Inashangaza Kenya wanalalamika mambo ya Loliondo na wanahojiwa Aljazeera TV. Je, kuna mamluki Loliondo toka Kenya?

Inashangaza Kenya wanalalamika mambo ya Loliondo na wanahojiwa Aljazeera TV. Je, kuna mamluki Loliondo toka Kenya?

Africa is one, Nelson Mandela alipopata uhuru S. A. alisema sipo huru mpaka parestina watakapokuwa huru
 
Sheria ya ardhi ya Tanzania inaweka bayana kabisa kuwa ardhi ni mali ya Umma,kama nchi inaona kipande fulani cha ardhi kina maslahi ya Taifa ina haki ya kuwaondoa wakazi wa eneo hilo na kuwatafutia mahali pengine pa kuendeleza maisha yao.

Hao wanaowatia ndimu hao wafugaji wa kitanzania ni kwa kuwa wao huko kwao ukishamilikishwa ardhi inakuwa ni yako milele,Tanzania hatuna sheria ya kipumbavu ya hivyo,ndio maana wanalizimisha tufanane.

Serikali ipo sahihi kuwaondoa
 
Ndiyo maana wengine tuliishia kukaa kimya tulipomuona "Mama" anahangaika kutafuta suluhu na wakenya.

Bomba la mafuta lenyewe ni Mkenya ameenda kuhamasisha maandamano Ufaransa kushinikiza TOTAL wajitoe!
 
Hata mlima Kilimanjaro ukiuzwa Kenya ndo watalalamika.

Yupo mtu mmoja alisema historia iandikwe upya, wabongo wakamsakama kwa maneno magumu.

Hata yule mtu mmoja alipohamisha makazi nikamsikia yule aliyekuwa huko elimu akijinasibu kuwa hatuna mpango wa kuandika historia yetu upya.

Upo mwaka fulani kule kwa pesambili walipandisha bendera ya Kenya au hamkusikia?

Mmesahau kuwa EAC ilivunjika baada ya Kenya kuona kuwa wanatubeba.

Tukubaliane tu wakenya wako mbele yetu miaka kumi zaidi.

I like Uhuru Kenyatta.
 
Taarifa ya Aljazeera TV imeambatanishwa kuhusu Wakenya wa Nairobi kutetea Loliondo kuwa Wamasai wabaki, Wakenya wa Nairobi wamewekeza kitu gani huko Loliondo?

Loliondo ni Tanzania wao Wakenya wanahojiwa na Aljazeera kuhusu sheria za ardhi Tanzania na wanapotosha kwa lengo gani?

Propaganda zinafanywa na Kenya kwa kiasi kikubwa kuharibu jina la Tanzania kimataifa, Loliondo ipo Tanzania kwa nini Wakenya wapo mbele kuelezea mambo ya Loliondo yasiyowahusu huko Aljazeera TV

Je, Wakenya wana maslahi na Loliondo?

Je, yale makundi ya mifugo Loliondo ina milikiwa na matajiri wa Kenya wa Nairobi ambao ndio wanahojiwa Aljazeera TV?

Ni Hakika kuna Wakenya wengi huko Loliondo.

Inashangaza Wakenya wa Nairobi ndio wanahojiwa na Aljazeera TV huku wakielezea kwa uchungu kuwa lazima wamasai wabaki Loliondo.

Wakenya wanasema kuna majeruhi katika hospitali za jirani walioumizwa na polisi.

Kwa nini wahojiwe Wakenya wa Nairobi na sio Watanzania wa Loliondo, Loliondo Itakuwa imevamiwa na Wakenya.

Ni wakati wa Serikali kuwa makini na wafugaji na watu toka Kenya waliojazana huko Loliondo.

Video Nimeambatanisha

Kwanini kila anayetetea wananchi huwa mnakimbilia kusema ni mamluki au katumwa na mabeberu? je, ni haki kwa serikali kuwaumiza wananchi wake kisa tu inataka pesa (ambazo watafaidi viongozi wachache) za mwekezaji?
 
Tanzania inaandamwa kwa mambo mengi sana kwa interest za kisiasa....Maadui nao wanatumia mwanya huo kujifaidisha maana wanajua mitanzania ni mijinga issue na haijui umuhimu wa kusimama na serikali yao kwenye baadhi ya issues.....Wanasiasa wa Tanzania nao kwa maslahi ya kisiasa bila wao kujua wanafaidisha majirani maadui..
 
