Inashangaza sana Jiji la Arusha linatoa ajira kwa watumishi wa Umma ilhali kuna watu wengi ambao hawana ajira

Inashangaza sana Jiji la Arusha linatoa ajira kwa watumishi wa Umma ilhali kuna watu wengi ambao hawana ajira

Huu ni utani na wananchi ambao hawana ajira. Jiji la Arusha mlifikiria hili mkiwa wazima wa afya ama mlikuwa mmekunywa rubisi?? Enyi serikali hebu wajalini wananchi wenu kwa usawa. Watu hawana ajira, inatokea ajira ya muda badala muwape ajira wasiokuwa na ajira mnawapa wenye ajira??? Wacha tukae bila ajira Wala pesa. Tutashinda huku mitandaoni kuwasema hadi mlewe. Wabinafsi wakubwa nyie. Keki ya Taifa hamtaki kutugea na sisi wananchi.
WANANCHI WENZANGU, NAFASI ZA KAZI HIZO HAPO...LAKINI NI KWA WATUMISHI TU.

Mkurugenzi wa halmashauri (DED) wa jiji la Arusha John Lipesi Kayombo akikaribishwa ofisini, sasa anatumia kofia ya pili ya cheo chake cha muda kama Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Jiji Arusha.

Habari za hivi punde​

1727292159881.png
Picha maktaba Posted on: August 21st, 2024 Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini (kushoto) amemkabidhi ofisi Mkurugenzi mpya wa Jiji la Arusha Bwana John Lipesi Kayombo mapema leo. Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na viongozi.

Makabidhiano ya ofisi kwa wakurugenzi (DED) hao yametokana na mabadiliko ya uteuzi yaliyofanywa mnamo Agosti 14, 2024 na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Sami Suluhu Hassan, kwa Mhandisi Juma Hamsini kuhamishiwa Jiji la Tanga na bwana John Kayombo kupangiwa Halmashauri ya Jiji la Arusha akitokea Jiji la Dodoma.

Kabla ya kwenda kuwa DED jiji la Dodoma, John Lipesi Kayombo aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufanya uteuzi tarehe 07 Julai, 2016.

Utendaji na uchapakazi wa DED John Lipesi Kayombo:

(March 2018)




Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa ufafanuzi wa muongozo wa ukusanyaji wa mapato kwa Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa

Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo

MD Kayombo akisisitiza jambo




Maafisa Watendaji wa Kata 14, Watendaji wa Mitaa 91 pamoja na Wahasibu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wameonywa kutopokea Rushwa wala hongo ya aina yoyote kutoka kwa wamiliki wa biashara mbalimbali katika Manispaa hiyo kwani kufanya hivyo watadhoofisha ukusanyaji wa mapato ya serikali kama ilivyokusudiwa.

Kauli ya onyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati akitoa ufafanuzi wa muongozo wa ukusanyaji wa mapato na kutoa maelekezo ya majukumu ya kazi kwa Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa kwenye kikao cha kazi kilichofanyika leo Jumamosi Machi 18, 2017 katika ukumbi wa Ofisi za Manispaa hiyo ilipo Mtaa wa Kibamba CCM.


March 4 , 2017

kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo ya Ubungo mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo (Aliyesimama) Boniface Jacob akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo, Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo na kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Ramadhan Kwangaya

Wenyeviti wakisikiliza kwa makini maelekezo mbalimbali wakati wa kikao cha kazi kilichoendeshwa na Mwenyekiti wa kikao hicho Mhe Boniface Jacob ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo (Picha zote na Nassir Bakari
 
Hapo kwenye sifa kuna moja inasema
...asiwe kada wa chama chochote, ila utashangaa Tlaatlaah na chawa mwenzie Lucas Mwashambwa, nk wamo
ni jambo la ajabu sana, eti zoezi linakaribia hata kufikia tamati ndio, anaibuka mtu kushangaa namna ya waliofanya zoezi hilo waliajiriwaje, wakati ndivyo wahusika wa zoezi hilo hupatikana miongoni mwa wananchi, nje na ndani ya utumishi wa umma..

