Tetesi: Inasemekana wagner group waamua kuisupport ukrane

Taiwan ile pale, mwambie China aende akaone balaa.
 
Binafsi mi naona NATO hawajapeleka silaha tu bali wanajeshi wa kutosha wa NATO wanapigana upande wa Ukrain.

Wanajeshi wa Ukrain peke yao wasingeweza kumtikisa Urusi hata kama wangepewa silaha kwa sababu wanajeshi wengi wa Ukrain wamekufa na raia wengine waliishakimbia nchi na pia wanajeshi waliopo hai wapo wanapambana kule upande wa Donbasa.

Hapa Urusi asipokuwa makini kuingia meza ya mazungumzo habari yake itaisha maana kaishalemazwa na vita takribani miaka 2 na sasa anashambuliwa kwa usaidizi wa NATO
 
Taiwan ile pale, mwambie China aende akaone balaa.
Umri wako unaweza akisi ulicho andika.

Kiwango cha upeo ulicho nacho wewe kuhusu masuala ya China na ya kimataifa na walichonacho viongozi wa China ni tofauti.

Si ajabu kuona una andika hiki ulicho andika.
 
Putin hapa kapatikana.

Hakuna Mwananchi wa Russia atamuunga mkono kwa yanayoendelea.
 
Putin alifanya kosa kubwa sana kuivamia Ukraine,japo hakuwa na jinsi kwa dalili za uchokozi za. NATO na US lakini angejizuiya mambo yasingekuwa magumu kiasi hiki.
Ameharibu uchumi wanchi,ameruhusu maadui kumsoma jinsi anavyo pigana,namengine mengi sasa wanaamua kumchokoza waone atafanyanini.

So far meshachelewa NATO tayari wapo kazini kumuondoa.
 
Russia haitaji support toka kwa China. Russia hainunui ndege vita inatumia zake, China inanunua ndege kwa Russia. Russia hainunui air defence system toka popote inatengeneza zake, China inanunua air defence za Russia. Kwa ufupi kwenye military tech China ni tegemezi kwa Russia na hivyo mpango wake wa kuivamia Taiwan lazima ajue wapi atapata backup. Na kwenye siasa za kimataifa mkono mtupu haulambwi. China bega kwa bega na Russia.

Kuhusu Ukraine hiyo ni kazi ndogo sana. Ukraine inajua moja ya mbinu ya Russia ni kusafisha kila kitu inapofanya operation zake za kijeshi na Russia haiwezi kuuharibu mji wake kwahiyo wataachwa wajae kwanza kisha Russia itaziba njia zote za kuingia na kutoka na winter inakaribia nchini Russia.
 
Usisahau Kuna china,Korea ya kaskazini,Iran,Syria,Algeria, Yemen, Vietnam na marafiki wengine wa Urusi wataibuka mara baada ya Hali kua kama unavyosema.
Hakuna rafiki kwa mtu anaekaribia kushindwa vita. Sahau.
 
Nimegundua kuwa kelele nyingi za Putin ilikuwa ni kurishia Nyau kumbe ni mweupe ka Azam flour ,pamoja na msaada wa Iran norh Korea Bado anakula kipigo Zelensk noma
 
Hivi nyie mnaijua Russia kweli? Hao Wagner Kama wanataka maslahi yao yote yafyekwe na kundi kupotea.
 
Hakuna rafiki kwa mtu anaekaribia kushindwa vita. Sahau.
Ukraine ndio inashindwa vita. Kujaribu kushikilia miji ya Russia ndio kete yake ya mwisho hiyo maana wachambuzi wa vita wanasema endapo mpango huo wa Ukraine utafeli basi kuna uwezekano wa Ukraine ika-surrender sababu kwanza Russia itayachukua maeneo yote yaliyopakana na Kursk na belgorod na kutengeneza buffer zone ili kuizuia Ukraine kurudia kujipenyeza tena.

Wakati huo huo Russia inaendelea kujitwalia maeneo zaidi ya Ukraine na mapambano yanaendelea.

Kursk ina ukubwa wa 29800km². Ukraine wanajeshi wa kulikalia eneo hilo wakati huo huo aendelee kupigana nchini mwake. Russia imeshapeleka wanajeshi Kursk na operation inaendelea taratibu hadi kazi ikamilike.
 
Acha kujipa moyo. Russia mwaka just aliingia hadi kyyiv na wakapigwa
 
Siku karibu ya 10 adui kaingia chumbani kwako anajaribu miondonbinu, anauza walinzi wako hujamtoa tu unasubiri nini?
 
Huko ngorongoro nasikia nayenyewe ngoma inachemkia chini kwa chini
 
Siku karibu ya 10 adui kaingia chumbani kwako anajaribu miondonbinu, anauza walinzi wako hujamtoa tu unasubiri nini?
Vita ni mbinu kila hatua inakuwa calculated. Kinachofanya counter offensive za Ukraine zifeli ni kwa sababu Ukraine inatafuta matokeo ya mapema ili kuwaaminisha west kuwa wanapiga kweli ndio maana taarifa nyingi za field wanazificha. Ukraine inasema Russia imeishambilia Kiev kwa ballist 2 na drone 30 na wamefanikiwa kuziangusha drone zote ila hawasemi kuhusu missiles, au drone 28 kati ya 30 zimeangushwa ila hawasemi drone mbili zimefanya nini. Kwahiyo habari za Ukraine sio za kuziamini sana.
 
Propaganda ni moja ya Silaha kubwa katika vita yo yote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…