Tetesi: Inasemekana Nape Nnauye kavuliwa Uanachama wa Chama cha Mapinduzi..

Status
Not open for further replies.
Nape siamini aisee... Ukivuliwa uanachama na jimbo unaliachia???
 
Ccm ni kubwa kuliko Nape
Ccm ilishawahi kutimua wazito kama maLim sef na wenzake 6,mpaka leo inadunda
Ccm ilishawahi kumpoka nyadhifa zake zote Jumbe
Kwenye chama chochote hata chama cha wapiga ngoma,lazima mzungumze lugha moja
Asichokijua Nape ni subira
 
Kwenu viongozi na makamanda wa CHADEMA nchi nzima.

Iwapo itathibitika kuwa ni kweli Nape kavuliwa uanachama wa CCM na sisi wapinzanzi tukaamua kumpokea,basi tujiandae kukabiliana na hii propaganda.

Mara tu atakapotua ndani ya chama(in case hatokwenda mahakamani) hoja yoyote ile tutakayoibua kulalamikia au kuhoji juu ya Bunge live,hoja hiyo itajibiwa kwa maneno kama vile:
"Nape ndio chanzo na Nape mnae katika chama chenu".

Pia wako watakaosema, "Muulizeni Nape na maneno mengine ya aina hiyo"

Tujiepushe kabisa kumpokea Nape.

Bashe ndio mtu tunaeweza kumpokea wakati wowote kwani hawatakuwa na la kusema na si Msukuma,Nape,na wengineo wanaotajwatajwa.
Walau umeangalia kwenye kona tofauti. Hawa watu hata wakija Chadema wabaki kuwa wanachama wa kawaida hadi mtaporidhika kuwa wanastahili kupewa uongozi ....otherwise CCM ya zamani ndio inaenda kuwa Chadema mpya .....mtajikuta mnahangaika kujibu tuhuma ambazo nyie ndio mliotuhumu miaka kibao .....binafsi sioni CCM kwenye wakati mgumu kuliko upinzani kuwa compromised beyond repair ....
 
Mtu amesema hakuwa na haja na uraisi...ila mkampatia uraisi...atang'ang'ania kwenye kiti mpak mwisho...na atakayempinga anawaka kama kawaida...!!!
 
Of coz nape should stape out and we will see. Ujinga hatutaki.
Mmmh " stape out"
Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema Nape Moses Nnauye amevuliwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi kufuatia kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti jijini Dar es salaam leo...

Habari hizi ni za kunyapia nyapia zinasema hata Lazaro nae yuko matatani.

Nape Nnauye alikuwa ni waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika Serikali ya Awamu ya Tano kabla uteuzi wake kutenguliwa. Aliteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la Rais John Pombe Magufuli. Yeye pia ni mbunge wa jimbo la Mtama lililoko mkoani Lindi.

Hivi sasa Nape ana miaka 40 alizaliwa mkoani Mwanza Novemba 7, 1977 ambako mama yake mzazi alikuwa mfanyakazi katika sekta ya elimu. Mama mzazi wa Nape anaitwa Keziah, ni mwalimu ambaye amefanya utumishi wake hadi alipostaafu mwaka 2015 akiwa katika ngazi ya Ofisa Elimu wa wilaya anayeshughulikia takwimu. Asili ya mama mzazi wa Nape ni mkoa wa Singida, yeye ni Mnyiramba.

Baba mzazi wa Nape ni Moses Nnauye (marehemu) ambaye alistaafu utumishi wa umma akiwa Brigedia Jenerali wa Jeshi. Asili ya baba yake Nape ni mkoa wa Lindi, yeye ni Mmakonde wa Chiuta, Nyangamara.

Uzoefu mkubwa wa Nape katika masuala ya Uongozi umejikita katika masuala ya siasa zaidi kuliko “utaalamu”. Amekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa tangu mwaka 2002 hadi 2012. Amekuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa kuanzia mwaka 2002 hadi leo.

Mwaka 2010 hadi 2011 aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Masasi, mahali alikotumikia kwa mwaka mmoja kabla ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mwaka 2011 na kisha mwaka huohuo akateuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa nafasi aliyoishikilia hadi mwishoni mwa mwaka 2015.

Nape alianza harakati za kusaka ubunge mwaka 2010, alishiriki katika kinyang’anyiro cha kura ya maoni ndani ya CCM katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam bila mafanikio (aliyeshinda kura za maoni ni Hawa Ng’umbi aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo). Mwaka 2015 Nape alihamishia majeshi nyumbani kwao, jimbo la Mtama. Bahati kubwa aliyokuwa nayo ni kwamba mwanasiasa nguli ndani ya CCM, Bernard Membe alikuwa ameshatangaza kuliacha jimbo hilo ili agombee urais.

