political monger senior
JF-Expert Member
- Nov 26, 2020
- 1,827
- 5,994
Zipo taarifa kuwa wachezaji wa kigeni wa Tabora United wote wana vibali vya kazi, kilichokosekana ni vibali vya makazi lakini kwa sababu wana business visa, wanaruhusiwa kucheza kwa muda hadi pale vibali vyao vitakapotoka. Kwanini leo hawajaruhusiwa kucheza? Kuna tetesi kuwa kuna bifu zito kati ya Mtendaji wa Shirikisho na mmiliki wa Tabora United!
Je, ingekuwa ni Simba au Yanga wakawa na issue hii wangeachwa wacheze wakiwa nane au mechi ingeahirishwa? Sina majibu. Wacha tu niendelee kulewa.
Unadhani aliyeathirika na huu “Utoto” wa leo ni Tabora United tu kupoteza points? Hapana. Mpira wote umeumia. Imagine watu wa betting, waliosafiri kwa ajili ya mechi, kama Azam atakuwa bingwa kwa tofauti ya alama tatu mwisho wa msimu, kama Feisal atakuwa Mfungaji Bora kwa tofauti ya mabao matatu! Mpira wote umeumia!
Imagine kuna raia wa kigeni alikuwa anaitazama ligi yetu kwa mara ya kwanza, kuna mtu alikuwa anataka kutoa sponsorship kwa moja ya timu zetu. Sina nia ya kutetea tabora kwa sababu ya unyumbani, nataka tuitazame issue hii kwa ukubwa wake.
Tabora United wana utoto wao wamefanya kwenye hili lakini, utoto wao kuna namna umekuwa utoto wetu sote. Ligi yetu inaonekana bado ina mambo ya kitoto. Kuna mtu leo angeweza kushawishika kulipia king’amuzi cha mwezi, baada ya utoto wa pale Azam Complex ameghairi!
Anyway, Mfaransa mmoja wa kuitwa François-Marie Arouet aliwahi kusema common sense is not so common! Hivi mechi ingepelekwa mbele mngepata dhambi?