Inakuwaje mtu anaoa lakini bado anategemea nyumbani asaidiwe?

Inakuwaje mtu anaoa lakini bado anategemea nyumbani asaidiwe?

Kifaru86

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2017
Posts
1,734
Reaction score
3,822
Tofauti na zamani ila ndoa nyingi zinazofugwa miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia vijana wengi wanaoa unakuta bado anategemea nyumbani asaidiwe.

Kuna wengine anaoa yeye na mkewe anaishi nae nyumbani kwao na hapo unakuta kila kitu anategemea nyumbani familia imuhudumie yeye na mkewe.

Ni kwanini hali hujitokeza nini chanzo?
 
Mkuu ongezea kuwa Ndoa hizo nyingi huwa hazidumu sana, kwasababu chance ya kidume kukimbia majukumu kwa kigezo hana hela ni kubwa..

Malezi ya kimagharibi pia yamepelekea hayo, TUMESAHAU Wale wenzetu wanadekezwa lakini pia maisha yao yanakuwa mazuri sana
 
Tofauti na zamani ila ndoa nyingi zinazofugwa miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia vijana wengi wanaoa unakuta bado anategemea nyumbani asaidiwe.

Kuna wengine anaoa yeye na mkewe anaishi nae nyumbani kwao na hapo unakuta kila kitu anategemea nyumbani familia imuhudumie yeye na mkewe.

Ni kwanini hali hujitokeza nini chanzo?
Inakuwaje Nchi inapata Uhuru lakini inaomba misaada?
 
Ujinga wa namna iyo nilishaukataa[emoji3525]
JamiiForums1558615499.jpg
 
Sana sana nimeona ikitokea kwa watoto ambao wazazi wao wana uwezo. Kuna jirani yangu yeye watoto wake wamefika mpaka chuo kikuu lakini bado wanamtegemea. Sasa yeye ana mdogo wake ambaye maisha yake ni ya shida na watoto wake wamesomeshwa na kaka yake ambaye ndiye mwenye uwezo. Cha ajabu wale watoto wamekomaa na maisha na wapo vizuri ukiwalinganisha na hao wengine. Hawa pia hawakuweza kufika chuo kikuu lakini wameweza kujenga nyumba zao na kuoa bila msaada wa mtu yeyote lakini wale wa kaka yake maisha yanawapiga chenga. Hitimsho ni kwamba watoto wa wakubwa wengi wao maisha yanawapiga chenga.
 
Back
Top Bottom