Inakuwaje mtu kwao Kigoma anakuwa Simba?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Nimechukulia Kgm kama mfano tu, hoja yangu ni kwamba kwa nini kila mtu TZ nzima ni mpenzi wa Yanga au Simba hata kama hawajazaliwa na wala hawakulia Dar, kwa nini wasiwe wapenzi wa timu zao huko Mikoani? Kwa mfano mtu Iringa kwa nini ashabikie Yanga au Simba na siyo Lipuli?

Kila Mkoa una timu zake sasa hizi timu za Mikoani zina maana gani kama watu wa Kigoma wanakuwa wanachama wa Simba au Yanga?

Je ni muendelezo ule ule wa sisi Waafrika weusi kutokuelewa Dunia inavyokwenda?
 
Ngumu kushabikia timu zisizoleta msisimko. Mimi hata hizo Yanga na Simba zenyewe naona mizinguo tu. Tutang'ang'ana na league za wenzetu, zina akili kwa kweli.
 
Lkn zitaletaje msisimko kama hakuna anayezijali? Hizo za nje unaziona hivyo kwa sababu wanachama wao hawasemi kama wewe, kumbuka mpira ni wanachama na ndiyo maana wanaziita Clubs kuna sababu!
 
Mimi bwana ni shabiki was Panone Fc ya kwetu moshi ligi daraja la kwanza huko.
 
Lkn zitaletaje msisimko kama hakuna anayezijali? Hizo za nje unaziona hivyo kwa sababu wanachama wao hawasemi kama wewe, kumbuka mpira ni wanachama na ndiyo maana wanaziita Clubs kuna sababu!
Kama hizi timu zetu zingeonesha potential tungekuwa na mapenzi nazo, lakini kila siku ni heart break. Hawatupi sababu za kuzishangilia.
 
Kwa hiyo ulitaka wengine wajenge na wewe uje tu kushabika? Nafikiri inaelekea unapenda mpira lkn haulewi maana ya football club!
 
Naelewa vizuri. Hata mwanao ukiona hawezi shule msupport kwenye jema analoliweza. Some football clubs were just not mean't to be period.
 
Kwa hiyo ulitaka wengine wajenge na wewe uje tu kushabika? Nafikiri inaelekea unapenda mpira lkn haulewi maana ya football club!
Potential ndio inayojengwa. Sasa hata kiwanja huna, where do you put that foundation? Hewani??
 
Kauzu FC na Kibada FC ndio timu zangu! Simba,Yanga izo timu tangia uhuru hamna cha maana wanachofanya.
 
Huwo ndiyo uelekeo mzuri, inashangaza na kusikitisha sana kuona nchi nzima ni Yanga au Simba!
 
Potential ndio inayojengwa. Sasa hata kiwanja huna, where do you put that foundation? Hewani??

Swali ni kwamba unataka nani afanye hiyo kazi? Kwa maana inaonyesha unalaumu hiki hakuna kile hakijafanyika!
 
sasa nishabikie toto africans kweli? wakati najua ni tawi la yanga?
 
Back
Top Bottom