Kuna siku niliwapigia yas huduma kwa wateja baada ya kuwa nanunua kifurushi cha intaneti cha elfu mbili kupitia mixx by yas halafu naambiwa sina salio la kutosha wakati nimeweka zaidi hiyo hela muda huo huo, alipokea muhudumu wa kike nilimfokea yule dada (niliongea nae kwa sauti ya jazba kwani ile dhana ya yas ni mtandao mbovu kweny ehuduma ishanijia kichwani) akanambia kwamba haoni tatizo kwenye account yangu labda nijaribu tena.
Nilipo jaribu tena ndiyo nikagundua kumbe nilikuwa naandika elfu ishirini (20000) badala ya elfu mbili (2000)
Kwahiyo naungana na wadau wengine hapo juu wanaosema huenda kuna namba unaikosea kutokana na kukwangua vocha vibaya ama kwa namna nyingine, kwa sababu kuna muda unajihisi unafanya kitu kwa usahihi kabisa kumbe kuna mahali unakosea