Inakuwaje unanunua vocha ya simu (scratch card) unaingiza namba kwa usahihi kabisa unaambiwa namba ya vocha uliyoingiza haipo?

🌤️🙋‍♂️✍️🎯👌👍👏👊🤝🙏
 
Duh, ukamfokea dada wawatu bure
 
Vocha hutoka kwa mfumo wa batch
Yawezekana iyo batch haikua activated ndo maana hukuweza itumia Kuna mchangiaji amesema aliwahi jaribu vocha ikamgomea baada ya week ndo ika kubali kwa hiyo ishu hapo ni activation ya batch husika haikua ime fanyika watu wa mfumo Wana lielewa vzuri hili
Cc. Vodacom Tanzania
 
Dah nimekumbuka mbali sana miaka ya nyuma wakati niko chuo Dar nilikuwaga napiga sana vocha za watu kwenye daladala hasa kama nakuwa nimesimama alafu anayeweka vocha amekaa. Nilikuwa nikiona mtu anatoa vocha na kuanza kukwangua mimi naweka simu yangu tayari. AKISHAMALIZA TU ile anatoa simu yake mimi tayari naanza kuingiza namba na kuikubali yeye akijakumaliza simu inamwambia vocha unayojaribu kuingiza imeshatumika. Duh uhuni mwingine siyo mzuri kabisa.
 
Ulifanya vizuri sana kujiita Kijana masikini
 
Aisee kuweka salio kwa vicha, duu kitambo kweli sijatumia hii huduma.
 
Aisee utakuwa uliniibia mimi tafadhali nirudishie! Niliibiwa kwa mtindo huo natoka Sinza kwenda Posta! Ilikuwa ya elfu tano wakati ule tulikuwa tunaita dola tano😆
 
Asante kwa elimu hiyo. Japo hii vocha niliinunua zaidi ya wiki kabla ya kuikwangua wacha ikae hata mwezi nitaijaribu tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…