Inakuwaje unanunua vocha ya simu (scratch card) unaingiza namba kwa usahihi kabisa unaambiwa namba ya vocha uliyoingiza haipo?

kama vocha umeikwangua mwenyewe na ikakujibu hivyo basi lazima kuna namba umeikosea kuingiza mfano 6 unaweza kuweka 0 au 8, au kwenye 3 ukaweka 9,namba 1 ukaingiza 7 na hii itategemea hiyo vocha umeikwangua vp labda lile tabaka la juu linaloficha namba hukulimalizia vizuri ndoapo kwenye 1 ukaweka 7 au kwenye 6 ukaweka 0..kuliko kuitupa vocha kama ulivyosema ni bora umpe mtu akusomee upya au akuandikie
🌤️🙋‍♂️✍️🎯👌👍👏👊🤝🙏
 
Kuna siku niliwapigia yas huduma kwa wateja baada ya kuwa nanunua kifurushi cha intaneti cha elfu mbili kupitia mixx by yas halafu naambiwa sina salio la kutosha wakati nimeweka zaidi hiyo hela muda huo huo, alipokea muhudumu wa kike nilimfokea yule dada (niliongea nae kwa sauti ya jazba kwani ile dhana ya yas ni mtandao mbovu kweny ehuduma ishanijia kichwani) akanambia kwamba haoni tatizo kwenye account yangu labda nijaribu tena.

Nilipo jaribu tena ndiyo nikagundua kumbe nilikuwa naandika elfu ishirini (20000) badala ya elfu mbili (2000)

Kwahiyo naungana na wadau wengine hapo juu wanaosema huenda kuna namba unaikosea kutokana na kukwangua vocha vibaya ama kwa namna nyingine, kwa sababu kuna muda unajihisi unafanya kitu kwa usahihi kabisa kumbe kuna mahali unakosea
Duh, ukamfokea dada wawatu bure
 
Vocha hutoka kwa mfumo wa batch
Yawezekana iyo batch haikua activated ndo maana hukuweza itumia Kuna mchangiaji amesema aliwahi jaribu vocha ikamgomea baada ya week ndo ika kubali kwa hiyo ishu hapo ni activation ya batch husika haikua ime fanyika watu wa mfumo Wana lielewa vzuri hili
Cc. Vodacom Tanzania
 
Hili limeshanitokea mara kadhaa matokeo yake naishia kutupa vocha na kuweka nyingine. Siku hizi huwa sinunui sana vocha za kukwangua nanunua tu bando kwa mtandao.

Leo nimekuta vocha ambazo nilikuwa nimenunua kitambo na huwa mara nyingi inakuwa kwa ajili ya msichana wa kazi.

Nikataka kuingiza vocha moja inasema vocha haipo. Nikarudia tena mara mbili jibu ni lile lile. Hii inakuwaje?
Dah nimekumbuka mbali sana miaka ya nyuma wakati niko chuo Dar nilikuwaga napiga sana vocha za watu kwenye daladala hasa kama nakuwa nimesimama alafu anayeweka vocha amekaa. Nilikuwa nikiona mtu anatoa vocha na kuanza kukwangua mimi naweka simu yangu tayari. AKISHAMALIZA TU ile anatoa simu yake mimi tayari naanza kuingiza namba na kuikubali yeye akijakumaliza simu inamwambia vocha unayojaribu kuingiza imeshatumika. Duh uhuni mwingine siyo mzuri kabisa.
 
Kuna siku niliwapigia yas huduma kwa wateja baada ya kuwa nanunua kifurushi cha intaneti cha elfu mbili kupitia mixx by yas halafu naambiwa sina salio la kutosha wakati nimeweka zaidi hiyo hela muda huo huo, alipokea muhudumu wa kike nilimfokea yule dada (niliongea nae kwa sauti ya jazba kwani ile dhana ya yas ni mtandao mbovu kweny ehuduma ishanijia kichwani) akanambia kwamba haoni tatizo kwenye account yangu labda nijaribu tena.

Nilipo jaribu tena ndiyo nikagundua kumbe nilikua naandika elfu ishirini (20000) badala ya elfu mbili (2000)

Kwahiyo naungana na wadau wengine hapo juu wanaosema huenda kuna namba unaikosea kutokana na kukwangua vocha vibaya ama kwa namna nyingine, kwa sababu kuna muda unajihisi unafanya kitu kwa usahihi kabisa kumbe kuna mahali unakosea
Ulifanya vizuri sana kujiita Kijana masikini
 
kama vocha umeikwangua mwenyewe na ikakujibu hivyo basi lazima kuna namba umeikosea kuingiza mfano 6 unaweza kuweka 0 au 8, au kwenye 3 ukaweka 9,namba 1 ukaingiza 7 na hii itategemea hiyo vocha umeikwangua vp labda lile tabaka la juu linaloficha namba hukulimalizia vizuri ndoapo kwenye 1 ukaweka 7 au kwenye 6 ukaweka 0..kuliko kuitupa vocha kama ulivyosema ni bora umpe mtu akusomee upya au akuandikie
Aisee kuweka salio kwa vicha, duu kitambo kweli sijatumia hii huduma.
 
Dah nimekumbuka mbali sana miaka ya nyuma wakati niko chuo Dar nilikuwaga napiga sana vocha za watu kwenye daladala hasa kama nakuwa nimesimama alafu anayeweka vocha amekaa. Nilikuwa nikiona mtu anatoa vocha na kuanza kukwangua mimi naweka simu yangu tayari. AKISHAMALIZA TU ile anatoa simu yake mimi tayari naanza kuingiza namba na kuikubali yeye akijakumaliza simu inamwambia vocha unayojaribu kuingiza imeshatumika. Duh uhuni mwingine siyo mzuri kabisa.
Aisee utakuwa uliniibia mimi tafadhali nirudishie! Niliibiwa kwa mtindo huo natoka Sinza kwenda Posta! Ilikuwa ya elfu tano wakati ule tulikuwa tunaita dola tano😆
 
Vocha hutoka kwa mfumo wa batch
Yawezekana iyo batch haikua activated ndo maana hukuweza itumia Kuna mchangiaji amesema aliwahi jaribu vocha ikamgomea baada ya week ndo ika kubali kwa hiyo ishu hapo ni activation ya batch husika haikua ime fanyika watu wa mfumo Wana lielewa vzuri hili
Cc. Vodacom Tanzania
Asante kwa elimu hiyo. Japo hii vocha niliinunua zaidi ya wiki kabla ya kuikwangua wacha ikae hata mwezi nitaijaribu tena
 
Back
Top Bottom