Infact,
haitakuja kua tofauti na jinsi hiyo ya ajira kwenye mambo muhimu na ya maana sana namna hiyo ya kitaifa.

Na it is simple.
Ili kuepuka hujuma, migomo, fujo za malipo ya ziada, kufuata mkumbo n.k huwezi kuajiri walio nje ya ajira pekee, kwasababu kwanza hawana uzoefu kabisa na hivyo ni muhimu pakawepo wa kuwaongoza katika kutimiza wajibu wao..

Mtindio huo wa ajira za muda mfupi hautabadilika katika kuhusisha watumishi walio nje na ndani ya ajira, kwani umeonyesha ufanisi mkubwa lakini pia umeepusha hujuma na migomo ya madai bila subra n.k🐒
 
Mtumishi wa umma hata muuza karanga ni mtumishi wa umma kwahiyo tuma maombi
 
Zoezi linatumia vifaa vya gharama kama vishikwambi na BVR kwahyo kumpa mtu ambaye ata akikimbia na kifaa hujui utampatia wapi ni moja ya sababu ya kuajiri watumishi wa umma ili kukwepa hyo risk.
 
Mtumishi wa umma anakuwa tayari kwa kazi kwa sababu anajua how the chain flow. Hakuna vetting itakayohutajika. Kuna matukio katika nchi yanakuwa yameungana kwa namna moja au nyingine na national security. Matukio kama usimamizi wa mitihani ya kitaifa, uandikishaji wa wapiga kura, usimamizi wa upigaji kura, hata sensa yote yanakaribiana na national security. Kwa hiyo kuchukua watu na kulipia lupus, kisa ajira, mimi binafsi naona sio sawa. Ajira zipo na karibia kila wiki sekretriat ya ajira katika Utumishi wa umma, wanatangaza nafasi za kazi za umma. Achilia mbali private sector.
Wewe mtu kujali usalama wa Nchi yake haitokani kwamba alikuwa Mtumishi miaka mingap nadhani hiyo mtazamo ni old school hata hao watumishi wanaweza haribu unakuta Wana vinyongo vyao au something. Msipokuwa fair na makini kwanye Hili la Vijana na ajira ni bomu Baya kuliko la Nuclear. Asikiaye na afahamu. Bora Ifike mahali elimu isimame mpk Fursa ziwe za kutosha😝 Unfairness yoyote ktk maisha ya watu haswa Vijana ni Hatari. Naongea sababu ninawaona wahanga na jinsi wanavyoumia ktk maongez Yao huwez kujua wanaomba au kuwaza nn.
 
27 September 2024

Karibu Mtazamaji wa Uchaguzi TV INEC katika muendelezo wa Kipindi Maalumu Kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura


View: https://m.youtube.com/watch?v=5D3JjcqcZl0

Uboreshaji wa Daftari​


Kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakuwa mara mbili kati ya kipindi kinachoanza mara baada ya uchaguzi mkuu na kabla ya siku ya uteuzi. Wanaohusika katika zoezi hili ni wananchi ambao: -
  1. Wametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea ambao hawakuandikishwa hapo awali;
  2. Watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025;
  3. Waliojiandikisha awali na wamehama Kata au Jimbo moja kwenda jingine;
  4. Waliopoteza sifa mfano wale waliofariki kuondolewa katika Daftari;
  5. Wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji; na
  6. Waliopoteza au kadi zao kuharibika.
Watendaji wa Uandikishaji/ Uboreshaji
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi hutumia watendaji mbalimbali wakati wa Uandikishaji na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Watendaji hawa ni pamoja na:-
  1. Waratibu wa Uchaguzi wa Mkoa;
  2. Maafisa Waandikishaji;
  3. Maafisa Waandikishaji Wasaidizi;
  4. Waandishi Wasaidizi; na
  5. Mwenyesha Kifaa cha Bayometriki
Mawakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura
Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Chama cha Siasa chenye usajili wa kudumu kinaweza kumteua mtu mmoja katika kila kituo cha uandikishaji kuwa Wakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura.

