Kuhusu kukosea kosea kwa maneno kunazidi kuongezeka kwa Mheshimiwa Rais wetu. Wkt akihojiwa na BBC aliongea kuwa wenzake Mbowe walishafungwa na ilikuwa inasubiriwa Mbowe tu arudi kutoka ughaibuni naye afungwe!
Ninavyojua mimi kwa mtu asiyeelewa (yaan layman) hata kupelekwa mahakamani ni sawa na kufungwa. Kwa maana hiyo usahihi kwa wakati huo wasiadizi wa Rais walipaswa kuwa wameshaeleza kwa ufasaha kuwa Mbowe alikuwa anasubiriwa akirudi afikishwe mahakamani kujibu tuhuma zake na sio kufungwa kama alivyoeleweka Rais wakati huo.
Leo pia kwa kujua kuwa suala la Mbowe lingejitokeza mkutanoni Rais alipaswa kuwekwa vema kuwa iwapo angegusia issue ya msamaha angeweka "caveat" kuwa iwapo mahakama itamwona Mbowe ana hatia basi masuala ya msamaha wa Rais yataangaliwa huko mbeleni. Au angeelekeza tu kwa DPP kuwa iwapo inaonekana kesi ya Mbowe haina maslahi kwa umoja wa Taifa letu basi aangalie namna ya kuachana nayo
Ukitafakari kwa kina maana anayokuwa amekusudia kuiongea Mh. Rais inatofautiana sana na maneno ambayo humtoka na hivyo badala yake kuzaa minong'onon mingi ambayo kwa kiasi inasumbua sana.
Ukweli wasaidizi wa Mh.Rais kwa upande wa Sheria na hotuba probably hawajajipanga vizuri na kumsababishia kutoeleweka vizuri na WaTanzania na dunia inayofuatilia siasa zetu.
Ushauri - Rais aangalie namna ya kubadili wasaidizi wake upande wa Hotuba na hata Sheria. Hawa watazidi kumharibia sana kadri siku zinavyosonga mbele!
Ni hayo tu.
Mod. ninaomba usiunganishe au kufuta uzi huu kwani umebeba ujumbe wa kipekee!