Inaonesha Wasaidizi wa Rais hawako makini kivile!

Inaonesha Wasaidizi wa Rais hawako makini kivile!

Kusameheana kupo na inawezekana iwapo mama akiamua kumwambia DPP kesi aachane nayo kwa maslahi mapana ya taifa.
 
Hudhani kwa ni Mara ya kwanza kukosea? Umesahau juzintu kwenye ile hotuba yake kwa taifa alisema kabla ya Uhuru tulikua hatuna shule za binafsi.
Mfumo wa vyama vingi ulianza 1995
Ila hata Kama wanaoandika hotuba wanakosea, Ina maana yeye haoni hayo makosa?

Yeye ni kama mwenzake aliesema sadam wa kuwait
 
sio kwa nia mbaya ila ni mzanzibar, uzanzibar wake una athiri uongeaji pia mfano juzi anasema polisi wanaweka ma bichwa yao kwenye gari
hivo basi haitotokea siku azungumze kama tunavotegemea
Usilete hoja nyepesi kwenye masuala nyeti dogo
 
sijawahi kumsikia akisema hivo,ila kama kweli alisema hivi huwezi kumrekebisha kwenye haya maana ni jambo ambalo alipaswa kulijua huko shuleni kwamba zilikuwepo hizo shule
Ina maana hukufatilia hotuba ya raisi alipokua akihutubia taifa?
 
Kitu..kikubwa kwa mtu uliezoea kusmamia ukweli huwezi kuuishi uongo, hichi ndicho kinatokea hapa.Ile kesi inaleta kigugumizi sana Mama hawezi kusema fulani ama kundi fulani limempotosha ndy anajikuta indirectly anasema maneno tofauti tofauti. Mtoa mada kuusimamia uongo lazma uwe na kipaji cha Uongo!Mi niko na mama...Uongo sio kipaji chake..Kesi ni ghalasa na sasa ifuutwe basi!!Tanzania ni ya wote, na wote ni yeye,wewe, yule, Freeman na mimi!!
 
Mama nahisi ana ishu personal na Mbowe, kila akitajiwa kuhusu Mbowe huwa anapaniki sana na anajikuta anaropoka mambo yasiyo ya msingi.

Nadhani ni zaidi ya tunayoyajua kuhusu mama na uhusika wake kwa hii kesi ya Mbowe.

Kuhusu msamaha mwenyewe kwanza nimemshangaa yeye kusema anaweza kusamehe, sasa Mbowe bado hajahukumiwa yeye mam anawezaje kusamehe kama sio yeye ndio ameishikilia hii kesi??

Rais anaweza kusamehe mtu endapo atakutwa na hatia mahakamani, lakini mtu ambaye bado ni mtuhumiwa nadhani mtu mwenye mamlaka ya kuondoa kesi ni DPP, naelewa anapisema "anaweza kumsamehe" alimaanisha anaweza kumpa maelekezo DPP asiendelee na kesi waifunge Mahakamani which means Mbowe atakuwa Freeman kama jina lake Ila mama hakupaswa kutumia lugha za namna hiyo Kama kweli yeye Hana personal interest na hiyo kesi.

There is more into it tutakuja kujua ukweli tu.
Kwani Rais kasema atasamehe bila mtu kuhukumiwa? Na je kama atatoa maelezo kwa DPP?

Acheni ujinga ,Mbowe kaelezwa wazi aache dharau na kuleta chokochoko Nchini.
 
Rais Samia alikwishakiri kuwa alifeli fomu IV. Na yule mwingine aliyetangulia alishindwa kwenda full combination (PCM, nk) akaishia half-combi (CM) Mkwawa. Hivi kwa nini ni vigumu kupata Rais smart kama Mkapa, Nyerere? Hawa CCM sijui huwa wanachaguana kwa vigezo gani tu!!
 
hata kuhusu ndege hawakusema wakati wakupata uhuru tulikua na ndege ngapi'
 
Kuhusu kukosea kosea kwa maneno kunazidi kuongezeka kwa Mheshimiwa Rais wetu. Wkt akihojiwa na BBC aliongea kuwa wenzake Mbowe walishafungwa na ilikuwa inasubiriwa Mbowe tu arudi kutoka ughaibuni naye afungwe!

Ninavyojua mimi kwa mtu asiyeelewa (yaan layman) hata kupelekwa mahakamani ni sawa na kufungwa. Kwa maana hiyo usahihi kwa wakati huo wasiadizi wa Rais walipaswa kuwa wameshaeleza kwa ufasaha kuwa Mbowe alikuwa anasubiriwa akirudi afikishwe mahakamani kujibu tuhuma zake na sio kufungwa kama alivyoeleweka Rais wakati huo.

Leo pia kwa kujua kuwa suala la Mbowe lingejitokeza mkutanoni Rais alipaswa kuwekwa vema kuwa iwapo angegusia issue ya msamaha angeweka "caveat" kuwa iwapo mahakama itamwona Mbowe ana hatia basi masuala ya msamaha wa Rais yataangaliwa huko mbeleni. Au angeelekeza tu kwa DPP kuwa iwapo inaonekana kesi ya Mbowe haina maslahi kwa umoja wa Taifa letu basi aangalie namna ya kuachana nayo

Ukitafakari kwa kina maana anayokuwa amekusudia kuiongea Mh. Rais inatofautiana sana na maneno ambayo humtoka na hivyo badala yake kuzaa minong'onon mingi ambayo kwa kiasi inasumbua sana.

Ukweli wasaidizi wa Mh.Rais kwa upande wa Sheria na hotuba probably hawajajipanga vizuri na kumsababishia kutoeleweka vizuri na WaTanzania na dunia inayofuatilia siasa zetu.

Ushauri - Rais aangalie namna ya kubadili wasaidizi wake upande wa Hotuba na hata Sheria. Hawa watazidi kumharibia sana kadri siku zinavyosonga mbele!

Ni hayo tu.

Mod. ninaomba usiunganishe au kufuta uzi huu kwani umebeba ujumbe wa kipekee!
Yeye alishatoa hukumu, na leo kakazia sasa sijui kama wateule wake wataweza kwenda kinyume nae
 
Back
Top Bottom