Inaonekana Sabaya anataka kuzama na Mbowe

Inaonekana Sabaya anataka kuzama na Mbowe

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
20,189
Reaction score
29,663
Katika ushahidi wake leo, aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya ameendelea kudai kuwa Kuna watu walinipanga kuja kumuua. Ikumbukwe hata kesi iliyopita ya unyanganyi kwa kutumia silaha, Sabaya kwenye ushahidi wake alidai Kuna watu walipanga kumuua na amewahi kujificha na familia yake.

Swali la kujiuliza Ni kwanini Sabaya amerudia Mara ya pili kwenye ushahidi wake kudai kwamba kulikuwa na kundi lilipanga kumuua? Kuna Mambo matatu ya kutazama.

1. Ukijaribu kuangalia ushahidi wa Sabaya unalenga mwishoni kwenye kundi Fulani la watu waliotaka kumuua. Na ikumbukwe Kuna kesi ya ugaidi dhidi ya Mh Mbowe na wenzake ambayo kwenye mashtaka inadai watuhumiwa walipanga kuwadhuru Viongozi, hasa Sabaya. So Sabaya anajaribu kuomba symphathy ya dola dhidi ya watuhumiwa. Hivyo anatumia nguvu kubwa sio kujitetea Bali kutaka kuonesha jinsi akina Mbowe walivyotarajia kumuua.

2. Ni Kama Sabaya ameshakata tamaa na kesi kwa hivyo anajua anaweza kupatikana na hatia na kufungwa hivyo ameamua kutumia ushahidi wake kukazia kuwa Ni kweli kina Mh Mbowe walipanga kumuua. Hivyo kwenye ushahidi wake lazima ataje mipango ya kumuua Kama njia ya kudhibitisha kwamba kina Mh Mbowe kweli wanahusika na mashtaka ya ugaidi.

3. Sabaya anajitetea kuwa amenusurika kuuawa kwenye ushahidi wake Mara mbili Kama njia ya kuwakumbusha wenye madaraka na dhamana kwamba Kama mtanifunga na mbowe mumfunge. Yani Ni Kama anapiga kelele kwmba Mbowe alitaka kumuua hivyo itakuwa unfair kama ataachwa huru Halafu yet afungwe.

Hivyo, Sabaya kurudia rudia kudai Kuna watu waliotaka kumuua, Ni njia ya kutaka kuzama na mbowe kwenye maji wafe wote. Cha msingi Ni kusubiri muda utatuambia Nini. Je watazama wote au mmoja atazama.
 
Nikifatilia global tv kesi ya sabaya inaonekana imetaka tu ifunge lakini ile kesi wanansheria wa serikali pamoja na mashahidi wa serikali ni wepesi kama karatasi!

Hakuna la maana ambalo unaweza kusema kweli jamaa alihusika direct sehemu hii! Anaemtuhumu Sabaya kuwa alimpa rushwa ya milion 90 yupo nje analanda wakati anajinasibu alimpa milion 90 ili asimkate kwa kosa la kukwepa kodi.

Alipoulizwa askari ambae ni shahidi kuwa huyo mtu mmemkata? Akajibu hapana! Kwanini hamjakmata wakati amekwepa kodi? Kimyaaa! Sawa njoo kwenye footage za cctv camera yani hakuna sura ya mtu inayoenekana lakini wanaipeleka mahakaman kama ndiyo ushahidi wao.
 
Huyu mujamaa anatapatapa, anaweza kusema hivyo wala hakuna anayemzuia, akimaliza hayo athibitishe juu ya hao waliokuwa wanataka kumuua, Mbowe ni jabali, jiwe kuu ambalo wenye hofu wanaogopa hata kulitamka jina lake.

Sabaya apambane na tuhuma zake, anatakiwa ajue huu ndio muda wa kula mavuno yake.
 
