Inakuwaje Mutual Fund za Kenya zinatoa faida 25%?

Inakuwaje Mutual Fund za Kenya zinatoa faida 25%?

Kiongozi faida ni kama hizi za UTT tu sababu MF nyingi duniani mifumo yanuendeshaji inafanana kama vile mifumo ya kibank worldwide inafanana.. ingawa kwa kenya soko lao pana zaidi.. kwa maana ya kuwa wanakampuni kubwa nyingi zaidi..

na kuhusu risk kama unazungumzia risk za ww kama foreigner kuwekeza kule hapana risk ya kuogopa sababu unajisajili kwenye mfumo rasmi na foreign investor wanaruhusia kama ilivyo hapa UTT

Anyway kikubwa kwa Kenya wana uwanja mpana wa hii mifuko.. na ipo ambayo ina miaka mingi sokoni na ipo ambayo ya miaka ya karibuni kuna inayotoa dividends na kuna ambayo haitoi unakuwa unakuza mtaji kikubwa kwanza weka malengo kisha tafuta mfuko unaofaa malengo yako

Ngoja nikupe mfano mdogo kupitia mie sababu nina UTT kwa nje nilitaka uwekezaji wa kitofauti nilitaka niwekeza kwanza kwanza kwanza kwa fedha ya kigeni ila nikitumia Tsh lakini pia nilitaka njia ya kuwekeza kwenye masoko ya hisa ya duniani (mainly china and US) mfano kwenye masoko ya kampuni za teknolojia (microsoft,apple) , afya(pizfier), madini (gold) na mengineyo.. sasa kawaida unatakiwa uwe na pesa ndefu kuwekeza direct kwenye masoko hayo au kama unaishi marekani unaweza kuwekeza kwenye ETF zao ila nje ya marekani as individual ni ngumu

Sasa kwa kenya walianzisha Funds ambayo inatoa uwekezaji wa ETF kitu ambacho nilikuwa nakitaka ili ku diversify my portfolio ndio maana nikawekeza huko kwenye mfuko wao wanauita NDOVUlezee

Nilichokifanya ili transactions ziwe rahsi nilifungua account ya KCB TZ sababu ni bank ya kenya na mfuko niliowekeza custodian ni KCB ili kupunguza ukiritimba wa kati ya taasisina taasisi so na deposit kwenye account nalipia kupitia account yangu ila kwenye uwekezaji wangu inasoma pesa ya kenya na mfuko mwingine US dollar
Mkuuu naomba utuelezee more about this
 
Hii elimu ya finance wabongo wengi hatuna na hatuipati kabisa kwa wakati sahihi. Sad !!

Mtu unakaribia kuingia umri wa majeruhi, mkononi umebahatika kusave let say TSH 20M (very very hardly earned & saved), na kwa umri ulivyo unaona kabisa hii ni 'penalti ya mwisho'.....

Connections za kibiashara hauna!
Biashara za kuingia mwenyewe kichwa kichwa napo unaogopa kifo cha mende!
Elimu au knowledge ya mutual funds/bonds hauna!

Unabaki njiapanda tu na kuwaachia bank hiyo TSH 20m waendelee kuipukuchua kwa monthly charges zao za kiwizi.

Kwakweli kwenye financial literacy, watz wengi tuna knowledge gap kubwa mno!

Fredwash , kali linux
100% !!
 
Kiongozi itakuwa
Rahisi kwangu kukuelezwa kama nitafaham unahitaj kujua nini labda cha zaidi
mkuu kwema? mimi ni mwanachama wa UTT wa muda sasa, nimevutiwa na maelezo uliyotoa katika uzi huu, nimeshawishika kuanza kuwekeza katika mutual fund za Kenya. Naomba kujua mfuko mzuri ni upi, riba yake ni asilimia ngapi? makato ya kodi na gharama nyungine yapoje? na nikitaka kujiunga sasa hivi naanzia wapi? Asante sana mkuu kwa darasa zuri
 
Karibu mkuu nishaifungua ila saturday ndio siku nzuri walau napataga mda wa kuingia huku mara kwa mara
 
Karibu mkuu nishaifungua ila saturday ndio siku nzuri walau napataga mda wa kuingia huku mara kwa mara

cheers mkuu. Nimeshakutumia pm.

Okay, on your suitable time nitafurahi kusoma response yako on my issue privately. Blessings.
 
Karibu mkuu nishaifungua ila saturday ndio siku nzuri walau napataga mda wa kuingia huku mara kwa mara
Kaka Kwema? kwanini ulichagua mutual fund ya ndovu? Nimefanya tafiti ndogo, nimegundua LOFTY CORBAN ndio mutual fund yenye rate kubwa Kenya kwa sasa, why umechagua ndovu? Hii Lofty Corban nimeona wana mifuko mitatu, upo mmoja ambao ni hight risk, nataka kuweka hela kidogo, na mwingine ni low risk, ntaweka hela nyingi.
Ila mifuko yao ina Kes na USD option nzuri ni ipi? taratibu gani naweza kufuata kujiunga? je hiyo riba ya asilimia kumi na nane wakikata na kodi si tunarudi kwenye riba sawa na UTT?
 
mkuu Fredwash naomba uje useme neno hapa
 
mkuu kayanda01 vipi una neno la kutia hapa?
 
Nimeshangaa sana watu wanakula faida 25% kwa mwaka tofauti na hapa bongo kubwa ni 15% huku wengi wakiishia 12%
Kulikoni wadau,
Huku performance nzuri ilikuwa 2021 mfuko wa wekeza maisha ulifikisha mpaka asilimia 25% sasahivi wakitoa sana ni 15%
 
Hii Jamii forum bwana, nyuzi za maana hivi zinaishia page ya tatu zinakufa, watu hawataki kuchangia, ingekuwa ni uzi wa kujadili ngono tungekuwa page ya 200
 
Back
Top Bottom