Inakuwaje Rais anapokataa kuishi Dodoma?

Inakuwaje Rais anapokataa kuishi Dodoma?

Kama mabalozi wapo Dar na wamegoma Dom basi na sisi tunakaa karibu ili kuomba iwe rahisi
 
tumetumia fedha nyingi kujenga makao makuu dodoma ili shughuli za kiserikali zihamie huko na dar zibaki shughuli za kibiashara, chakushangaza makongamano bado yako JNICC, sasa waziri mkuu na naibu wake wanapokuwa dar wanalala hotel au nako wanamakazi? makamu wa rais na waziri mkuu wakiwa dar automatically igp cdf watakuwa dar ndo mji haupitiki.

haya tuache hao wakuu wa nchi, hata mahafali ya chuo kikuu nayo kuna sababu gani yakufanyikia dar? kuna shida gani wahitimu wa udsm ifm kufanyia mahafali yao dodoma, sasa hivi barabara hazipitiki kila kona ni misafara ya majoho, hotel na guest nazo tabu kila kona pako full,

hebu jiulize ukipanda nyehunge kutoka mwanza kwenda dodoma saa saba mchana uko dodoma, ukipanda sgr kutoka dar to dom saa nne uko dodoma, kinacholazimisha kwenda dar ni nini? baada ya kongamano.mnapita hapohapo dodoma mkienda mwanza kigoma kagera kartesh tabora singida, hivi tunafikiri sawasawa kweli?
 
Dawa ni Moja tuu...Kumchagua Mgogo kuwa Tenant wa Chamwino...na akitoka Mgogo tunampangisha mtu wa Singida au mwenyeji wa Kanda ya Kati...wakishazoea ndio sasa twaweza kodisha yeyote kutoka pembe yoyote ya Jamhuri ,manake trend itakua imeshakuwa set
 
Nchi bado inasukwa jamani, mnadhani nani anapenda kuishi porini?

Treni ya umeme hiyo, tuwe tunaenda Dodoma na kurudi siku hiyo hiyo, viwanja vya ndende vinajengwa tuwe tunaenda na kuridi Dar es salaam siku hiyo hiyo, mnadhani kuishi Dodom ni rais?

Mwacheni naye ale raha, urais wenyewe ulimdondokea tu, labda asingeipata hiyo nafasi milele, sasa kaipata bata muhimu.

Magufuli alikuwa anapajenga Chato, bahati yenu alifaraki mapema wote mgehamia kule.
 
Je vyombo vya ulinzi haviwezi kumlazimisha ?

Je vyombo vya ulinzi vinashindwa Nini kumtaka Rais akaishi Dodoma?

Hasara za Rais kutokuwa na makazi maalumu si ni hasara kwa walipa Kodi maana gharama za kumlinda uongezeka ?

Mabilioni yaliyojenga ikulu dodoma je ni hasara? Hasara kwa Nani? Kama muhusika haishi pale?

Magogoni, kizimkazi na Dodoma ni wapi makao makuu ya nchi?
Kotekote !
As long as it’s part of Tanzania 🇹🇿 United Republic 😳👍🇹🇿👍
 
Back
Top Bottom