Brigedia Chan-ocha
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 1,353
- 2,846
Ni taarifa ya mshtuko mkubwa kama ni kweli, nimepenyezewa hapa kuwa Kampuni ya vinywaji ya TBL-Mwanza inataka kuhamishia Uganda shughuli zake kwa madai kuwa soko la vinywaji nchini limeporomoka sana hadi kuwabidi kupunguza uzalishaji wa bia zao lakini wapi, biashara haiendi.
Naona wanywaji wengi kwa sasa wamepunguza unywaji kwa kiwango kikubwa na wengine wanalazimika kwenda supermarket kununua bia za makopo na kwenda kunywea nyumbani, hivyo bar nyingi kwa sasa hazina wateja sana, vile vile, zile posho kwa wafanyakazi wa serikali zimefutwa, wafanyakazi wengi hawasafiri sana kwenda nje ya nchi ambapo napo walikuwa wakilipwa posho ya kutosha, nasikia hata pesa ya chai maofisini imefyekwa sana hata pesa za kununulia magazeti maofisini zimefutwa, si hilo tu, zile posho za kukirimu wageni wanaowatembelea viongozi mbalimbali majumbani mwao ambazo JK. aliziidhinisha nazo zimekatwa kabisa, sasa hapo watu watakunywaje bia Jamani? deal nyingi zimepungua sana.
Kwa sasa kila mtu anabana matumizi yasiyo ya lazima hata kupokea wageni kutoka kijijini ni shida sana kwa sasa.
Acha tuisome namba Ila naomba JPM afanye kazi kwelikweli, abane matumizi kwa faida, natarajia kuona Reli mpya, Ndege za Serikali, Meli, Barabani za lami tena nasikia zimebaki barabara mbili au tatu zinazounganisha mikoa-mikoa ambazo bado hazina lami, hongera saba serikali, kazeni buti kwa maendeleo ya nchi.
.............................................TUFUNGE MKANDA..............................................