Tetesi: Inasemekana Nape Nnauye kavuliwa Uanachama wa Chama cha Mapinduzi..

Tetesi: Inasemekana Nape Nnauye kavuliwa Uanachama wa Chama cha Mapinduzi..

Status
Not open for further replies.
Sikia mkuu kila chama kina njia zake za kuhoji.Huwez kuta wabunge wa chadema wanahoji maamuzi ya mwenyekiti wao hadharani. Vivyo hivo kwa ccm ndio utasema anahoji mambo ya maendeleo lkn inatakiwa ujue bado nape ni CCM na anayoyahoji lzm yatakuwa na impact flan ktk chama chake xo lazma afuate utaratibu wa kuwasilisha malalamiko yake.Nape bila CCM hajawa mbunge so kuidharau njia iliyompa madaraka sidhani ka ni sahh.Maamuz yyt juu ya utekelezaji wa sera kama ni kupinga kuna vikao halali huko.Ushawah ona chadema wanabishana mbowe akisema tutoke nje bungeni?Kama kubishana wanabishania kwenye vikao vyao.Sasa nape anataka kubishana na chairman wake kwenye mitandao mara kwa wananchi wake anajifanya eti wamemuuliza. Hivi itkuaje leo kubenea au Lema kwenye page yake akaandika HIVI HUKO KUSUSIA BUNGE NDO KUTUWAKILISHA WANANCHI?Nambie itakuaje?

Ndugu Misuli, sifikirii kama Komredi Nape ni Balidhuli kama tunavyofikiria, Nape ni mtoto wa Chama, Nape amekuzwa na CCM, Nape kasomea itikadi ya CCM chuo cha Kivukoni.

Naikumbuka siku Nape anashinda ujumbe wa NEC alikuwa bado ni Mwafafunzi pale Kivukoni, ilikuwa ni Bonge la Party ilikuwa 2002-2003.

Nape leo hii hawezi hivi hivi kumvua kanga hadharani mama mlezi aleye mlea.

Tusiwe watu wa ndiooo , tuwe watu wa kuhoji na kutafakari.

Kuhusu CDM sijui wanavyofanya kazi, naongelea chama ambazo kidogo naelewa mambo yake.
 
Ndo kusema hawataki bao LA mkono tena, ukivuliwa uanachama VIP na ubunge unakoma?Kama usipokoma unakuwa unawakilisha chama kipi.
 
Hizi tetesi bado tetesi tu? itakuwa mambo ya ajabu hii thread ime trend kiasi hiki kwa mambo ya umbea tu
 
CCM isikie hivi hivi,wanakukaanga kwa mafuta yako.Kama kweli wamempiga chini,akijifanya yeye ndio yeye,watamfungulia lundo la udhahifu wake kwani record zote zake hadi magoli ya mkono wanazo.
Atulie tu kama Mama Simba.

Hilo ndio kosa letu Watanzania.

Katokea mtu ana challenge utawala, mnamshauri akae kimya??

Kuna ubaya gani mtu ukihoji kuhusu rasimali za wengi??

Mnataka aishi maisha ya kinafiki kusifia ambacho anaona sio sawa kwa mtazamo wake??
 
Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema Nape Moses Nnauye amevuliwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi kufuatia kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti jijini Dar es salaam leo...

Habari hizi ni za kunyapia nyapia zinasema hata Lazaro nae yuko matatani.

Nape Nnauye alikuwa ni waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika Serikali ya Awamu ya Tano kabla uteuzi wake kutenguliwa. Aliteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la Rais John Pombe Magufuli. Yeye pia ni mbunge wa jimbo la Mtama lililoko mkoani Lindi.

Hivi sasa Nape ana miaka 40 alizaliwa mkoani Mwanza Novemba 7, 1977 ambako mama yake mzazi alikuwa mfanyakazi katika sekta ya elimu. Mama mzazi wa Nape anaitwa Keziah, ni mwalimu ambaye amefanya utumishi wake hadi alipostaafu mwaka 2015 akiwa katika ngazi ya Ofisa Elimu wa wilaya anayeshughulikia takwimu. Asili ya mama mzazi wa Nape ni mkoa wa Singida, yeye ni Mnyiramba.

