Inaonyesha Haji Mnoga alichezea U 17 ya Uingereza na sasa Taifa Star

Inaonyesha Haji Mnoga alichezea U 17 ya Uingereza na sasa Taifa Star

Muite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
2,971
Reaction score
6,607
Wataalam naombeni kujua kuhusu hili, maana amezaliwa England kwa Mama Mzungu na Baba Mtanzania wa Zanzibar.

Kwenye timu ya England U 17 amecheza pia. Na sasa ni kati ya mabeki wetu wa kutegemewa Taifa Star.

Je, mchakato wa uraia wake upoje?

Nikiri nimechelewa kulijua hili.

PIA NAOMBENI MAJIBU YASIYO NA MATUSI MAANA MTANZANIA UKIOMBA KUJUA JAMBO UTAONA ATAKACHOJIBIWA HADI AKOME
 
Kuhusu kuchezea hizi timu za under 17 na under 20 hakuna kikwazo kwa wachezaji kwa taifa atakalohitaji kutumikia. Lkn ukicheza timu ya wakubwa ya taifa fulan huwez jucheza timu yeyote dunian hivyo huyu mchezaji alikuwa bado na option either achezee england or tanzania na kwavile amevaa jezi ya tz ya wakubwa kamwe hatochezea england maana yake ameopt kuchezea tanzania
 
Umesema mzazi wake mmoja ni Mtanzania na mwingine anatoka kile kisiwa Cha Uingereza?

Kama ni hivyo akiwa chini ya miaka 18 basi Mnoga atakuwa na Uraia pacha yaani ni Mtanzania na Muingereza kwa wakati mmoja.

Hivyo alikuwa na haki ya kucheza Uingereza au Tanzania under nini huko.

Akifikisha miaka 18 atachagua uraia anaoutaka either apewe Utz au Ubrtish

Ila mpaka Sasa jibu unalo ameshachagua uraia Gani?
 
Hili suala la Uraia pacha serikali ichukue maamuzi magumu ilikubali sambamba na kuifanya bandari zetu kuwa duty free.

Haiwezekani, unakomaa na lisheria ambapo baadhi ya watu unatambua kuwa Wana uraia pacha unawatambua kama Watanzania ila wengine unasema unawapa hadhi maalumu

Wawe wazi kama kanisa Katoliki ambao Pombe, kitimoto wameruhusu na wanavibariki kama vyakula na bado wapo poa tuu hakuna tatizo lolote, tofauti na wale machoni pa watu wanakomaa kuwa ni haramu lakini wakiwa chobinga wanamwagilia Moyo kwa pombe na kujenga afya kwa mdudu huku wakijua Mungu wanayemdanganya anawaona
 
Na uhakika ana uraia wa UK ila nataka kukwambia tu ukweli ni ile hali serikali na kigugumzi kuhusu uraia pacha ila hata viongozi wengi tu wana pass mbili na hata wafanya biashara. Tukishikilia sheria kwa nguvu wengi tutasafirisha ila tunajuwa sheria sio kwa wote, inachagua.. Mimi binafsi sina shida nakuwa na uraia pacha ni kuweka masharti tu basi lakini sina shida nayo.
 
Ndiyo maana BBC ina hasira na sisi! BBC haitambui kuwa Tanzania tumefuzu...ona maandishi Yao.
===
Saturday's three qualifiers join Algeria, Burkina Faso, Cape Verde, Egypt, Equatorial Guinea, Guinea, Guinea Bissau, Mali, Mozambique, Morocco, Nigeria, Senegal, South Africa, Tunisia and Zambia at the finals alongside Ivory Coast, who qualified automatically as hosts.
 
Hatuna huo uwezo na tekinolojia ya kutrack watu hao.
 
Hili suala la Uraia pacha serikali ichukue maamuzi magumu ilikubali sambamba na kuifanya bandari zetu kuwa duty free.

Haiwezekani, unakomaa na lisheria ambapo baadhi ya watu unatambua kuwa Wana uraia pacha unawatambua kama Watanzania ila wengine unasema unawapa hadhi maalumu

Wawe wazi kama kanisa Katoliki ambao Pombe, kitimoto wameruhusu na wanavibariki kama vyakula na bado wapo poa tuu hakuna tatizo lolote, tofauti na wale machoni pa watu wanakomaa kuwa ni haramu lakini wakiwa chobinga wanamwagilia Moyo kwa pombe na kujenga afya kwa mdudu huku wakijua Mungu wanayemdanganya anawaona
Aahaaaa,eti chobingo
 
Ndiyo maana BBC ina hasira na sisi! BBC haitambui kuwa Tanzania tumefuzu...ona maandishi Yao.
===
Saturday's three qualifiers join Algeria, Burkina Faso, Cape Verde, Egypt, Equatorial Guinea, Guinea, Guinea Bissau, Mali, Mozambique, Morocco, Nigeria, Senegal, South Africa, Tunisia and Zambia at the finals alongside Ivory Coast, who qualified automatically as hosts.
Aisee nilisoma hii asubuhi nikabaki ninawashangaa kama wana football editor. Konyo sana hawa.
 
