Inakuwaje kwa madaktari tuliowasomesha lakini wamekimbilia bungeni kufuata maslahi mazuri!

Inakuwaje kwa madaktari tuliowasomesha lakini wamekimbilia bungeni kufuata maslahi mazuri!

Waalimu wote ni wanasiasa bwashee!

Ila daktari ana umaalumu wa kipekee popote pale duniani.

Kutibu ni ibada!

Ibada au kwenye ibada hakutakiwi kulazimisha ni hiyari tu, sawa akisharudi kwa lazima itakuwa je ? Kama mimi doctor kila alie shiriki nirudi akiumwa akija harudi home ndio dawa
 
Yuko sahihi kabisa.

Sisi tulipomaliza chuo ilikuwa ni lazima kuitumikia serikali kwa miaka 5 kabla hujaenda sekta binafsi au haujajiajiri!
Mlisomeshwa bure na hakuna hata senti tano mlikuwa nairudishia serikali. Hivyo, ilikuwa halali kufanya kazi serikalini 5 years.

Sasa mimi nilidhani mtu akitafuta kazi yenye maslahi mazuri akiwa ndani ya nchi ndiyo vizuri zaidi. Hii ni kwa sababu nadhani mtu huyu ataweza kurudisha mkopo wa elimu haraka na wengine wapate furusa ya kusoma.

Nadhani mtu huyu anastahili pongezi kwani mbali na mkopo wenyewe kupigwa retention fee nje ya makubalianao, bado mshahara wake unakatwa PAYE ya nguvu, makato ya mifuko ya hifadhi jamii, bima, nakadhalika. Lakini, malimbikizo ya ama nyongeza ama stahiki zake mfanyakazi huyu zinazocheleweshwa hata siku moja hajawahi kuidai Serikali retention fee!!! Ni ajabu sana mfanyakazi wa namna hii anayefanya kazi nchi kumuita majina yasiyofaa.

Lugha za kukatisha tamaa ziepukwe ili watu wafanye kazi kwa morali, hizo elimu hawakuzipata kwa kusinzia wametokwa jasho na damu kuzipata; vinginevyo wafanyakazi hawa wana akili nzuri tu za kufanya maamuzi ya kushangaza! Tusifike huko.
 
Huyu mtu ni mgonjwa. Acheni ubishi. Mpeni matibabu stahiki tena toka kwa huyo daktari aliyemnanga kabla hali haijawa mbaya zaidi.
Double Standards za kiwango cha sgr.Wamechepuka wengi tu na wengine baada ya kukosa ajira wamegeuka Machinga,hao nao wasakwe watulipe fedha zetu za mkopo wa elimu ya juu.
 
Ndio tunao madaktari waliokacha taaluma zao na kugombea ubunge ili wapate maslahi makubwa na mazuri zaidi.
Je, hawa wako kundi gani?

Hawa wameacha kabisa kutibu tofauti na wale wanaoendelea kutumikia taaluma zao katika sekta binafsi au kwenye taasisi za dini na zile za kijamii.

Maendeleo hayana vyama!
Mi nadhani kuna fyuzi haziko sawa kwa huyu jamaa.
Syo madaktari tu walosomeshwa na serikalo na ambao hawafanyi kazi serikalini.
Mi sjui bana naishia hapa
 
Back
Top Bottom