Wajibu / Majukumu ya Mawakala wa Uandikishaji
  1. Kufuatilia zoezi la uboreshaji na kutazama kama linazingatia Sheria, Kanuni na Maelekezo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
  2. Kushirikiana na Waandishi Wasaidizi kutambua wakazi wa eneo hilo na kutoa taarifa juu ya watu wasio na sifa.
Pamoja na majukumu tajwa, Mawakala wa Uboreshaji hawaruhusiwi kufanya yafuatayo:-
  1. Kuingilia shughuli za uendeshaji wa zoezi la Uboreshaji. Msimamizi wa kituo ndiye mwenye mamlaka ya mwisho juu ya nani anastahili kuandikishwa au kuboresha taarifa zake kwa mujibu wa Sheria.
  2. Kufanya kampeni za kisiasa katika kituo cha uandikishaji
  3. Kuorodhesha majina ya watu wanaojiandikisha.
Kiapo cha Kutunza Siri cha Mawakala wa Uandikishaji
Kila Wakala wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, ni lazima kula kiapo cha kutunza siri za taarifa za mwombaji au Mpiga Kura aliyeandikishwa.

Wakala atakula kiapo mbele ya Afisa Mwandikishaji au Afisa Mwandikishaji Msaidizi. Hata hivyo, kutokuwepo kwa Wakala wa uandikishaji katika kituo cha kuandikisha Wapiga Kura hakuzuii utekelezaji wa majukumu ya Uandikishaji Wapiga Kura.


Watazamaji wa Uandikishaji
Kwa mujibu wa Kanuni za 46, 47, 48, 49, 50 na 51 (1) za Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za Mwaka 2024 zilizoandaliwa chini ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024 Watazamaji wa ndani na kimataifa, wanaruhusiwa kutazama mchakato wa Uboreshaji utakavyofanyika katika vituo vya Uandikishaji.

Watazamaji wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutembelea vituo vya Uandikishaji, ni lazima waombe na kupatiwa idhini ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Watazamaji. Aidha, Watazamaji 24 watakao ruhusiwa na Tume watapewa barua za kuwatambulisha kwa Maafisa Waandikishaji na Mwongozo wa watazamaji wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulioandaliwa na Tume.

Maafisa Waandikishaji watatakiwa kuwapa barua za kuwatambulisha kwa Watendaji wa vituo ambavyo watavitembelea. Aidha, Watazamaji wa Uandikishaji wa Wapiga Kura hawapaswi kutoa maelekezo kwa Mwandishi Msaidizi katika kituo husika.

Kuweka Wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura
Kwa mujibu wa Kifungu vya 11 (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Tume inatakiwa kuweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura ili kutoa fursa kwa wananchi:
  1. Kulikagua Daftari;
  2. Kufanya marekebisho ya majina au mahali wanapoishi;
  3. Kuingiza au kufuta majina ya Wapiga Kura;
  4. Kuweka pingamizi kwa Mpiga Kura aliyeandikishwa na hana sifa za kuwemo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Kumuwekea Pingamizi aliyeandikishwa kwenye Daftari la Awali
Kifungu cha 27 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024,kinaruhusu Mkurugenzi wa Uchaguzi au Afisa Mwandikishaji au mtu yeyote aliyeandikishwa kuwa Mpiga Kura, kuweka pingamizi dhidi ya jina lililopo katika Daftari la Awali la Wapiga Kura. Kifungu cha 28 Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, kinaweka utaratibu wa kuweka pingamizi.

Mtu aliyewekewa pingamizi hutakiwa kupelekewa taarifa ili aweze kutoa ufafanuzi ndani ya siku saba (7).

Kifungu cha 29 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024 Mahakama itapaswa kutoa uamuzi wa rufaa hiyo ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kupokea rufaa hiyo, uamuzi wa Mahakama ya Wilaya na iwapo aliyewekewa pingamizi hakubaliani na 25 maamuzi ya Afisa Mwandikishaji ya kuendelea kukataliwa kuwemo katika Daftari, ana haki ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi Wilaya ndiyo utakuwa uamuzi wa mwisho na mtu hatoweza kukata rufaa katika Mahakama nyingine yoyote

Source : INEC
 
Back
Top Bottom