tumetumia fedha nyingi kujenga makao makuu dodoma ili shughuli za kiserikali zihamie huko na dar zibaki shughuli za kibiashara, chakushangaza makongamano bado yako JNICC, sasa waziri mkuu na naibu wake wanapokuwa dar wanalala hotel au nako wanamakazi? makamu wa rais na waziri mkuu wakiwa dar automatically igp cdf watakuwa dar ndo mji haupitiki.
haya tuache hao wakuu wa nchi, hata mahafali ya chuo kikuu nayo kuna sababu gani yakufanyikia dar? kuna shida gani wahitimu wa udsm ifm kufanyia mahafali yao dodoma, sasa hivi barabara hazipitiki kila kona ni misafara ya majoho, hotel na guest nazo tabu kila kona pako full,
hebu jiulize ukipanda nyehunge kutoka mwanza kwenda dodoma saa saba mchana uko dodoma, ukipanda sgr kutoka dar to dom saa nne uko dodoma, kinacholazimisha kwenda dar ni nini? baada ya kongamano.mnapita hapohapo dodoma mkienda mwanza kigoma kagera kartesh tabora singida, hivi tunafikiri sawasawa kweli?