Inasemekana bifu zito kati ya Mtendaji wa Shirikisho na Mmiliki wa Tabora United ndio sababu ya kucheza pungufu

Inasemekana bifu zito kati ya Mtendaji wa Shirikisho na Mmiliki wa Tabora United ndio sababu ya kucheza pungufu

political monger senior

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2020
Posts
1,827
Reaction score
5,994
Zipo taarifa kuwa wachezaji wa kigeni wa Tabora United wote wana vibali vya kazi, kilichokosekana ni vibali vya makazi lakini kwa sababu wana business visa, wanaruhusiwa kucheza kwa muda hadi pale vibali vyao vitakapotoka. Kwanini leo hawajaruhusiwa kucheza? Kuna tetesi kuwa kuna bifu zito kati ya Mtendaji wa Shirikisho na mmiliki wa Tabora United!

Je, ingekuwa ni Simba au Yanga wakawa na issue hii wangeachwa wacheze wakiwa nane au mechi ingeahirishwa? Sina majibu. Wacha tu niendelee kulewa.

Unadhani aliyeathirika na huu “Utoto” wa leo ni Tabora United tu kupoteza points? Hapana. Mpira wote umeumia. Imagine watu wa betting, waliosafiri kwa ajili ya mechi, kama Azam atakuwa bingwa kwa tofauti ya alama tatu mwisho wa msimu, kama Feisal atakuwa Mfungaji Bora kwa tofauti ya mabao matatu! Mpira wote umeumia!

Imagine kuna raia wa kigeni alikuwa anaitazama ligi yetu kwa mara ya kwanza, kuna mtu alikuwa anataka kutoa sponsorship kwa moja ya timu zetu. Sina nia ya kutetea tabora kwa sababu ya unyumbani, nataka tuitazame issue hii kwa ukubwa wake.

Tabora United wana utoto wao wamefanya kwenye hili lakini, utoto wao kuna namna umekuwa utoto wetu sote. Ligi yetu inaonekana bado ina mambo ya kitoto. Kuna mtu leo angeweza kushawishika kulipia king’amuzi cha mwezi, baada ya utoto wa pale Azam Complex ameghairi!

Anyway, Mfaransa mmoja wa kuitwa François-Marie Arouet aliwahi kusema common sense is not so common! Hivi mechi ingepelekwa mbele mngepata dhambi?
 
Kwa tukio lililotokea jana kwenye Mchezo wa Ligi Kuu Azam FC Vs Tabora United NIMEUMIA sana nisiwe mnafki

Sio mm tu jamii yote ya Wapenda Soka imeumia kwa Utoto waliofanya Tabora United kuichafua ligi yetu, Ligi namba 5 kwa Ukubwa Afrika Mechi inachezwa kwa Dk 15 Aibu sana

TFF ni Baba wa Mpira wetu, na hivi Vilabu vyote ni watoto wake, Hivi mtoto akiunyea mkono unaukata? Tabora wameonesha utoto Tff walikua wanalijua hili mapema walishindwa nn kuhairisha Mechi kwa kutumia busara tu, Mbona kwa hizi Team kubwa busara hutumika sana au kwasababu Tabora United ni team ndogo?

Rejea tukio lililowakuta Simba Miaka miwili nyuma waliposafiri kwenda Kagera Wachezaji 12 kati ya 22 wakapata Mafua walibaki 10 wazima lakini Mechi ilihairishwa busara ilitumika!!! Why kwa jana imeshindikana??

Mchezo wa Yanga Vs Simba Miaka miwili nyuma ulihairishwa Kisa Muda tu kuleta changamoto mbona busara ilitumika ukapangiwa siku nyingine au kwasababu hawa ni Wakubwa!!

TFF sio nawalaumu ila mliweza kuzuia Aibu hii kuikumba ligi yetu lakini hamjafanya hivyo, Brand ya Ligi imechafuka walioichafua ni Tabora Utd na nyie Tff[emoji119]

Hongereni Azam FC kwa Ushindi, Hongera Feisal kwa Hattrick.
 
Nadhani walipanga haya matokeo ki KANUNI

Ndio unaeza sema kwa haraka haraka kuwa kilichotokea katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Azam FC na Tabora united FC ni UPANGAJI WA MATOKEO KI KANUNI ,ndio ni upangaji matokeo ,kwanini tunasema hivi ?

Kwanza kabla ya mechi huwa kuna Pre -Match Meeting ,hapa kuna kua na wahusika wote wa mchezo, Vilabu,TFF,waamuzi na Bodi ya ligi ,ina maana mpk kikao hiki kinafanyika ...Hawakuona hilo...lakini Kanuni pia inasema Wachezaji 8 hadi 7 wanaeza endelea na mchezo , lakini Kanuni hizo hizo kuna sehemu inasema wachezaji chini ya 7 mchezo hautoendeleea

Sasa basi kama Tabora United ilikua na wachezaji 8 tu,ina maana pre - match meeting walilliona hili hivyo wangeweza kutumia Kanuni kuhairisha huu mchezo ,lkn kwakua walishapanga wakaruhusu Tabora united apeleke timu uwanjani ,kilichotokea tumeona

Na kama Tabora United wasingepeleka timu ,Ki kanuni angepigwa Faini na kushushwa madaraja ya ligi ..hivyo na wao katumia kanuni kucheza 8 ,kisha wakatumia tena kanuni kuimaliza mechi wakiwa 6 .

