Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kazimia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kazimia
Kumbe mtumbuaji alitumbuliwa? We jamaa shetani anakuona ujue!Kiboko yao ni Nangungu mkoani Lindi tafuta kwenye YouTube gesi asilia aliyofukiziwa Mwendazake kabla hajatumbuliwa
Mwaka 2012 nilienda huko na kikundi fulani tulikuwa tunahubiri injili kule Sakura na maeneo yote ya kipumbwi pale kwenye majahazi ya kwenda Zanzibar.Nilikua nasikiliza wimbo wa Utaonaje by Billnass, nasikia humo ndani anatuhamasisha wasikilizaji wake kwa kusema
"Ukitaka kuroga nenda Pangani."
nimeishi Korogwe kwa Maji Marefu nimejionea uchawi wa kila aina. Ila kwa sasa Inaonekana huko pangani Tanga kuna mambo mazito.
Copy to Mshana Jr BIN NUN Maya Angelou na wengine wote
Damu ya Kristo Yesu inanguvu..Mwaka 2012 nilienda huko na kikundi fulani tulikuwa tunahubiri injili kule Sakura na maeneo yote ya kipumbwi pale kwenye majahazi ya kwenda Zanzibar.
Pia tulijitolea kufundisha katika shule ya kipumbwi secondary. Aisee wale watoto asilimia tisini wamevalishwa hirizi (tulifahamu siku ya ijumaa maana tulipoamua kuimba kidogo ili tufanye maombi ya shukrani kabla ya kuondoka watoto karibu shule nzima walilipuka mapepo). Wale hawakuwa na utulivu darasani, yaani hawawezi kukaa kimya. Ni kama kuna nguvu fulani inawatawala.
Siku ya kwanza kwenye mkutano wetu wa injili uwanjani waganga (ambao ni masheikh) walikuja na zile tanbihi wanazunguka pale wakitamka maneno yao. Tukaanza kuomba Mungu atupe ushindi ili waondoke na ikiwezekana wampokee Yesu.
Kesho yake hawakuja na tukapewa taarifa kwamba wameondoka pale kijijini. Basi tukiwa na moto hasa tukapeleleza na kujua makazi yao na vilinge tukaenda kuwasha moto wa kiroho huko. Yaliyotokea baada ya pale ni historia.