Tetesi: Inasemekana Nape Nnauye kavuliwa Uanachama wa Chama cha Mapinduzi..

Tetesi: Inasemekana Nape Nnauye kavuliwa Uanachama wa Chama cha Mapinduzi..

Status
Not open for further replies.
Kama ni "kufosi" fani Nape analazimisha tu kuwa mwanasiasa ila kipaji chake halisi ni kama cha Ndanda Kossovo, Ali Choki nk.
Yaani alipoonyesha uthubutu wa kumsema Lowassa waziwazi (probably kwa kutumwa tu) ndio watu wakadhani ni bonge la mwanasiasa!
Hata itikikadi na uenezi alizokuwa anafanya ni kufyatuka na kuropoka tu, hakuna mkakati hata mmoja ambao aliuanzusha...
 
Bado wanaharakati wote wataondoka . Anyway Nape alishaliona hili nankupitia tweet zake wenye macho marefu tulijua hawezi kusurvive, unapishana na prince of zamunda utaishi zamunda kweli.
 
Mkuu sio CCM tu,ni chama chochote kile huwezi baki salama kama unapingana na FIKRA za mwenyekiti tena waziwazi na kwa kejeli na quotes za mipasho kwenye social networks. Tuliona akina zito,tukaona kafulila hata ACT yenyewe hakuna anayeweza kuwa juu ya FIKRA za zito akabaki salama,kwani Lucas limbu yuko wapi?Msiongee tu kwa sababu yanayotokea CCM na anayeyafanya anatimiza matamanio ya upinzan,EBU MCHUKUE NAPE MWEKE CHADEMA afu ndo angekua anafanya haya anayofanya.Je angebaki salama?SO NAPE ANA UHALALI KABISA NA NI HAKE YAKE KUFUKUZWA UANACHAMA na kama anaakili inatakiwa ajitoe mwenyewe.

Twende mbele turudi nyuma, Uncle sio mwana diplomasia, bado ana fikra kwamba ukimtisha mtu ndio atakusikiliza.

Mfano mimi nikikuuliza Bombadia ina faida gani na nchi utanijibu nini??
 
Mbona mmechelewa sana kumtimua Nape Nnaye Naomba isiwe tetesi tu.
 
safi sana, muasisi wa goli la mkono na oil chafu kutimuliwa
 
Twende mbele turudi nyuma, Uncle sio mwana diplomasia, bado ana fikra kwamba ukimtisha mtu ndio atakusikiliza.

Mfano mimi nikikuuliza Bombadia ina faida gani na nchi utanijibu nini??
Unaamn ni kweli nape aliulizwa hivo?pili je nape ndo kosa pekee alilofanya?Kauli ngapi za nape kama UNAAKILI timamu unajua kabisa hiki ni kijembe?
 
Unaamn ni kweli nape aliulizwa hivo?pili je nape ndo kosa pekee alilofanya?Kauli ngapi za nape kama UNAAKILI timamu unajua kabisa hiki ni kijembe?

Hata kama ni vijembe, kuongoza taasisi kubwa kama CCM au taasisi yoyote kubwa inahitaji kuwa na uvumilivu, ustahimilivu, werevu na weledi wa kushughulikia changamoto kama hizo.

Ni mfano kuwa baba wa familia, unaweza kuwa na mtoto mvuta bangi, kikojozi, asiependa shule n.k sasa kama mzazi utawafukuza nyumbani au utaka nao chini kuwaelekeza kuelekea njia bora??
 
Hayo yanawezekana lkn sio kwenye siasa.lkn hata ktk family ka kuna mtoto mtukutu huwa kuna njia za kumwadhibu.kwenye siasa nako kuna njia za kukuadhibu.
 
Hayo yanawezekana lkn sio kwenye siasa.lkn hata ktk family ka kuna mtoto mtukutu huwa kuna njia za kumwadhibu.kwenye siasa nako kuna njia za kukuadhibu.

Unajua tatizo ambalo limetudidimiza Watanzania kwa Miaka 50 ni UNAFIKI. Unafiki ndio umetufanya tufike hapa tulipo au tuwe na hali tulikuwa nayo.

