DOKEZO Inakuwaje mradi unapewa hela zaidi ya walizoomba na haukamiliki?

DOKEZO Inakuwaje mradi unapewa hela zaidi ya walizoomba na haukamiliki?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Nimepitia bajeti ya wizara ya Afya 2024/25 iliyosomwa bungeni May 14, nimekutana na kituko kwa baadhi ya miradi. Mmoja wa mradi wenye kituko ni Uimarishaji ya Hospitali za Rufaa - Mawezi. Mradi huu ulihitaji Sh bilioni 7 na ukapokea bilioni 12 lakini bado haujakamilika, upo 86%. Yaani kuna sehemu ya hospitali haitoi huduma, sasa nawaza hili linawezekanaje, je hakuna anayefuatilia kujua kwamba hela imezidi na bado mradi unasuasua

Hela iliyozidi ni 69.8% ya hela iliyokadiriwa kutumiwa na mradi huo, je kuna upigaji?
Screenshot 2024-05-14 111851.png


Ufafanuzi wa Serikali - Wizara ya Afya yafafanua juu ya gharama za Mradi wa Hospitali za Rufaa Mawenzi
 
Ili kuongeza uwazi, ukweli na uwajibikaji, ni bora matumizi ya bajeti hizi (distribution or expenditure of money) yawekwe wazi. Yaani, kama ni ukarabati wa vituo vya afya viainishwe au kama ni ujenzi wa miundombinu yote itajwe. Hii itasaidia hata sisi wananchi kuweza kufanya tathmini ya utendaji kazi wa viongozi wetu. Kwa sababu bajeti zinasomwa ila zinakuwa zimefungwa (ziko kwenye closed way na general). Sio rahisi kujua vitu vitakavyo tengenezwa lakini pia kujua ni kwa kiwango kipi. Kwa hali hii upigaji au hela hewa ni rahisi sana kutokea.
 
Back
Top Bottom