Inakuwaje baadhi ya wanawake wapo tayari kumwacha mwanaume anayempenda kisa fedha baadaye anarudi na kutaka muwe wapenzi kisirisiri?

SawA mama
 
Siyo tu kwa sababu ya pesa.

Mwanamke pia anaweza akamwacha mwanaume mwenye pesa au ambaye anampenda lakini hana dalili ya kumwoa, halafu akaolewa na mwingine (ili mradi aolewe) halafu baada ya ndoa akarudi kwa ex wake kimyakimya kuendelea na mahusiano ya siri.

Hawa ndiyo wanawake
 
Sio wanawake tu sema binadamu wengi. Ata wanaume huwa tunaacha vimbau mbau vyetu tunakimbilia wenye tako alafu baadae tunaanza kuvisumbua kurudiana vimbaumbau tulivyo viacha.
Ni hali tu ya tamaa kutaman kuishi/kupata kitu flan kwakuhis ndio kitakupa furaha lakin mwisho wa siku unakuta mambo ni tofauti na ulivyo tegemea
 
Wanawake Ni viumbe "compliketed" sana, na ndio maana Mtume Paulo alituusia sisi wanaume kwamba tuishi nao kwa AKILI.
 
Kuna watu Wana bahati
Ila Dunia haiko fair!

Hata sie wengine tulivumilia wasio na kitu ,walipopata walituacha!

Hii inatokea pande zote!
 
Kuna demu alikuwa anadate wanaume 2,mmoja Ana mpunga wa kueleweka mwingine naye kapuka.
Sasa demu alijichanganya akaukwaa ujauzito wa huyu Mwana kapuku.Akaamua kumbambikizia mimba huyu jamaa wa mpunga.Jamaa akalea mimba.

Miaka kadhaa ikapita shillingi ikageuka.Huyu jamaa aliyekuwa na pesa akasota na huyu aliyekuwa kapuku mwanzoni upepo ukamuelekea akawa tajiri.
Demu hakusita kugeuza meza,akaamua kurudisha mtoto kwa baba Yake halali Sasa.
Life likasonga.
 
Wanawake walio wengi
Daaah huyo demu kavu kishenzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…