Tunapenda maisha ya upambe upambe, kujipendekeza pendekeza, mfano kama Steve Nyerere kind of life style.

Kitu hata kama ni kibaya hatuwezi kuhoji kwa sababu mkuu atakasirika au watu flani wachachache wana maslahi nacho.

Sasa leo akitokea mtu akahoji kitu anaonekana ni tofauti kabisa na anapingwa vibaya sana, japokuwa hao wanaompinga kwenye mioyo yao wanajua ni kweli.

Hii ni kwa vyama vyote na watanzania kwa ujumla, tuwe na Ujasiri wa kuhoji pale tunapoona maslai ya umma yanachezewa na wachache, hii ndio kazi ya upinzani.
 
Mbona hii post ni kama inatoa WASIFU wa huyo Nape?

It's kinda campaigning
 
Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema Nape Moses Nnauye amevuliwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi kufuatia kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti jijini Dar es salaam leo...

Habari hizi ni za kunyapia nyapia zinasema hata Lazaro nae yuko matatani.

Nape Nnauye alikuwa ni waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika Serikali ya Awamu ya Tano kabla uteuzi wake kutenguliwa. Aliteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la Rais John Pombe Magufuli. Yeye pia ni mbunge wa jimbo la Mtama lililoko mkoani Lindi.

Hivi sasa Nape ana miaka 40 alizaliwa mkoani Mwanza Novemba 7, 1977 ambako mama yake mzazi alikuwa mfanyakazi katika sekta ya elimu. Mama mzazi wa Nape anaitwa Keziah, ni mwalimu ambaye amefanya utumishi wake hadi alipostaafu mwaka 2015 akiwa katika ngazi ya Ofisa Elimu wa wilaya anayeshughulikia takwimu. Asili ya mama mzazi wa Nape ni mkoa wa Singida, yeye ni Mnyiramba.

Baba mzazi wa Nape ni Moses Nnauye (marehemu) ambaye alistaafu utumishi wa umma akiwa Brigedia Jenerali wa Jeshi. Asili ya baba yake Nape ni mkoa wa Lindi, yeye ni Mmakonde wa Chiuta, Nyangamara.

Uzoefu mkubwa wa Nape katika masuala ya Uongozi umejikita katika masuala ya siasa zaidi kuliko “utaalamu”. Amekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa tangu mwaka 2002 hadi 2012. Amekuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa kuanzia mwaka 2002 hadi leo.

Mwaka 2010 hadi 2011 aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Masasi, mahali alikotumikia kwa mwaka mmoja kabla ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mwaka 2011 na kisha mwaka huohuo akateuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa nafasi aliyoishikilia hadi mwishoni mwa mwaka 2015.

Nape alianza harakati za kusaka ubunge mwaka 2010, alishiriki katika kinyang’anyiro cha kura ya maoni ndani ya CCM katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam bila mafanikio (aliyeshinda kura za maoni ni Hawa Ng’umbi aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo). Mwaka 2015 Nape alihamishia majeshi nyumbani kwao, jimbo la Mtama. Bahati kubwa aliyokuwa nayo ni kwamba mwanasiasa nguli ndani ya CCM, Bernard Membe alikuwa ameshatangaza kuliacha jimbo hilo ili agombee urais.

Nape akapambana na kushinda kura ya maoni ndani ya chama chake kwa kupata kura 9,344 dhidi ya mpinzani wake Selemani Mathew (mchezaji wa zamani wa Yanga) aliyepata kura 4,766 (baada ya kushindwa Selemani alihamia Chadema na kugombea kwa tiketi ya chama hicho). Kura za jumla zilizopigwa Oktoba 25 zilimtangazia Nape ushindi wa jumla wa kura 28,110, Mathew wa Chadema akatokea wa pili kwa kupata kura 13,918 huku mgombea wa CUF akishikilia nafasi ya tatu.

