Inaonesha sababu ya Putin kuishambulia Ukraine si kujiunga NATO

kagoshima

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2015
Posts
2,887
Reaction score
5,687
Baada ya Finland na Sweden ku apply kujiunga NATO tulitegemea Putin aje na vitisho vile vile dhidi ya ukrain, lakini kanywea. Kwanini?

Putin ni mtu muongo muongo sana. Putin anaitamani ukrain, angependa iunganishwe na Russia, ni vivyo hivyo kwa Moldova. Sababu ya kuingia kupiga mabomu ukrain eti kujiunga NATO imetumika tu ku-justify uvamizi.

Haya sasa kuna waliopeleka maombi rasmi mbona ka mute?
 
Huwezi amini atapata wakili wa kumtetea ,ningekuwa mwanasheria kesi Kama hizo sichukui hata Kama Kuna bilioni 100 mfukoni maana nitahahakisha anafungwa
duuh ni hatari yaani 22 kapita nao
 
Putin anataka itengeneza USSR halafu kati ya washirika wakubwa sana wenye kujiweza kiuchumi ambapo Putin asingemudu kumpoteza ni Ukraine.....imebidi atumie by force by power akilini anaamini Ukraine ni Urusi ndogo
 
Tulia awamu yao yakujikuta kama cremia bado.🚶
 
Yawezekana sababu haikuwa kujiunga NATO pekee
maana ukraine alishasema kuwa mpango wa kujiunga NATO
Ameshaachana nao lakin jamaa bado hawapo tayari kusitisha vita,
nadhani putin lengo lake nikuigawa ukraine,
 
Yawezekana sababu haikuwa kujiunga NATO pekee
maana ukraine alishasema kuwa mpango wa kujiunga NATO
Ameshaachana nao lakin jamaa bado hawapo tayari kusitisha vita,
nadhani putin lengo lake nikuigawa ukraine,
Ukrein alikuwa hasemi ukweli kwani kaweka msimamo huo mpaka ndani ya katiba yake.
 
Mbona Putin alishaweka wazi hizo sababu zake?

1. Kulinda watu wake huko donbas region waliokuwa wanashambuliwa na ukraine tangu 2014 70% [emoji736]️

2. Ku denazify ukraine, umeona hawa jamaa waliokubali yaishe Huko Azovstal Steel plant, hao jamaa ni Neo-Nazis, na ipo wazi baada ya kupambana sana na warusi wakaingizwa kwenye payroll na serikali ya ukraine...70%[emoji736]️

3. Kupunguza fyoko fyoko za utawala wa ukraine kujiunga na NATO 100[emoji736]️

4. Preemptive military operation dhidi ya Ukraine na washawishi wake (NATO) Kuishambulia urusi (Crimea) ili kuirudisha chini ya ukraine. 80[emoji736]️

Hivi vyote vitakamilika kwa wakati.

Russia angeanza moja kwa moja operation yake pale donbas shughuli ingekuwa pevu sana, na asingefanikiwa, ila kawavuruga kweli kweli nchi nzima kisha karudi kwenye lengo lake kuu
 
Kuna mtaalamu mmoja aliwahi kusema,
Style ya kirusi kwenye negotiation table haijabadilika Toka enzi za Muscovy.

Wataanza na vitu vichache, mkishindwa kukubaliana.
Walianza na kutaka:
1) Ukraine wasijiunge NATO
2)Kuitambua Crimea kuwa sehemu ya Urusi.
3)Kuyapa autonomy majimbo ya Luhansk na Donetsk kifupi waunde Federation.
Mazungumzo yalifanyika Belarus

Ujue the second round wataongeza mahitaji, msipokubaliana
Angalia:
1) wasijiunge NATO
2)Kuitambua Crimea
3)kuyatambua majimbo yaliyo jitenga kuwa nchi huru.
4)Denazification
5)Kuirudisha lugha ya Kirusi kuwa lugha rasmi.

Third round Hali itazidi kuwa mbaya, hivyo ni Bora kulimaliza mnapoanza meza ya mazungumzo.
Wameongeza Sasa sio tu Luhansk na Donetsk, Sasa Kherison imeenda, Odessa itaenda yaani watapoteza eastern na south, kutokuwa na access ya bahari.

Sasa Vladimir Vladirmovich Putin anasema wanapigania ardhi yao ya asili, maana yake kuna possible ya huo upande kuja kuunganishwa na Urusi siku Moja.
 
Na Dunia itakuwa inamwangalia tu huyo Putin akijiongezea vijisababu vya kuichukua kwa nguvu Ukrain?
 
tupe kipengelee hlf urudi utuambie nan yupo juu ya katiba ya nchi jiran

Sent using Jamii Forums mobile app
Kipengere Cha kujiunga NATO kipo kwenye katiba ya ukrein na siyo Siri mkuu. Mtu kujilinda ni mhimu na ndiyo maana unajenga nyumba unaweza nondo na mageti Ili ujihakikishie usalama wako huku Kuna polis wanakulinda.
 
So mkuu unataka kusema Putin ni muongo muongo kama Jiwe? [emoji848]
 
Huwezi amini atapata wakili wa kumtetea ,ningekuwa mwanasheria kesi Kama hizo sichukui hata Kama Kuna bilioni 100 mfukoni maana nitahahakisha anafungwa
Naye Ashughulikiwe!
[emoji1484][emoji1484]
[ Kumbukumbu la Torati 19
21 Wala jicho lako lisiwe na huruma; uzima kwa uzima, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.

وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

[ AL - BAQARA - 179 ]
Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili msalimike.
 
Huwezi amini atapata wakili wa kumtetea ,ningekuwa mwanasheria kesi Kama hizo sichukui hata Kama Kuna bilioni 100 mfukoni maana nitahahakisha anafungwa
... ni haki yake kupata wakili wa kumtetea. Pili hayo ni madai tu, until proven guilty by the court ndio hapo unaweza kumwona mbaya; ila kwa sasa hivi ana haki zote including kupata wakili wa kumtetea.
 
Jiulize, kwa nini hao Sweden na Finland wametoa tamko kipaindi hiki cha urusi kuishambulia ukrane?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…