Baba mzazi wa Nape ni Moses Nnauye (marehemu) ambaye alistaafu utumishi wa umma akiwa Brigedia Jenerali wa Jeshi. Asili ya baba yake Nape ni mkoa wa Lindi, yeye ni Mmakonde wa Chiuta, Nyangamara.

Uzoefu mkubwa wa Nape katika masuala ya Uongozi umejikita katika masuala ya siasa zaidi kuliko “utaalamu”. Amekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa tangu mwaka 2002 hadi 2012. Amekuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa kuanzia mwaka 2002 hadi leo.

Mwaka 2010 hadi 2011 aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Masasi, mahali alikotumikia kwa mwaka mmoja kabla ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mwaka 2011 na kisha mwaka huohuo akateuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa nafasi aliyoishikilia hadi mwishoni mwa mwaka 2015.

Nape alianza harakati za kusaka ubunge mwaka 2010, alishiriki katika kinyang’anyiro cha kura ya maoni ndani ya CCM katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam bila mafanikio (aliyeshinda kura za maoni ni Hawa Ng’umbi aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo). Mwaka 2015 Nape alihamishia majeshi nyumbani kwao, jimbo la Mtama. Bahati kubwa aliyokuwa nayo ni kwamba mwanasiasa nguli ndani ya CCM, Bernard Membe alikuwa ameshatangaza kuliacha jimbo hilo ili agombee urais.

Nape akapambana na kushinda kura ya maoni ndani ya chama chake kwa kupata kura 9,344 dhidi ya mpinzani wake Selemani Mathew (mchezaji wa zamani wa Yanga) aliyepata kura 4,766 (baada ya kushindwa Selemani alihamia Chadema na kugombea kwa tiketi ya chama hicho). Kura za jumla zilizopigwa Oktoba 25 zilimtangazia Nape ushindi wa jumla wa kura 28,110, Mathew wa Chadema akatokea wa pili kwa kupata kura 13,918 huku mgombea wa CUF akishikilia nafasi ya tatu.

Nguvu

Mambo mawili makubwa yanajenga nguvu na uwezo wa Nape katika siasa za sasa. Kwanza, huyu ni mmoja wa wanasiasa vijana wenye nguvu na ushawishi mkubwa wa maamuzi ndani ya CCM. Mchango wake kwenye siasa za jumla za kuiimarisha CCM katika miaka ya hivi karibuni hauwezi kupimika. Yeye ndiye mwanasiasa kijana wa CCM aliyefanikiwa kuzunguka sehemu kubwa ya nchi akiinadi CCM kwa kutumia staili ya “kushambulia chama chake” akishirikiana na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana. Staili ile kwa kiasi fulani iliisaidia CCM kujadiliwa tena na wananchi, wengi wakianza kuona kuwa kumbe hata viongozi sasa wanasema hadharani kuwa chama kina matatizo ya maadili na mengine mengi.

Kukaa ndani ya CCM muda mrefu na kusimamia mambo mengi ya mabadiliko ya kimfumo ndani ya chama hicho kunamfanya Nape awe mmoja wa vijana wa sasa ndani ya CCM wanaokifahamu chama hicho kwa undani. Uzoefu wa namna hiyo ni jambo kubwa na umemjengea uwezo wa kutosha na uzoefu wa kujua wapi kuna matatizo gani yanayohitaji ufumbuzi wa aina gani. Hili ni jambo kubwa sana kwake japokuwa tutaendelea kupima utendaji wake.
Iwe ni kweli au sio kweli kama amefukuzwa lakini watanzania wooote lazima wajue kuwa wapinzani pia ni watanzania wenzao na kuwa upinzani sio dhambi wala laana na Walioko chama tawala pia sio wahuni, wezi wala wahalifu ni watanzania wenzao. Kinachotakiwa kufanywa na watanzania ni kutumia njia za kawaida kabisa za kuomba kura, kupiga kura, kuhesabu kura kama zilivyopigwa na kutangazwa mshindi kutokana na kura zilivyopigwa. Kwa kauli na vitendo vyake enzi zake Nape hukuonyesha kama watanzania walioko vyama vya upinzani ni watanzania wenye akili na haki ya kuliongoza taifa hili. Aliwaona akina Kingunge, Sumaye na wengine kama wendawazimu fulani. Hakujuwa kuwa baada ya Mwl. Nyerere kufa CCM imebaki haina mwenyewe hata mmoja.
 
