Inashangaza sana mtu analipa hela kuangalia mpira kwenye TV huku bado anasikiliza kwenye redio

Inashangaza sana mtu analipa hela kuangalia mpira kwenye TV huku bado anasikiliza kwenye redio

Msichoke

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
569
Reaction score
400
Siku za hivi karibuni kumekuwa na mwamko kwa Watanzania kufuatilia ligi kuu ya hapa nyumbani, ujio wa Azam TV unawakusanya wapenda soka kwenye vibanda umiza hasa zinapocheza SIMBA au YANGA.

Maajabu makubwa ni pale unapomuona mtu kalipia pesa aangalie mpira kwenye TV lakini muda mwingi anautumia kuusikiliza kwenye radio.

Huwa najiuliza tatizo ni nini?
(a) Aamini anachokiona hivyo lazima asikilize na chombo kingine?
(b)Watangazaji wa TV hawana ladha?
(c)Mazoea ya mpira kusikiliza redioni tangu enzi?
 
Attachments

  • umiza.jpg
    umiza.jpg
    8.1 KB · Views: 68
mpira unaotangazwa kwenye radio unawahi kupata matokeo kabla wa kwenye TV kwa hiyo mtu anakua na shauku ya kujua nini kinatokea kabla ya kuona kwenye runinga
 
mpira unaotangazwa kwenye radio unawahi kupata matokeo kabla wa kwenye TV kwa hiyo mtu anakua na shauku ya kujua nini kinatokea kabla ya kuona kwenye runinga
Sasa kuna raha gani kuangalia marudio kwenye TV?
 
Kwa sisi tunaoelewa mambo ya transmission, tunajua kuwa matangazo ya sauti yanawahi kwa sekunde 2 au 3 mbele ya matangazo ya picha. Hivyo huyo anaesikiliza kwenye radio goli likifungwa anasikia mapema kuliko wanaoangalia kwenye tv.
 
Siku za hivi karibuni kumekuwa na mwamko kwa Watanzania kufuatilia ligi kuu ya hapa nyumbani,ujio wa Azam TV unawakusanya wapenda soka kwenye vibanda umiza hasa zinapocheza SIMBA au YANGA.
Maajabu makubwa ni pale unapomuona mtu kalipia pesa aangalie mpira kwenye TV lakini muda mwingi anautumia kuusikiliza kwenye radio.
Huwa najiuliza tatizo ni nini?
(a) Aamini anachokiona hivyo lazima asikilize na chombo kingine?
(b)Watangazaji wa TV hawana ladha?
(c)Mazoea ya mpira kusikiliza redioni tangu enzi?
Mkuu ulisha wahi kumsikiliza mwalimu kashasha ndio utajua utamu radio
 
kwanza Mimi nafurahia kumsikiliza mwalimu Alex kashasha so hata kwenye TV sipendelei sana kukaa maana watangazaji na mchambuzi wao hawanivutii
 
huku kwetu zikipigwa game za epl kuna watu wana tabia iyo ya kutangaza goli kabla sie wa kuangalia tv hatujaliona......tushawapa sana visago na kuwakimbiza bandani
 
Ukiingia na Redio kwenye kibanda umiza lazima utoke na manundu.
 
Ushamba wa namna hii umejizolea umaarufu mkubwa sana pande za Arusha mitaa ya Unga Ltd.
 
Back
Top Bottom