Nape akapambana na kushinda kura ya maoni ndani ya chama chake kwa kupata kura 9,344 dhidi ya mpinzani wake Selemani Mathew (mchezaji wa zamani wa Yanga) aliyepata kura 4,766 (baada ya kushindwa Selemani alihamia Chadema na kugombea kwa tiketi ya chama hicho). Kura za jumla zilizopigwa Oktoba 25 zilimtangazia Nape ushindi wa jumla wa kura 28,110, Mathew wa Chadema akatokea wa pili kwa kupata kura 13,918 huku mgombea wa CUF akishikilia nafasi ya tatu.

Nguvu

Mambo mawili makubwa yanajenga nguvu na uwezo wa Nape katika siasa za sasa. Kwanza, huyu ni mmoja wa wanasiasa vijana wenye nguvu na ushawishi mkubwa wa maamuzi ndani ya CCM. Mchango wake kwenye siasa za jumla za kuiimarisha CCM katika miaka ya hivi karibuni hauwezi kupimika. Yeye ndiye mwanasiasa kijana wa CCM aliyefanikiwa kuzunguka sehemu kubwa ya nchi akiinadi CCM kwa kutumia staili ya “kushambulia chama chake” akishirikiana na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana. Staili ile kwa kiasi fulani iliisaidia CCM kujadiliwa tena na wananchi, wengi wakianza kuona kuwa kumbe hata viongozi sasa wanasema hadharani kuwa chama kina matatizo ya maadili na mengine mengi.

Kukaa ndani ya CCM muda mrefu na kusimamia mambo mengi ya mabadiliko ya kimfumo ndani ya chama hicho kunamfanya Nape awe mmoja wa vijana wa sasa ndani ya CCM wanaokifahamu chama hicho kwa undani. Uzoefu wa namna hiyo ni jambo kubwa na umemjengea uwezo wa kutosha na uzoefu wa kujua wapi kuna matatizo gani yanayohitaji ufumbuzi wa aina gani. Hili ni jambo kubwa sana kwake japokuwa tutaendelea kupima utendaji wake.
 
Kwenu viongozi na makamanda wa CHADEMA nchi nzima.

Iwapo itathibitika kuwa ni kweli Nape kavuliwa uanachama wa CCM na sisi wapinzanzi tukaamua kumpokea,basi tujiandae kukabiliana na hii propaganda.

Mara tu atakapotua ndani ya chama(in case hatokwenda mahakamani) hoja yoyote ile tutakayoibua kulalamikia au kuhoji juu ya Bunge live,hoja hiyo itajibiwa kwa maneno kama vile:
"Nape ndio chanzo na Nape mnae katika chama chenu".

Pia wako watakaosema, "Muulizeni Nape na maneno mengine ya aina hiyo"

Tujiepushe kabisa kumpokea Nape.

Bashe ndio mtu tunaeweza kumpokea wakati wowote kwani hawatakuwa na la kusema na si Msukuma,Nape,na wengineo wanaotajwatajwa.

Yaani shujaa wenu Nape Nnauye tena mnaanza kumkwepa makamanda?
 
nchi yao hii kejeli kwa wenzao kila kukicha

Pasipo kujua dunia hii haina mwenye nayo

Nasema hivi wacha wafukuzwe tena watoke kabisa na wengine washaanza kudai katiba mpya

Wapumbavu ndo wameifikisha nchi hapa
In kweli kabisa! Kipindi matumbo yao yalikuwa yakishiba, hawawajui wenye njaa! Ngoja wajifunze wapuuzi wakubwa!
 
aende cdm...ili akawaelezee vizui wananchi wa vijijin maana ya bombardier na faida zake...ccm alikuwa hapati nafasi vizur
 
Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema Nape Moses Nnauye amevuliwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi kufuatia kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti jijini Dar es salaam leo...

Habari hizi ni za kunyapia nyapia zinasema hata Lazaro nae yuko matatani.

Nape Nnauye alikuwa ni waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika Serikali ya Awamu ya Tano kabla uteuzi wake kutenguliwa. Aliteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la Rais John Pombe Magufuli. Yeye pia ni mbunge wa jimbo la Mtama lililoko mkoani Lindi.

