Inasemekana TBL Mwanza kuhamishia Shughuli zake Uganda

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
1,353
Reaction score
2,846
Ni taarifa ya mshtuko mkubwa kama ni kweli, nimepenyezewa hapa kuwa Kampuni ya vinywaji ya TBL-Mwanza inataka kuhamishia Uganda shughuli zake kwa madai kuwa soko la vinywaji nchini limeporomoka sana hadi kuwabidi kupunguza uzalishaji wa bia zao lakini wapi, biashara haiendi.

Naona wanywaji wengi kwa sasa wamepunguza unywaji kwa kiwango kikubwa na wengine wanalazimika kwenda supermarket kununua bia za makopo na kwenda kunywea nyumbani, hivyo bar nyingi kwa sasa hazina wateja sana, vile vile, zile posho kwa wafanyakazi wa serikali zimefutwa, wafanyakazi wengi hawasafiri sana kwenda nje ya nchi ambapo napo walikuwa wakilipwa posho ya kutosha, nasikia hata pesa ya chai maofisini imefyekwa sana hata pesa za kununulia magazeti maofisini zimefutwa, si hilo tu, zile posho za kukirimu wageni wanaowatembelea viongozi mbalimbali majumbani mwao ambazo JK. aliziidhinisha nazo zimekatwa kabisa, sasa hapo watu watakunywaje bia Jamani? deal nyingi zimepungua sana.

Kwa sasa kila mtu anabana matumizi yasiyo ya lazima hata kupokea wageni kutoka kijijini ni shida sana kwa sasa.

Acha tuisome namba Ila naomba JPM afanye kazi kwelikweli, abane matumizi kwa faida, natarajia kuona Reli mpya, Ndege za Serikali, Meli, Barabani za lami tena nasikia zimebaki barabara mbili au tatu zinazounganisha mikoa-mikoa ambazo bado hazina lami, hongera saba serikali, kazeni buti kwa maendeleo ya nchi.

.............................................TUFUNGE MKANDA..............................................
 
hii ni tetesi au maoni yako binafsi?
 
Hilo la posho ya chai sio sahihi,
bado tunapoke laki2 kama posho ya chai kila mwezi! Ndo inatumika kuendeshea vikao vidogo vidogo
 
Sielewi mada yako imejikita kwenye nini hasa, Mara TBL kuhamia Uganda kutokana na kuyumba kwa soko lao, Mara safari za nje as if TBL ilikua hao watumishi wakisafiri wanaondoka na products za kiwanda kwenye mabegi yao,Mara posho ya chai, yaani sikuelewi kabisa mkuu! Bora ungetumia muda huu ulioandika haya madudu kujifunza kuwa uchumi haulindwi au kujengwa na wafanyakaz peke yao kwaiyo mtikisiko huu hausababishwi na vitu pekee ulivyovitaja hapo juu, otherwise itakua ni majungu yako tu dhidi ya hao wafanyakazi
 

Sasa usichoelewa ni nini? hayo yote yawezekana yamasababishwa na hatua za serikali kubana matumizi...

Kama huelewi kitu bora ukae kimya
 
habari nzuri kama matumizi ya pombe yanapungua kwani pombe ni maradhi, fanyeni viwanda vingine
 
Sasa usichoelewa ni nini? hayo yote yawezekana yamasababishwa na hatua za serikali kubana matumizi...

Kama huelewi kitu bora ukae kimya
Sijamuelewa mtoa Uzi anahusishaje ukosefu wa chai maofisin na kuhama kwa TBL, wewe huna mamlaka ya kunitaka nikae kimya kwa jambo nisilolielewa, ni bora angetoa Uzi wa kubana matumizi kuliko kutuchanganyia habari za kuhama kwa TBL na kukosekana kwa chai maofisin
Kuhama kwa TBL na watumishi kuto safiri nje ya nchi !! Atoe Uzi wa kutueleza kubana matumizi na si kutuchanganyia madesa ya bia na vitu visivyo na uhusiano wanywaji wengi wa bia hasa bia hizi za kuvimbisha tumbo (safari lager,kilimanjaro n.k) ni watu wa kawaida sana kama wafanyabiashara ndogo ndogo, wachomelea vyuma na wauza mitumba wala si hao peke yao waliokua wakisafiri nje ya nchi, Labda useme ugumu wa maisha umechangia viwanda vya vinywaji kukosa soko La bidhaa zao so TBL wanataka kuondoka.
 
Wafanyakazi hawasafiri nje,hawana sababu wafunge,wakaongeze walevi na wazinzi huko waendako!
 


Ni ngumu kuamini hayo unayoyasema kwa sababu kwanza soko la Bia UG limeshajaa kwa maana kuna EABL huko na sidhani kama kuna nafasi tena ya Kampuni nyingine ya Bia!
 
TBL watuombe radhi walevi, yani tunavyotwanga hizi pombe wao wanasema soko limeshuka!!!!!! huku ni kutudharau na kutujaribu walevi, mkawaambie hao TBL sisi walevi hatujaribiwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…