Hao wengine ni akina nani, maana mnasema wanatajwa kwenye mitandao
 
Unapoisema Bombadia kwa kusudi la "kuisimanga",jiandae kwa lolote.
Ile ndio "kampeni" ya baba mwenye nyumba!!
Bombadia ni Dili la Bashite na GSM wao ndiyo Madalali wanakula 10% kiimya kiimya na Nape anajua mchezo wote, Bashite hapendi Bombadia kuongelewa na wana Siasa ndiyo maana Lisu alikamatwa pindi alipoiongelea tu, cheza na vyote lakini Dili lao usiguse.
 
Sikia mkuu kila chama kina njia zake za kuhoji.Huwez kuta wabunge wa chadema wanahoji maamuzi ya mwenyekiti wao hadharani. Vivyo hivo kwa ccm ndio utasema anahoji mambo ya maendeleo lkn inatakiwa ujue bado nape ni CCM na anayoyahoji lzm yatakuwa na impact flan ktk chama chake xo lazma afuate utaratibu wa kuwasilisha malalamiko yake.Nape bila CCM hajawa mbunge so kuidharau njia iliyompa madaraka sidhani ka ni sahh.Maamuz yyt juu ya utekelezaji wa sera kama ni kupinga kuna vikao halali huko.Ushawah ona chadema wanabishana mbowe akisema tutoke nje bungeni?Kama kubishana wanabishania kwenye vikao vyao.Sasa nape anataka kubishana na chairman wake kwenye mitandao mara kwa wananchi wake anajifanya eti wamemuuliza. Hivi itkuaje leo kubenea au Lema kwenye page yake akaandika HIVI HUKO KUSUSIA BUNGE NDO KUTUWAKILISHA WANANCHI?Nambie itakuaje?
Dili ya bombadia sio ya CCM pesa za bombadia ni za walipa kodi pia Kumbuka ununuzi wake haukupata baraka za Bunge Dodoma bali ilinunuliwa kibabe kwa shinikizo la Madalali Bashite na watu wake ili wapiga cha juu 10% hivyo haipaswi kujadiliwa kichama wasitake kutengeneza kisingizio cha kumuonea Kumbambikia shutuma feki wapate kumpora kadi ya CCM, wanamtisha sana ndiyo maana Nape kaogopa kwenda Nairobi kumjulia hali Lisu.
 
Sikia mkuu kila chama kina njia zake za kuhoji.Huwez kuta wabunge wa chadema wanahoji maamuzi ya mwenyekiti wao hadharani. Vivyo hivo kwa ccm ndio utasema anahoji mambo ya maendeleo lkn inatakiwa ujue bado nape ni CCM na anayoyahoji lzm yatakuwa na impact flan ktk chama chake xo lazma afuate utaratibu wa kuwasilisha malalamiko yake.Nape bila CCM hajawa mbunge so kuidharau njia iliyompa madaraka sidhani ka ni sahh.Maamuz yyt juu ya utekelezaji wa sera kama ni kupinga kuna vikao halali huko.Ushawah ona chadema wanabishana mbowe akisema tutoke nje bungeni?Kama kubishana wanabishania kwenye vikao vyao.Sasa nape anataka kubishana na chairman wake kwenye mitandao mara kwa wananchi wake anajifanya eti wamemuuliza. Hivi itkuaje leo kubenea au Lema kwenye page yake akaandika HIVI HUKO KUSUSIA BUNGE NDO KUTUWAKILISHA WANANCHI?Nambie itakuaje?

Hivi matatizo ya CCM hayana mfano mwingine kujilinganisha zaidi ya CHADEMA?
 
Nape ajishushe! Zama zimebadilika, akivuliwa uawanachama hata akigombea tena watamchakachua.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom