Mwaka 2012 nilienda huko na kikundi fulani tulikuwa tunahubiri injili kule Sakura na maeneo yote ya kipumbwi pale kwenye majahazi ya kwenda Zanzibar.
Pia tulijitolea kufundisha katika shule ya kipumbwi secondary. Aisee wale watoto asilimia tisini wamevalishwa hirizi (tulifahamu siku ya ijumaa maana tulipoamua kuimba kidogo ili tufanye maombi ya shukrani kabla ya kuondoka watoto karibu shule nzima walilipuka mapepo). Wale hawakuwa na utulivu darasani, yaani hawawezi kukaa kimya. Ni kama kuna nguvu fulani inawatawala.
Siku ya kwanza kwenye mkutano wetu wa injili uwanjani waganga (ambao ni masheikh) walikuja na zile tanbihi wanazunguka pale wakitamka maneno yao. Tukaanza kuomba Mungu atupe ushindi ili waondoke na ikiwezekana wampokee Yesu.
Kesho yake hawakuja na tukapewa taarifa kwamba wameondoka pale kijijini. Basi tukiwa na moto hasa tukapeleleza na kujua makazi yao na vilinge tukaenda kuwasha moto wa kiroho huko. Yaliyotokea baada ya pale ni historia.