Hilo lisikusumbue ishu kubwa endapo angechezea timu ya taifa ya wakubwa
 
Kuhusu kuchezea hizi timu za under 17 na under 20 hakuna kikwazo kwa wachezaji kwa taifa atakalohitaji kutumikia. Lkn ukicheza timu ya wakubwa ya taifa fulan huwez jucheza timu yeyote dunian hivyo huyu mchezaji alikuwa bado na option either achezee england or tanzania na kwavile amevaa jezi ya tz ya wakubwa kamwe hatochezea england maana yake ameopt kuchezea tanzania
Amebug pa kubwa
 
Sio kweli diego costa kacheza Brazil ya wakubwa kombe la mabara baadae akachukua uraia wa spain kacheza
Wachezaji kama
Larpote kacheza France kaenda Spain
Zaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hakuna madhara yeyote tutakayoyapata tukiingia uraia wa nchi mbili, ,una opportunities nyingi sana watanzania wanazikosa duniani kwasababu ya uraia pacha hakuna na nchi ina kosa vitu vingi kwasababu hiyo. tunatakiwa kulivalia njuga hadi viongozi wetu waelewe. shida ni kwamba, majority ya wote wanaoupinga, including baadhi ya viongozi, ni washamba na exposure kwao ni ndogo. ati utahatarisha usalama wa nchi kwa kuwa na uraia pacha?

chukua mfano, kenya,ghana, nigeria, rwanda, uingereza, israel, marekani na nchi zengine kibao, zina uraia pacha, wamedhurika nini?jifunze kwa wakenya tu hapo uraia pacha umewadhuru nini? protectionism ya watanzania ndio inaturudisha nyuma na watu wanafikia hatua wanaona kuwa watanzania ni mzigo. nchi wanaipenda lakini unakuwa mzigo mkubwa kuubeba. hivi mtu akitaka kuja kuidhuru Tanzania, anahitaji kutumia waraia pacha kweli? wakati akikaa tu marekani au ulaya kwa kutumia hizo simu tu mnazonunua, mitandao ya kijamii mnayotumia, au hata kuhack internet hata ya taifa lenu lote akajua kila kitu hadi chooni mmeenda saa ngapi anajua. nchi nzima tupo kiganjani mwa mzungu, google earth tu hapo hii ya kawaida ambayo ni ya raia unaweza kuona hadi mtaa na kuamua ukapige wapi au ukafanye nini hata kama haujawahi kufika tz. sembuse mitambo kibao ya kiulinzi ambayo hawajadisclose? ati unaogopa uraia pacha, imetusaidia nini? mambo ya sera z aujamaa/urusi zitatutoka lini?

halafu, uzalendo hauji kwa kuwa mtanzania, unaweza kuwa mtanzania pure ukaitosa nchi. chukua mfano, manyanyaso yanayofanywa kwa raia, umasikini, maisha magumu, manyanyaso ya ccm, kwani akija mto toka nje anataka information muhimu unafikiri hao mnaowaumiza moyo hawatawasaliti? mnafikiri hawajawasaliti? tena ni wazawa pure. si wanawapa mpunga tu, ukiwa na pesa unaweza kupata chochote kwa mzawa na asiye mzawa, viongozi wetu huu ukoko vichwani mwao sijui utakuja kuwatoka lini.
 
Wataalam naombeni kujua kuhusu hili, maana amezaliwa England kwa Mama Mzungu na Baba Mtanzania wa Zanzibar. Kwenye timu ya England U 17 amecheza pia. Na sasa ni kati ya mabeki wetu wa kutegemewa Taifa Star.

Je mchakato wa uraia wake upoje ??

Nikiri nimechelewa kulijua hili.

PIA NAOMBENI MAJIBU YASIYO NA MATUSI MAANA MTANZANIA UKIOMBA KUJUA JAMBO UTAONA ATAKACHOJIBIWA HADI AKOME
Kuchezea timu ya England under 17 hakumzuii kuchezea taifa lingine ambalo ni raia!! Kwa mujibu wa FIFA alikukuwa na haki ya kuchezea England kwa sababu alizaliwa England kwa hiyo ni muingereza kwa kuzaliwa. Lakini kwa kuwa baba yake ni Mtanzania, anaweza kuomba uraia wa Tanzania na kustahili kuchezea Taifa la Tanzania. Ila kama angechezea Timu ya wakubwa ya uingereza hata mara moja tu, hapo asingekuwa na haki ya kuchezea Timu ya Taifa ya nchi yoyote nyingine!! Hiyo ni mkwa mujibu wa FIFA. Mtu mmoja hawezi akachezea timu zaidi ya moja ya Taifa katika maisha yake!!
 
Sio kweli diego costa kacheza Brazil ya wakubwa kombe la mabara baadae akachukua uraia wa spain kacheza
Wachezaji kama
Larpote kacheza France kaenda Spain
Zaha

Sent using Jamii Forums mobile app
Unachosema siyo kweli!! Kwa mujibu wa kanuni za FIFA kuhusu uchezeaji wa timu za Taifa, MTU MMOJA HAWEZI KUCHEZEA ZAIDI YA NCHI MOJA KWENYE TIMU YA TAIFA YA WAKUBWA KATIKA MAISHA YAKE!! Kuchezea timu za under 17, 21 etc haimnyimi mtu kuchezea Taifa jingine!! Lakini kuanzia 2020, kanuni zilibadilika. Mtu anaweza kuchezea si zaidi ya mechi 3 kwenye timu ya Taifa ya Wakubwa akiwa na umri usiozidi miaka 21, na bado akaruhusiwa kuchezea Taifa jingine ambalo ana nasaba nalo kupitia mmoja wa wazazi wake!! Lakini mtu zaidi ya miaka 21 akicheza timu ya Taifa ya wakubwa mara moja tu, hawezi kuruhusiwa kuchezea timu nyingine!! Lakini hapa hatuzungumzii mechi za kirafiki au mechi za kufuzu (qualifiers)
 
Back
Top Bottom