Serekali hii hii ya majizi ya kura ndio watu wasimame nayo? Ukitaka kuungwa mkono ingia madarakani kwa njia halali, kinyume na hapo pambana na hali yako.
 
Siri zao wanazijua wao.

Bottom Line, kwa sheria ya Tanzania, serikali inaweza mwamishwa mtu yoyote, mahali poppte, kwa manufaa ya taifa.
Kupuuzia hizo siri ndio kuliangamiza taifa, hakuna kufanya hivyo.

"Manufaa ya taifa" sio "manufaa ya watu wachache" lazima ujue kutofautisha hapo.
 
Wamasai ndio kabila linaongoza kwa kutowa rushwa Tanzania.

Mkulima hana haki mbele ya mmasai, waulizeni watu wa Morogoro hasa Kilosa ndio watawaambia Wamasai ni watu gani.
Kama una ushahidi wa rushwa wanazotoa wamasai kwanini huwapeleki mahakamani?

Wale jamaa wanapigwa na kuumizwa halafu unaleta stori ya kutunga hapa ili ku justify madhila wanayofanyiwa, wacha utoto wako.
 
Wewe Itakuwa mmasai

Jiwe limepigwa gizani

Ukisikia ohoooo ujue limekupata

Mbona watu walihamishwa kimara kupisha barabara?

Ardhi ni ya serikali Wataishi hapo kwa kuzaliana mpaka lini?
Tena mmasai wa Kenya. Mimi nashauri serikali iendelee na oparation zake hadi pale mabwanyenye ya Kenya na haya ma puppet yao yaliopo nchini yarudi yalipotoka.
 
Taarifa ya Aljazeera TV imeambatanishwa kuhusu Wakenya wa Nairobi kutetea Loliondo kuwa Wamasai wabaki, Wakenya wa Nairobi wamewekeza kitu gani huko Loliondo?

Loliondo ni Tanzania wao Wakenya wanahojiwa na Aljazeera kuhusu sheria za ardhi Tanzania na wanapotosha kwa lengo gani?

Propaganda zinafanywa na Kenya kwa kiasi kikubwa kuharibu jina la Tanzania kimataifa, Loliondo ipo Tanzania kwa nini Wakenya wapo mbele kuelezea mambo ya Loliondo yasiyowahusu huko Aljazeera TV

Je, Wakenya wana maslahi na Loliondo?

Je, yale makundi ya mifugo Loliondo ina milikiwa na matajiri wa Kenya wa Nairobi ambao ndio wanahojiwa Aljazeera TV?

Ni Hakika kuna Wakenya wengi huko Loliondo.

Inashangaza Wakenya wa Nairobi ndio wanahojiwa na Aljazeera TV huku wakielezea kwa uchungu kuwa lazima wamasai wabaki Loliondo.

Wakenya wanasema kuna majeruhi katika hospitali za jirani walioumizwa na polisi.

Kwa nini wahojiwe Wakenya wa Nairobi na sio Watanzania wa Loliondo, Loliondo Itakuwa imevamiwa na Wakenya.

Ni wakati wa Serikali kuwa makini na wafugaji na watu toka Kenya waliojazana huko Loliondo.

Video Nimeambatanisha

Ecosystem ya Loliondo inavuka mpaka Kenya, ni moja, ni kama ilivyo ecosystem ya Serengeti/Masai Mara au Mkomazi na Tsavo kwa upande wa Same/Taita Taveta. Athari za upande mmoja zinavuka mpaka upande mwingine
 
Wakenya wanachotaka ni mbuga yetu ife na watalii waende uko kwao
Kwann na wao wasijaze watu wazaliane humo masai mara
 
Ingekua magufuli yupo usingewasikia wakifoka foka hao mazombi inabidi viongozi waangalie sana hawa watu ni wabaya sana hawatutakii mema japo majirani zetu!
 
Kupuuzia hizo siri ndio kuliangamiza taifa, hakuna kufanya hivyo.

"Manufaa ya taifa" sio "manufaa ya watu wachache" lazima ujue kutofautisha hapo.
Wamasai waliamishwa serengeti na kupelekwa Ngorongoro kuinasua Mbuga ya Serengeti kwa manufaa ya taifa mwaka 1959, vivyo hivyo sasa wanaamishwa Ngorongoro kwenda handeni kunusuru Ngorongoro kwa manufaa ya taifa. Manufaa gani, kama huelewi, basi hutonielewa. Manufaa ya taifa ya Serengeti na Ngorongoro yanajulikana, yapo wazi kabisa.

