Inakuwaje kila anayeusema ukweli kuwa Bunge ni dhaifu, itafsiriwe kuwa amelidhalilisha Bunge na kuitwa kwenye Kamati ya Maadili?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imemuhoji mbunge Jerry Slaa, mbunge wa Ukonga, kwa tiketi ya CCM, kutokana na amri iliyotolewa na Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai, kwa madai kuwa amesema uongo na kulidhalilisha Bunge hilo!

Ikumbukwe kuwa mbunge Jerry Slaa, siku chache zilizopita, akiwahutubia wakazi wa Jimbo lake la Ukonga "alitoboa" siri kuwa wabunge hawalipi kodi za serikali, kutokana na kipato chao, kama wafanyavyo wananchi wengine.

Ieleweke pia kuwa wabunge hao wanawawakilisha wananchi kwenye majimbo yao kwenye Bunge hilo.

Sasa sioni makosa ya Mbunge Slaa aliyoyafanya kwa kuusema ukweli kwa wakazi wake wa Jimbo analoliwakilisha

Kumekuwepo na kilio kikubwa mno toka kwa Umma wa wananchi wa nchi hii, kutokana na kodi kubwa Sana "wanazokamuliwa" na Bunge hilo hilo, Katika miamala ya simu, kulipia kodi ya majengo kwa kutumia LUKU na kulipia kodi kwa kila lita moja unayonunua kwenye vituo vya mafuta kwenye Petrol stations.

Hivi si kila mwananchi amepewa uhuru huo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 18(1) sasa inakuwaje tena kila anayeusema ukweli kuhusu Bunge hilo kuwa dhaifu, anatishwa na Spika Ndugai, kuwa ataburuzwa kwenye Kamati hiyo ya Bunge?

Hivi ni mtanzania gani asiyeujua ukweli mchungu, kuwa Bunge letu kuwa dhaifu, kunatokana na wabunge karibu wote, kuwa ni wa chama kimoja cha CCM?

Inajulikana kuwa kazi ya Bunge ni kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi, sasa inapotokea Bunge hilo likawa la kupitisha kila hoja inayoletwa na serikali hii, linaweza kuepuka vipi, kuitwa dhaifu?

Niseme wazi kuwa Mbunge Slaa, ameutoboa ukweli kwa kusema kuwa wabunge wanspaswa kumuogopa Mungu, kwa kusimamia haki za wananchi, badala ya kujipendekea wao wenyewe binafsi.

Hivi inaingia akilini kweli kwa wabunge hao kupitisha sheria za kuwakamua kodi kubwa Sana, za PAYE, kodi za miamala ya simu, kodi za majengo kwa kupitia LUKU, kwa wananchi wa kipato kidogo Sana cha laki 2 na kuwaacha wabunge hao, bila kulipia chochote, wenye kipato kikubwa Sana cha zaidi ya shilingi milioni 10 kwa mwezi?

Imenenwa kwenye Biblia Katika kitabu cha Mithali, sura ya 14:34 inayosema kuwa "Haki huliinua Taifa na dhambi ni aibu ya watu wote" mwisho wa kunukuu.

Kulijengea kinga Bunge hilo ili lisikosolewe, kama afanyavyo Spika Ndugai, hakulisaidii Bunge hilo, badala yake ndiyo linazidi kulifanya kuwa dhaifu

Kama Bunge letu halitotenda Haki kwa wananchi wake, basi litarajie wakati wote kupokea shutuma kuwa Bunge hilo ni dhaifu na lisitegemee kuwa kwa kutumia vitisho vya Spika wake, Job Ndugai, atazima kelele hizo.
 
Yaan wangewaingizia tu kwenye simu zao mishahara na posho at least wangefeel ht wasipolipa PAYEE
 
Mwulize Pascal atakupa ukweli jinsi mziki wa kuhojiwa na kamati ulivyo! Alivyorudi kutoka kule akajisalimisha Lumumba kukabidhi akili yeye akabaki na kopo tupu! Lakini itoshe kusema bunge hili la Ndugayi ni dhaifu!
 
Kulijengea kinga Bunge hilo ili lisikosolewe, kama afanyavyo Spika Ndugai, hakulisaidii Bunge hilo, badala yake ndiyo linazidi kulifanya kuwa dhaifu
Kwa katiba hii inayompa Ndugai umungu mtu bunge ni dhaifu, halitusaidii, halihitaji kuisimamia serikali kwani wananchi hutuna NGUVU ya kuhoji utendaji wake popote. Speaker kaligeuza mahala pa mipasho yake na vigodoro. Simuoni Mbunge ambae yuko tayari kujilipua. Katiba Mpya ndio DAWA.
 
Ni kweli bunge ni dhaifu sana kutokana na uongozi dhaifu.
Hata wabunge waliopo kule kuna ambao hawastahili kabisa kuwepo lkn wapo kutokana na uongozi dhaifu.
 
No institution can be better than its people.Mbunge wa kongwa ni dhaifu.Yangu ni hayo tu
 
Watanzania hatuna bunge, waliopo bungeni wamewekwa na magufuli kwa hila na barrel of gun. Hatuwatambui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…