Hivi sasa Nape ana miaka 40 alizaliwa mkoani Mwanza Novemba 7, 1977 ambako mama yake mzazi alikuwa mfanyakazi katika sekta ya elimu. Mama mzazi wa Nape anaitwa Keziah, ni mwalimu ambaye amefanya utumishi wake hadi alipostaafu mwaka 2015 akiwa katika ngazi ya Ofisa Elimu wa wilaya anayeshughulikia takwimu. Asili ya mama mzazi wa Nape ni mkoa wa Singida, yeye ni Mnyiramba.

Baba mzazi wa Nape ni Moses Nnauye (marehemu) ambaye alistaafu utumishi wa umma akiwa Brigedia Jenerali wa Jeshi. Asili ya baba yake Nape ni mkoa wa Lindi, yeye ni Mmakonde wa Chiuta, Nyangamara.

Uzoefu mkubwa wa Nape katika masuala ya Uongozi umejikita katika masuala ya siasa zaidi kuliko “utaalamu”. Amekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa tangu mwaka 2002 hadi 2012. Amekuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa kuanzia mwaka 2002 hadi leo.

Mwaka 2010 hadi 2011 aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Masasi, mahali alikotumikia kwa mwaka mmoja kabla ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mwaka 2011 na kisha mwaka huohuo akateuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa nafasi aliyoishikilia hadi mwishoni mwa mwaka 2015.

Nape alianza harakati za kusaka ubunge mwaka 2010, alishiriki katika kinyang’anyiro cha kura ya maoni ndani ya CCM katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam bila mafanikio (aliyeshinda kura za maoni ni Hawa Ng’umbi aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo). Mwaka 2015 Nape alihamishia majeshi nyumbani kwao, jimbo la Mtama. Bahati kubwa aliyokuwa nayo ni kwamba mwanasiasa nguli ndani ya CCM, Bernard Membe alikuwa ameshatangaza kuliacha jimbo hilo ili agombee urais.

Nape akapambana na kushinda kura ya maoni ndani ya chama chake kwa kupata kura 9,344 dhidi ya mpinzani wake Selemani Mathew (mchezaji wa zamani wa Yanga) aliyepata kura 4,766 (baada ya kushindwa Selemani alihamia Chadema na kugombea kwa tiketi ya chama hicho). Kura za jumla zilizopigwa Oktoba 25 zilimtangazia Nape ushindi wa jumla wa kura 28,110, Mathew wa Chadema akatokea wa pili kwa kupata kura 13,918 huku mgombea wa CUF akishikilia nafasi ya tatu.

Nguvu

Mambo mawili makubwa yanajenga nguvu na uwezo wa Nape katika siasa za sasa. Kwanza, huyu ni mmoja wa wanasiasa vijana wenye nguvu na ushawishi mkubwa wa maamuzi ndani ya CCM. Mchango wake kwenye siasa za jumla za kuiimarisha CCM katika miaka ya hivi karibuni hauwezi kupimika. Yeye ndiye mwanasiasa kijana wa CCM aliyefanikiwa kuzunguka sehemu kubwa ya nchi akiinadi CCM kwa kutumia staili ya “kushambulia chama chake” akishirikiana na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana. Staili ile kwa kiasi fulani iliisaidia CCM kujadiliwa tena na wananchi, wengi wakianza kuona kuwa kumbe hata viongozi sasa wanasema hadharani kuwa chama kina matatizo ya maadili na mengine mengi.

Kukaa ndani ya CCM muda mrefu na kusimamia mambo mengi ya mabadiliko ya kimfumo ndani ya chama hicho kunamfanya Nape awe mmoja wa vijana wa sasa ndani ya CCM wanaokifahamu chama hicho kwa undani. Uzoefu wa namna hiyo ni jambo kubwa na umemjengea uwezo wa kutosha na uzoefu wa kujua wapi kuna matatizo gani yanayohitaji ufumbuzi wa aina gani. Hili ni jambo kubwa sana kwake japokuwa tutaendelea kupima utendaji wake.
kama tetesi hizi zina ukweli basi ndiyo itakuanza chanzo cha mtifuano uliokuwa unasubiriwa kwa hamu maana upo uwezekano wa kuisambaratisha CCM
 
Nakumbuka siku za nyuma wakati wa awamu ya JK kulikuwa na kampeni ya kuvua gamba lakini busara za JK baada ya kuona nguvu ya wanaotakiwa kuvuliwa ni kubwa akaamua kurudi nyuma kwa hofu ya kusambaratika kwa chama. Sasa hili la Nape kama lina ukweli sidhani kama ataondoka peke yake lazima kuna kundi kubwa litamfuata nyuma na litakalobaki litakuwa la vibaraka watakaosaidia kuiua CCM.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom