa akanichana "nenda kwenye point acha maelezo mengi".

Dah nikajikaza kiume, "ok, in a nutshell shida yangu ni hii..." cha ajabu akaomba details, kumpatia akaanza kuuliza yale yale aliyonikatisha wakati namueleza, reaction yangu nikaanza kujibu short and simple na yeye maswali yakawa mengi nilimshangaa sana.

Niliambiwa nirudi siku inayofata asubuhi opening hours, nimejihimu na kupanda boda ili niwahi foleni kufika kweli nimemkuta, kumpa salamu jibu lake.. "Njoo baadae" no time slot.

Mimi sio snitch na sipendi kuchongea ila kwa dharau alizonazo huyu pimbi natamani ata nimtafute in charge wake nitoe malalamiko. Imagine ile siku ya kwanza tuko wengi tu anasema "Jipangeni kwenye foleni, nyie si watu wazima au?" Na kulikua na watu wa makamo pale.

Kwani ukimjibu mtu vizuri unapungukiwa nn? Nakukumbusha tu mshahara unaolipwa ni kutokana na kodi zetu iweje hau heshimu walipa kodi?? Kiumri ni braza makadirio umenizidi miaka 4 au 5 apo ila heshima ni bure mzee.

Ni TRA Tanzania
Kuna mtu aliwahi sema "Najua Kuna siku mtanikumbuka. Na mtanikumbuka kwa mema Wala si kwa mabaya"
 
Kwahiyo nilivyo kuambia upange foleni nilikosea?

Pia kukuambia nenda direct nilikosea?
Umeamua uje usema hapa wakuu mtu alikuwa anazunguka ana elezea anarudi kulekule ndio maana nikamwambia aende direct kwenye point
Sasa mbona baada ya yeye kwenye point analalamuka wewe ukarudia tena kumuuliza yale yale aliyokuwa anajaribu kukueleza hapo shida itakuwa ipo kwako ulikosea kukurupuka ungemsikiliza kwanza pengine alikuwa na hoja
 
Sasa mbona baada ya yeye kwenye point analalamuka wewe ukarudia tena kumuuliza yale yale aliyokuwa anajaribu kukueleza hapo shida itakuwa ipo kwako ulikosea kukurupuka ungemsikiliza kwanza pengine alikuwa na hoja
Mimi nipo kwenye jokes mkuu
 
Ushauri wangu ni kwamba serikali ya CCM iache kuchezea fedha za umma kwa kufisadi na matumizi ya kipumbavu kama vile kuwalipa wake za marais badala yake hizo fedha ziende kuhudumia wananchi maskini. Wewe unashauri nini mkuu?
Ndio kuna wajinga wanauliza mboni kule sinza fremu ina shati 2 na suruali 3 tu sijui kufanyaje hawajui kuna watu wanapewa tu hela za ubwete
 
Mkuu uli fail pakubwa mtu kama huyo unamchana hapo hapo tena kwa msisitizo ajue yuko hapo kutoa huduma na ajue analipwa kwa kazi anayofanya kama hataki kazi akakae nyumbani kwake kuna watanzania wengi wenye uhitaji wa kazi na wanaweza kuhudumu vizuri sana.

unaruhusu vipi mtu mjinga kama huyo akuletee upuuzi. Afu unaogopa nini kumtaja hapa taasisi na sehemu anayofanya kazi ikiwezekana na majina yake, ukikutana na mtu wa sampuli iyo mnyooshe kwa lugha ngumu next time ajue wajibu wake sehemu ya kazi.
 
Nahisi katika mtaala mpya limekosekana somo la customer service, kwa ujumla ofisi nyingi za umma baadhi ya watumishi wanakosa hii kitu ya kiungwana. Pengine teknolijia ikisambaa tutamaliza kadhia nyingi online ili tusikutane na Hawa wananzengo.
 
Kuna pimbi mmoja NBC aliniibia pesa. Nilikuwa ndeposit fedha nyingi eti badala azihesabu kwa kutumia machine, akanza kuzihesabu kwa mkono kisha akawa anaziingiza sasa mashine. Ndipo ikapelea noti moja ya 10000 wakati pesa nilizihesabu vizuri tena nikarudia.

Nikaja kutonywa na mtu kwamba huwa wanajifanya kuhesabu kwa mkono kwanza ili kumzubaisha mteja. Ukizubaa tu anatupa noti moja chinikisha anaanza sasa kuhesabu kwa mashine.

Nilimkamia sana yule mwanmke siku moja nikarudi pale nimkamatishe bahati nzuri hakuwepo. Ningekiwasha asingekuja kunisahau maishani mwake.
kwa hio akihesabu na kudeposit hela unaona hapo hapo mkuu....Ila salio linapungua ukiondoka
 
kwa hio akihesabu na kudeposit hela unaona hapo hapo mkuu....Ila salio linapungua ukiondoka
Hapana sio hivyo mkuu. Nilitoka nyumbani nikiwa ninehesabu pesa zangu vizuri zimetimia nilipompa cashier akajifanya anahesabu kwa mikono kabla ya kuhesabu kwa mashine. Alipozihesabu kwa kutumia mashine ikapungua note moja ya 10000 kumbe aliidondosha chini kwa makusudi ili baadaye nikiondoka aichukue ale.
 
Back
Top Bottom