Nguvu

Mambo mawili makubwa yanajenga nguvu na uwezo wa Nape katika siasa za sasa. Kwanza, huyu ni mmoja wa wanasiasa vijana wenye nguvu na ushawishi mkubwa wa maamuzi ndani ya CCM. Mchango wake kwenye siasa za jumla za kuiimarisha CCM katika miaka ya hivi karibuni hauwezi kupimika. Yeye ndiye mwanasiasa kijana wa CCM aliyefanikiwa kuzunguka sehemu kubwa ya nchi akiinadi CCM kwa kutumia staili ya “kushambulia chama chake” akishirikiana na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana. Staili ile kwa kiasi fulani iliisaidia CCM kujadiliwa tena na wananchi, wengi wakianza kuona kuwa kumbe hata viongozi sasa wanasema hadharani kuwa chama kina matatizo ya maadili na mengine mengi.

Kukaa ndani ya CCM muda mrefu na kusimamia mambo mengi ya mabadiliko ya kimfumo ndani ya chama hicho kunamfanya Nape awe mmoja wa vijana wa sasa ndani ya CCM wanaokifahamu chama hicho kwa undani. Uzoefu wa namna hiyo ni jambo kubwa na umemjengea uwezo wa kutosha na uzoefu wa kujua wapi kuna matatizo gani yanayohitaji ufumbuzi wa aina gani. Hili ni jambo kubwa sana kwake japokuwa tutaendelea kupima utendaji wake.
Sishangai Nape kutemwa. CCM ilishakufa tangu 2015 kimebaki kivuli tu cha CCM na Rais Magufuli tu kama yeye. Tangu lini mtu kama Polepole akawa msemaji wa chama kikubwa sana kama CCM kilichopigania Uhuru wetu na ule wa mataifa mengine?
 
Unajua tatizo ambalo limetudidimiza Watanzania kwa Miaka 50 ni UNAFIKI. Unafiki ndio umetufanya tufike hapa tulipo au tuwe na hali tulikuwa nayo.

Tunapenda maisha ya upambe upambe, kujipendekeza pendekeza, mfano kama Steve Nyerere kind of life style.

Kitu hata kama ni kibaya hatuwezi kuhoji kwa sababu mkuu atakasirika au watu flani wachachache wana maslahi nacho.

Sasa leo akitokea mtu akahoji kitu anaonekana ni tofauti kabisa na anapingwa vibaya sana, japokuwa hao wanaompinga kwenye mioyo yao wanajua ni kweli.

Hii ni kwa vyama vyote na watanzania kwa ujumla, tuwe na Ujasiri wa kuhoji pale tunapoona maslai ya umma yanachezewa na wachache, hii ndio kazi ya upinzani.
Sikia mkuu kila chama kina njia zake za kuhoji.Huwez kuta wabunge wa chadema wanahoji maamuzi ya mwenyekiti wao hadharani. Vivyo hivo kwa ccm ndio utasema anahoji mambo ya maendeleo lkn inatakiwa ujue bado nape ni CCM na anayoyahoji lzm yatakuwa na impact flan ktk chama chake xo lazma afuate utaratibu wa kuwasilisha malalamiko yake.Nape bila CCM hajawa mbunge so kuidharau njia iliyompa madaraka sidhani ka ni sahh.Maamuz yyt juu ya utekelezaji wa sera kama ni kupinga kuna vikao halali huko.Ushawah ona chadema wanabishana mbowe akisema tutoke nje bungeni?Kama kubishana wanabishania kwenye vikao vyao.Sasa nape anataka kubishana na chairman wake kwenye mitandao mara kwa wananchi wake anajifanya eti wamemuuliza. Hivi itkuaje leo kubenea au Lema kwenye page yake akaandika HIVI HUKO KUSUSIA BUNGE NDO KUTUWAKILISHA WANANCHI?Nambie itakuaje?
 
Ccm ni kubwa kuliko Nape
Ccm ilishawahi kutimua wazito kama maLim sef na wenzake 6,mpaka leo inadunda
Ccm ilishawahi kumpoka nyadhifa zake zote Jumbe
Kwenye chama chochote hata chama cha wapiga ngoma,lazima mzungumze lugha moja
Asichokijua Nape ni subira
CCM isikie hivi hivi,wanakukaanga kwa mafuta yako.Kama kweli wamempiga chini,akijifanya yeye ndio yeye,watamfungulia lundo la udhahifu wake kwani record zote zake hadi magoli ya mkono wanazo.
Atulie tu kama Mama Simba.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom