Inakuwaje tuambiwe Corona inapungua ilhali wagonjwa wanaongezeka?

Ile tafrija mliyo ifanya ilikuwa ya nini? Au ndiyo kutafuta kiki?
 
Kuna watu wanashinda airport kuwasubiria watu weupe wakishuka tu wanatutangazia kuwa ni watalii
 
Wacha kuandika ujinga wewe, leo hii china corona imelipuka tena kwa speed ya rocket [emoji573] lkn bado viwanja vyetu vya ndege mnaendelea kuwapokea wachina kila siku kisa ni watalii
 
Hatareeeee
Ni ajabu wewe bado unaamini taarifa za hawa watu.

Kama wamesema hivyo, ujuwe kuna sababu inayowafanya waseme hivyo. Inaweza kuwa ni hadaa ya kuombea misaada toka nje kupitia mgongo wa huo ugonjwa.
 
Maana rahisi ya uongozi ni kuonyesha mfano.
Nakubaliana na wewe lakini katika suala la maisha yako utakuwa ni ujinga kufuata anachofanya kiongozi wako. Na katika maisha ya kila siku ni wajibu wa kila mtu kutii sheria bila shurti.
 
Kunakupona na kuugua shoda iko wapi

Mkuu acha dharau, tuliambiwa tumeishinda korona. Maana yake isingekuwepo na hata kabisa hata kwa wagonjwa. Tukatoa na dua za shukrani.

Ukweli ni kuwa corona ipo na sisi. Tuchukue tahadhari na hili ndio jambo viongozi wanapaswa kusisitiza. Kuikana corona hakufanyi iondoke. Kukebehi uvaaji wa barakoa hakuiondoi corona!
 
Taarifa za watu kufa au kuugua ni ndugu pekee ndio wanaojua sasa watu wasitutengenezee takwimu zao uchwara , na kama watu wakifa au kuugua hawajifichi wanaonekana na sio siri tena.
Huu ndio ujinga wa ajabu sana ndani ya nchi hii.

Na ninaamini unajiona mjuaji kwa haya uliyoandika hapa kwa sababu ya ujinga tu wa kutojua maana na sababu za takwimu kuhusu mambo kama haya.
 
Siasa tu hizo corona ipo sana.
 
Kifupi ukiambiwa Corona Tanzania imekwisha changanya na za kwako. Nchi za wenzetu zinajiandaa na mlipuko wa pili wa ugonjwa sisi tume relax. [emoji120][emoji120][emoji120]

Fundi mchomelea mageti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…