Ni ujanja ujanja na uhuni tu wa kikanuni umetumika

NB: Ligi kuu Tanzania Bara ni namba 5 Kwa UBORA afrika

Credit
Kocha mkuu
 
Kuahirisha hii match kisa huruma ingekuwa kulea uzembe na kutowajibika kwa viongozi wa kitayose,
Walipewa siku 45 za kulipa pesa za wachezaji, wao hawakulipa, just imagine siku 45, wamefungiwa toka week iliyopita na bado hawajalipa, wamekuja lipa dakika ya mwisho, kisha wanataka huruma za TFF, hakuna kitu ka hicho,
Walichopata wanastahili
 
Kitayosa wamechemsha wenyewe kwa kutotoa taarifa mapema kuwa wachezaji wao ni wagonjwa wametoa taarifa uwanjani
 
Safi sana kito nimejizolea pesa ya bure kwenye beting zangu na ulibak wewe tu kitoyosesese sijui nn ok sasa kama kuna mwenye namba ya mmoja wa timu ya kitoyose anitumie nichangie timu mana wamefanya niwe na raha isiyo kifani
 
Nadhani walipanga haya matokeo ki KANUNI

Ndio unaeza sema kwa haraka haraka kuwa kilichotokea katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Azam FC na Tabora united FC ni UPANGAJI WA MATOKEO KI KANUNI ,ndio ni upangaji matokeo ,kwanini tunasema hivi ?

Kwanza kabla ya mechi huwa kuna Pre -Match Meeting ,hapa kuna kua na wahusika wote wa mchezo, Vilabu,TFF,waamuzi na Bodi ya ligi ,ina maana mpk kikao hiki kinafanyika ...Hawakuona hilo...lakini Kanuni pia inasema Wachezaji 8 hadi 7 wanaeza endelea na mchezo , lakini Kanuni hizo hizo kuna sehemu inasema wachezaji chini ya 7 mchezo hautoendeleea

Sasa basi kama Tabora United ilikua na wachezaji 8 tu,ina maana pre - match meeting walilliona hili hivyo wangeweza kutumia Kanuni kuhairisha huu mchezo ,lkn kwakua walishapanga wakaruhusu Tabora united apeleke timu uwanjani ,kilichotokea tumeona

Na kama Tabora United wasingepeleka timu ,Ki kanuni angepigwa Faini na kushushwa madaraja ya ligi ..hivyo na wao katumia kanuni kucheza 8 ,kisha wakatumia tena kanuni kuimaliza mechi wakiwa 6 .

Ni ujanja ujanja na uhuni tu wa kikanuni umetumika

NB: Ligi kuu Tanzania Bara ni namba 5 Kwa UBORA afrika

Credit
Kocha mkuu
Uko sahihi kiongozi. Ila mwenye uzi kakimbia. Baada ya kukulupuka n kutokujua sheria/ kanuni za soccer.
Asante
 
Uko sahihi kiongozi. Ila mwenye uzi kakimbia. Baada ya kukulupuka n kutokujua sheria/ kanuni za soccer.
Asante
Hahahaha,halafu zipo tu mtandaoni mtu anaeza zisoma vzr tu,akaacha kuwa mjinga mjinga
 
Binafsi nimeumia mno kitayose kucheza pungufu, TFF ijiangalie inakosesha ladha ya soka,

Raha ya timu ishinde kihalali
 
Hahahaha,halafu zipo tu mtandaoni mtu anaeza zisoma vzr tu,akaacha kuwa mjinga mjinga
Kanuni zipo ila ni za hovyo. Kama timu haijaingia uwanjani huwa inapigwa faini kubwa na kuzuiwa kushiriki hiyo ligi au mashindano.

Sasa kuruhusu mechi kuchezwa kwa timu moja kuwa na wachezaji 8 halafu bila faini au adhabu nyingine kwa hiyo timu hapo chama cha mpira kinafikiria nini? Vipi hiyo klabu ikiamua kwenda na mwendo huo huo wa kupeleka wachezaji pungufu na kusingizia wengine wanaumwa hiyo itakuwa na faida gani kwa ligi hata kama kanuni zinaruhusu?
 
Binafsi nimeumia mno kitayose kucheza pungufu, TFF ijiangalie inakosesha ladha ya soka,

Raha ya timu ishinde kihalali
Yaani badala useme viongozi wa vilabu wajiangalie unasema TFF ambayo imefuatw kanuni ndio ijiangalie hivi sisi watanzania tuna maisha ya aina gani yaani tunatamani kila kitu tupindishe ili kubebana na ushkaji mwingi.
Mambo kama haya waliyaleta Biashara Mara na Caf hawakuwa na huruma na wakasimamia kanuni tukakaa kimya ila ikiwa ni TFF mtu tu anatamani sheria zipindishwe kishkaji
 
Back
Top Bottom