Ili kuongeza uwazi, ukweli na uwajibikaji, ni bora matumizi ya bajeti hizi (distribution or expenditure of money) yawekwe wazi. Yaani, kama ni ukarabati wa vituo vya afya viainishwe au kama ni ujenzi wa miundombinu yote itajwe. Hii itasaidia hata sisi wananchi kuweza kufanya tathmini ya utendaji kazi wa viongozi wetu. Kwa sababu bajeti zinasomwa ila zinakuwa zimefungwa (ziko kwenye closed way na general). Sio rahisi kujua vitu vitakavyo tengenezwa lakini pia kujua ni kwa kiwango kipi. Kwa hali hii upigaji au hela hewa ni rahisi sana kutokea.