Angekua hana akili, Mwenyekiti wako angemuahidi cheo kizuri kipindi kile cha kampeni baada tu ya kuona mwamba anamsababishia pumzi yake kukata mara kwa mara?
By the way, mlitaka abakie nchini ili muendelee kumfanyia zile hila zenu? Yule ni akili kubwa! Baada ya kuwagundua, akawazidi akili kama kawaida yake. Na mashabiki wake tunamuelewa sana.
Usisahau pia Mh. Tundu Lissu ni baba wa familia! Na mke wake anaishi naye huko huko Ubelgiji anakopata matibabu yake yaliyotokana na lile jaribio lenu lililoshindwa la kutaka kumuua mchana kweupe.