Tetesi: Inasemekana Viongozi wa CHADEMA wanaenda kukamatwa na kutoachiliwa mpaka Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uishe

Tetesi: Inasemekana Viongozi wa CHADEMA wanaenda kukamatwa na kutoachiliwa mpaka Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uishe

MAMLAKA YA BUNGE YA KUMUONDOA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA CHINI YA IBARA YA 46A ya KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977.​


Ibara ya 46A YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977; INAYOHUSU KUMUONDOA MADARAKANI (IMPEACHMENT) RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 [Cap. 2 R.E. 2002.] Leo hii Ijumaa 22/10/2010) - Somo la Katiba [Constitutional Law]

ZOEZI HILI HUCHUKUA JUMLA {KAMA KILA KITU KINAKWENDA SAWA - ceteris paribus} YA SIKU 150 au miezi mitano.

Rais (Mhimili wa Utawala) anaweza kuondolewa madarakani chini ya Ibara hii kwa tuhuma za aina nne:
  • kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
  • Kukiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi [Leadership Code]
  • Kukiuka vipengele vilivyomo katika maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya Siasa yaliyotajwa katika Ibara ya 20 (2) ya Katiba, au
  • Amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1. Ili kuanzisha mchakato huo inahitaji idadi ya asilimia 20 (20%) ya Wabunge waliopo wafikishe Notisi ya maandishi na kuiwasilisha kwa Spika. Siku 30 zipite kabla ya kikao cha kujadili hizo tuhuma:

2. Baada ya kupita hizo siku 30, MTOA HOJA ATAIWASILISHA BUNGENI.

-Aidha tuhuma zitupwe au
- Wapendekeze kuunda Kamati ya Kuchunguza tuhuma hizo.

3. Bunge litapiga kura ili iundwe Kamati ya Kuchunguza tuhuma hizo; lakini kura hizo lazima zifikie au zizidi theluthi mbili ya kura zote. Kama ndio,

4. Spika anatakiwa kutaja majina ya Kamati ya Uchunguzi chini ya Ibara ya 46A(4) ambao ni:
(a) Jaji Mkuu (Mwenyekiti)
(b) Jaji Mkuu wa Zanzibar
(c) Wajumbe saba wanaoteuliwa na Spika; kwa kuzingatia Kanuni za Bunge na Uwakilishi wa Vyama vya Siasa Bungeni.

Matokea ya No. 3 hapo juu chini ya Ibara 46A (5) ni kwamba

  • RAis anasimamishwa kazi
  • Vivyo Ibara ya 37 (3) inafanya kazi. (Edapo Rais hatakuwepo madarakani wakati huo)

Jambo hili la kumsimamisha kazi Rais litaendelea hadi hapo Spika atakapomfahamisha Rais juu ya matokeo ya uchunguzi uliofanywa [Ibara ya 46A (5)]

Na. 4 hapo juu Kamati inapewa siku 7 kukamilisha uchunguzi wake na kumpa fursa Rais ya kujieleza [Ibara ya 46A (6)]

Kamati ya uchunguzi inapewa siku 90 kukamilisha ripoti yake na kuiwasilisha kwa Spika.

Ibara ya 46A (8) - Spika anawasilisha Ripoti ya Uchunguzi kwa Bunge

Ibara ya 46A (9) - Bunge lenye idadi isiyopungua theluthi mbili litajadili Ripoti hiyo na kumpa Rais fursa ya kujieleza.

Bunge linatakiwa liibuke na aidha ya majibu yafuatayo:

(i) Kwamba tuhuma zimethibitishwa.
(ii) Kwamba Rais hafai kuendelea kufanya kazi
(iii) Kwamba Rais hafai kuwa Rais
(iv) Kwamba tuhuma hazikuthibitishwa.

Ibara 46A(10) - Baada ya hilo kufanyika, endapo ni (i) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatakiwa kuachia ngazi (resign) ndani ya siku tatu.

MCHAKATO HUO WOOOOTE ULIOTAJWA HAPO JUU UKIFUATAWA KAMA UNAVYOTOLEWA kisheria unatakiwa kumalizika ndani ya siku 150 sawa sawa na miezi 5 kamili.

JAMANI, HILI KWELI LINAWEZEKANA AU IBARA YA 46(A) ya Jamhuri ya Muungano wa TAnzania imewekwa kiini macho tu kwa sisi walalahoi wa Tanzania tuendelee kuota kwamba tukifanyikwa kinyume na Ibara hii basi rais ataendelea kupeta tu???????? Nasema hivi kwa sababu mchakato mzima ni mgumu na hauna mwelekea wa kufanikiwa hasa ikingatiwa idadi ya wabunge husika wa mchakato huu!!!!!!


Kuna vitu huwa najiuliza sijui ni civics ndio nilikuwa siielewi au walimu walikuwa hawajui kutufundisha, kwamba kama bunge na sirikali ni miimili tofauti kwanini kusingekuwa na mfumo wa kuwezesha wabunge wa chama kilichochukua uraisi wasifike 50% ili kupunguza kubebana pale mjengoni? maana kila mtu anamtetea boss wake na mambo ya wengi wape na ndiooooooooo, inatupeleka kwenye selewi.

Ni mafikirio yangu tu, Sisi watu wa afya mambo ya siasa hatukuyaelewa au walimu walikuwa hawajui wanachokifundisha kama ni sawa.
 
Washitakiwe tu maana kauli za kusema Samia Must Go ni Uhaini Mkubwa sana .
Kwa akili zako ndogo zilivyo sawa kufikiria hivyo utaambiwa uliambiwa you must go to toilet.
Kwani wewe mshamba ukiambiwa must go unaelewa nini?
 
Uhaini wa kuandamana Kwa kupaza sauti wakibeba mabango haujawahi kuwepo popote duniani.
 
Washitakiwe tu maana kauli za kusema Samia Must Go ni Uhaini Mkubwa sana .
Dogo tulia, tayari mmeshikwa pabaya..
Tlaatlaah
 
Uhaini unatokea wapi hapo??

Tangu lini maandamano ya amani, ambapo ni halali Kwa mujibu wa Katiba yetu yakawa uhaini??

In fact hivyo vyombo vya Dola (ambavyo vinalindwa Kwa nguvu zote) ndivyo vinaweza kukabiliwa na kesi ya "murder" ya Ali Kibao🙄
 
Nilimpenda sana Samia, yaani nilikuwa nakupenda mpaka wanafikiria nimelogwa but after that incident.Niishie hapo.Ila Bashite ameanza kuweweseka kati ya wakuu wa mikoa yeye ndio yuko busy na issue za CDM wenzio kimya kisomo cha Tanga kimeanza kumpata
 
Back
Top Bottom