Sabaya kwa sasa ni kama mtu aliyechukuliwa na maji ya mto uliofurika, anajitahidi ku grab kila kitu karibu yake kujiokoa...
 
Nanukuu “walijaribu kuwadhuru viongozi”,sabaya hakuwa kiongozi yule ni aina ya vibaka wale wa Manzese ya zamani waliokuwa wanajikusanya kwa makundi na kuwatisha wenye mali zao na viwembe ili wawaibie.

Tofauti yao mmoja aliteuliwa na mwanasiasa wengine walikuwa wanajipa wao madaraka so unapojaribu ku-mention viongozi hawa vibaka watoe,hata humo CCM most of them ni wezi tu.
 
Akina Kingai wamesema hawakumpa taarifa Sabaya wala JWTZ wala TISS juu ya mipango ya kigaidi ya Mbowe.

Sasa kama Sabaya alikuwa anajificha akihofia kuwa kuna watu wanataka kumuua, basi lilikuwa ni wenge lake tu la kijambazi. Atulie anyolewe, jinai haifi. Mkolomije naye akae mguu sawa huko aliko.
 
Sabaya anatapatapa Maji yapo Shingoni kumbuka kwanza alisema anatumwa na Aliyemteua Waziri wa Fedha haikumsaidia,Leo anawakana wenzake 5 na Wale Siku ya kujitetea Watamtaja.
 
Akina Kingai wamesema hawakumpa taarifa Sabaya wala JWTZ wala TISS juu ya mipango ya kigaidi ya Mbowe.

Sasa kama Sabaya alikuwa anajificha akihofia kuwa kuna watu wanataka kumuua, basi lilikuwa ni wenge lake tu la kijambazi. Atulie anyolewe, jinai haifi. Mkolomije naye akae mguu sawa huko aliko.
Amefanya ujambazi , amepora mali na pesa za wafanya biashara, alitaka wamchekee.
Sabaya ni wakumfukia akiwa hai.
 
Nikifatilia global tv kesi ya sabaya inaonekana imetaka tu ifunge lakini ile kesi wanansheria wa serikali pamoja na mashahidi wa serikali ni wepesi kama karatasi! Hakuna...
Kwa ushahidi wote huo tena wa wazi, hivyo bado una mashaka!!yule hakuwa mkwepa kodi, sasa akamatwe vipi?bali alitishiwa kama ilikvyokuwa desturi ya ujambazi wa awamu ya 5!!

Basi tufanye hivi hii case ameshinda, aendelea kutumikia ile 30 ya kule!!!jamaa alikuwa jambazi na mwenzake sasa nao kaishaingia kwenye radar , naye muda wowote kilio kinaanza!!!ila maisha haya wakati mwingine bora ubakie mkulima tu, kuliko haya ya ulikuwa field marshal/General unakuja kuwa chini ya Nyampala!!hapanaa
 
Unamanisha ni kweli Mbowe alitaka kumuua Sabaya...?
 
Kwa ushahidi wote huo tena wa wazi, hivyo bado una mashaka!!yule hakuwa mkwepa kodi, sasa akamatwe vipi?bali alitishiwa kama ilikvyokuwa desturi ya ujambazi wa awamu ya 5!...
Pale hakuna ushahidi ulionyooka ni magumashi tu nakuambia! Wanaletwa mashahidi toka Dar shahidi wa msingi yuko Arusha palepale anaachwa!

Tena Derava wake ambae kwavyovyote alikuwanae siku ga tukio wanaodai walikuwa wote Arusha nje kituo cha kazi na gari la Serikali tena bila kibali cha mkuu wa kazi
 
Nikifatilia global tv kesi ya sabaya inaonekana imetaka tu ifunge lakini ile kesi wanansheria wa serikali pamoja na mashahidi wa serikali ni wepesi kama karatasi! Hakuna ...
Sabaya hatoboi, lazima atandikwe mvua zingine
 
Back
Top Bottom