Inakuwaje tuambiwe Corona inapungua ilhali wagonjwa wanaongezeka?

Inakuwaje tuambiwe Corona inapungua ilhali wagonjwa wanaongezeka?

Ile tafrija mliyo ifanya ilikuwa ya nini? Au ndiyo kutafuta kiki?
Aya ya kwanza ni lawama.

Aya mbili za mwisho ndiyo za msingi, kwamba korona haijaisha na wanaopuuza kuzingatia ushauri wa kujikinga dhidi ya maambukizi, hakuna shaka wataambukizwa. Ndio hao wakuongezeka na watakaongezeka zaidi.

Takwimu kisiwe kigezo cha kuzingatia ushauri bali kila mtu kwa maamuzi yake mwenyewe:

AJIKINGE AMKINGE JIRANI

AJILINDE AWALINDE WAPENDWA WAKE

Tanzania bila COVID-19 inawezekana. Timiza wajibu wako la utakuwa mmoja wao.
 
Kuna watu wanashinda airport kuwasubiria watu weupe wakishuka tu wanatutangazia kuwa ni watalii
Hakuna lawama yeyote zile ni takwimu zilizotolewa na viongozi.

Ninaweza kuwa natimiza wajibu wangu wa kujikinga lkn kama serikali yenyewe haitimizi wajibu wake ni kazi bure, maana huu ugonjwa haukuanzia Nangurukuru umekuja kwa ndege, mimi siwezi kudhibiti wanaoingia nchini mipakani, bandarini na airport.
 
Utakubaliana na mimi kuwa wajibu wa Serikali ni kuweka mazingira salama ya kuzuia maambukizi km kusimamia ipasavyo ushauri wa kujikinga dhidi ya maambukizi unafuatwa bila shurti, km sehemu zenye mikusanyiko (mipakani, viwanja vya ndege, usafiri wa abiria, nk) wahusika wawajibike kuhakikisha watu wanazingatia kanuni za kinga dhidi ya maambukizi. Wewe na mimi pua nyimbani kwetu tuwajibike.

Kwa mtu mmoja mmoja, kama ni lazima kuwepo kwenye mkusanyiko wa watu wenye kila uwezekano wa maambukizi, ni budi kujiandaa. Mtu ajilaumu mwenyewe akiambukizwa km hakuvaa barakoa lakini anakuwa karibu na mtu ambaye naye hakuvaa barakoa.

Kuongezeka kwa maambukizi hakika ni ya watu walioanza kupuuza. Hata Uganda na Rwanda ambako Serikali iliweka "lockdown" wagonjwa wanaongezeka, sebuse Tanzania ambako watu wako huru wakiendelea na maisha yao ya kila siku!

Sikubaliani na hoja ya kuitaka Serikali itangaze takwimu kwa kuwa siyo msingi wa mtu kuzingatia ushauri wa kinga ila ama ni kuweka hofu au kuijengea jamii imani potofu kuwa ugonjwa haupo. Takwimu ziendelee tu kutumika na utawala, ngazi zote, kufuatilia na kuthamini kiwango cha maambukizi ili kuchukua hatua stahiki na haraka iwezekanavyo.

JIKINGE UMKINGE JIRANI

JILINDE UWALINDE UWAPENDAO.
Wacha kuandika ujinga wewe, leo hii china corona imelipuka tena kwa speed ya rocket [emoji573] lkn bado viwanja vyetu vya ndege mnaendelea kuwapokea wachina kila siku kisa ni watalii
 
Hatareeeee
Ni ajabu wewe bado unaamini taarifa za hawa watu.

Kama wamesema hivyo, ujuwe kuna sababu inayowafanya waseme hivyo. Inaweza kuwa ni hadaa ya kuombea misaada toka nje kupitia mgongo wa huo ugonjwa.
 
Maana rahisi ya uongozi ni kuonyesha mfano.
Nakubaliana na wewe lakini katika suala la maisha yako utakuwa ni ujinga kufuata anachofanya kiongozi wako. Na katika maisha ya kila siku ni wajibu wa kila mtu kutii sheria bila shurti.
 
Kunakupona na kuugua shoda iko wapi

Mkuu acha dharau, tuliambiwa tumeishinda korona. Maana yake isingekuwepo na hata kabisa hata kwa wagonjwa. Tukatoa na dua za shukrani.

Ukweli ni kuwa corona ipo na sisi. Tuchukue tahadhari na hili ndio jambo viongozi wanapaswa kusisitiza. Kuikana corona hakufanyi iondoke. Kukebehi uvaaji wa barakoa hakuiondoi corona!
 
Taarifa za watu kufa au kuugua ni ndugu pekee ndio wanaojua sasa watu wasitutengenezee takwimu zao uchwara , na kama watu wakifa au kuugua hawajifichi wanaonekana na sio siri tena.
Huu ndio ujinga wa ajabu sana ndani ya nchi hii.

Na ninaamini unajiona mjuaji kwa haya uliyoandika hapa kwa sababu ya ujinga tu wa kutojua maana na sababu za takwimu kuhusu mambo kama haya.
 
Wiki iliyopita Waziri wa Afya alitutangazia kuwa Tanzania imebakiwa na wagonjwa wanne 4 tu walio na virusi vya COVID-19 baada ya wagonjwa waliofikia 500+ kabla kupona na ugonjwa kupungua kama sio kwisha kabisa. Leo Waziri Mkuu anatuambia kuna wagonjwa 66 nchi nzima.

Ni takriban wiki imepita tulifanya sherehe (Corona part) kusherehekea kuisha kwa ugonjwa wa Corona, Tanzania ya ajabu sana.

Kuna thread moja imeanzishwa humu JF inasema Tanzania inaweza kuwa Taifa la Watu Wajinga zaidi Duniani! naanza kukubaliana na mleta mada.

Kifupi ukiambiwa Corona Tanzania imekwisha changanya na za kwako. Nchi za wenzetu zinajiandaa na mlipuko wa pili wa ugonjwa sisi tume relax.

Muhimu jikinge binafsi na mkinge na mwenzako, nawa mikono, vaa barakoa, epuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima.
Siasa tu hizo corona ipo sana.
 
Kifupi ukiambiwa Corona Tanzania imekwisha changanya na za kwako. Nchi za wenzetu zinajiandaa na mlipuko wa pili wa ugonjwa sisi tume relax. [emoji120][emoji120][emoji120]

Fundi mchomelea mageti.
 
Back
Top Bottom