Wamepewa eneo Handeni, waende huko, kukaidi ni kukaidi mamlaka, kichapo kitatembea kama kinavyotembeaga kwa wengine wanaokaidi mamlaka.

Mtwara walijazwa hivyo hivyo, manufaa ya gesi wayapate wao tu, hakuna kitu kama hicho Tanzania.

Pia watu wanachanganya kinachoendelea Ngorongoro na Loliondo, ni vitu viwili tofauti, japo vyote vina wa affect watu wa jamii moja.

Tanzania ni yetu sote, uishindwa staarabika, utastaarabishwa.
 
Taarifa ya Aljazeera TV imeambatanishwa kuhusu Wakenya wa Nairobi kutetea Loliondo kuwa Wamasai wabaki, Wakenya wa Nairobi wamewekeza kitu gani huko Loliondo?

Loliondo ni Tanzania wao Wakenya wanahojiwa na Aljazeera kuhusu sheria za ardhi Tanzania na wanapotosha kwa lengo gani?

Propaganda zinafanywa na Kenya kwa kiasi kikubwa kuharibu jina la Tanzania kimataifa, Loliondo ipo Tanzania kwa nini Wakenya wapo mbele kuelezea mambo ya Loliondo yasiyowahusu huko Aljazeera TV

Je, Wakenya wana maslahi na Loliondo?

Je, yale makundi ya mifugo Loliondo ina milikiwa na matajiri wa Kenya wa Nairobi ambao ndio wanahojiwa Aljazeera TV?

Ni Hakika kuna Wakenya wengi huko Loliondo.

Inashangaza Wakenya wa Nairobi ndio wanahojiwa na Aljazeera TV huku wakielezea kwa uchungu kuwa lazima wamasai wabaki Loliondo.

Wakenya wanasema kuna majeruhi katika hospitali za jirani walioumizwa na polisi.

Kwa nini wahojiwe Wakenya wa Nairobi na sio Watanzania wa Loliondo, Loliondo Itakuwa imevamiwa na Wakenya.

Ni wakati wa Serikali kuwa makini na wafugaji na watu toka Kenya waliojazana huko Loliondo.

Video Nimeambatanisha

Interest za Kenya ni mbuga za kaskazini mwa Tanzania ambako ndo moyo wa utalii na mapato makubwa yanayotokana na utalii zinakufa kwa kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu hivyo wanyama kukimbilia Kenya na watalii kuacha kuja Tanzania na kwenda Kenya

Wanaoshupalia hili suala la Ngorongoro na Loliondo kama sio mamluki wa Kenya basi ni wapuuzi wachache wasioelewa mambo na kazi yao ni kudandia tu treni kwa mbele
 
Umewahi kumsikia Mkenya gani anahangaika kuongea kiingereza ? Hao wote wanaoongea ni watanzania usiwasingizie wakenya Kwa weakness za nchi yako

Wakenya wanaongea sana kiswahili fuatilia ile ya kuokota makopo na kuuza waliokua wanahojiwa ni wakenya tena Kwenye hiyo hiyo aljazeera!
 
Serekali hii hii ya majizi ya kura ndio watu wasimame nayo? Ukitaka kuungwa mkono ingia madarakani kwa njia halali, kinyume na hapo pambana na hali yako.

image ya nchi inapoharibika kwako wewe ni sawa tu kwasababu ya tofauti za kisiasa, kesho waKenya wakitaka kuchukua Mlima kilimanjaro kwako ni sawa tu.... Uganda wakivamia Bukoba kwako ni sawa tu...

Kuna wakati tujifunze kutofautisha siasa zetu hizi na mambo ya msingi yanayogusu Taifa letu kama Watanzania na yatakayoacha shida kwa vizazi na vizazi...hata hao unaoamini wanaibiwa kura infuture wakishika dola watapambana na hizo athari..

Wakenya wanatumia akili kama hizi kuhakikisha hizo Mbuga zinakufa na biashara inabidi kwao, unafikiri hapa athari ni kwa hawa unao waita majizi tu?
 
Back
Top Bottom