Inashangaza sana Mtumishi wa umma kulawiti watu watatu Igunga

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
2,268
Reaction score
7,119
Hata kama ni kweli zaidi ya miezi mitatu anawalawiti alafu anakuja kukamatwa mwezi huu!

IMG_20260413_104955_488.jpg

=======
Watu Watatu wakazi wa Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora wanadaiwa kulawitiwa na mtumishi wa halmashauri ya wilayani humo kwa nyakati tofauti.

Akizungumza na Mwananchi leo Aprili 12, 2026 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema wanaodaiwa kulawitiwa, wawili ni wanafunzi wa Shule ya Sekondari (17) na (18) na mmoja ni fundi pikipiki wilayani humo.

"Inadaiwa mtumishi huyu amekua akiwafanyia vitendo hivyo mara kadhaa hao wanafunzi pamoja na huyu fundi pikipiki ambaye ni mkazi pia wa hapo hapo Igunga," amesema Kamanda Abwao.

Amesema mtumishi huyo ambaye anafanya kazi halmashauri ya Igunga upande wa utawala na mkazi wa mtaa wa Stoo Igunga mjini, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Tabora kwa ajili ya mahojiano zaidi ikiwa ni pamoja na uchukuaji wa sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa kisayansi kwa pande zote mbili.

Amebainisha kuwa mbinu aliyokua akiitumia mtuhumiwa ni kuwarubuni na vitu tofauti na kuwapa fedha anapowahitaji.

"Tumefanya mahojiano ya awali na uchunguzi wa awali pia umefanyika, kuna baadhi ya vitu tumebaini lakini tunaendelea na uchunguzi kubaini tatizo zaidi ili tuweze kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria," amesema.

Amesema matukio hayo yanadaiwa kutekelezwa katika kipindi cha Desemba 2025 hadi Aprili 6 2026, katika nyakati tofauti na maeneo tofauti wilayani humo.

Kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi wa Tabora kuchukua tahadhari na kuacha kurubuniwa na vitu ambapo inapelekea kuharibu utu na heshima yao.

"Haiwezekani unakubali kirahisi kufanyiwa vitu vya ajabu na hutoi taarifa, unakuwa umeridhika tu na hela ndogo ambazo pia hazileti matokeo yoyote kwenye maisha yenu."

Amewahimiza wazazi na walezi kuhakikisha wanafanya ufuatiliaji wa karibu kwa watoto wao ili kubaini vitendo hivi kwa haraka vinapojitokeza, hasa ikizingatiwa vijana hao wawili ni wanafunzi wa kidato cha nne ni nguvu kazi ambayo inapaswa kurudi kuleta matokeo kwenye jamii.

"Lindeni watoto na wafuatilieni na mkiona mambo ambayo hamuyaelewi tupeni taarifa mapema tuchukue hatua, msisubiri mpaka tatizo liwe kubwa lakini pia msipende kumaliza kesi nyumbani kwa matukio kama haya," amesema Kamanda Abwao.

Chanzo: Mwananchi
 
Daktari akithibitisha kuwa waliingiliwa?
Anaweza kuthibitisha lakini mtuhumiwa asiwe yeye.. Maana kitakachomkamatisha mtu ni shahawa finger prints na DNA.. Sasa watuhumiwa walishaoga zaidi ya mara moja.. Ushahidi wote umeshafutisha!

mambo makuu yanayozingatiwa ili kuthibitisha kosa hili:

1. Ripoti ya Polisi na Fomu ya PF3
Hatua ya kwanza ni kutoa taarifa kituo cha polisi, ambapo mhanga hupewa Fomu ya Polisi namba 3 (PF3).

Fomu hii ni muhimu sana kwani inaruhusu daktari kufanya uchunguzi wa kitabibu na kutoa ripoti inayotumika kama ushahidi mahakamani.
Ni muhimu kuripoti haraka ili daktari aweze kuona alama ambazo zinaweza kupotea baada ya muda.

2. Uchunguzi wa Kitabibu (Medical Examination)
Daktari huchunguza mhanga ili kubaini mambo yafuatayo kama ithibati ya kitendo:

Muingiliano (Penetration): Daktari hutafuta uthibitisho wa kuingiliwa kinyume na maumbile.
Majeraha (Bruises/Tears): Uwepo wa michubuko, michubuko ya tishu (tears), au uvimbe katika eneo la haja kubwa.
Vinasaba
(DNA/Spermatozoa): Utafutaji wa mabaki ya mbegu za kiume au majimaji ya mwili kwenye mwili wa mhanga au nguo zake.
 
Hivi ni mimi huwa na wenge au nilipevuka akili mapema

17&18 kwa kijana wa kiume ni mkubwa kabisa na wamefanyiwa vitendo zaidi ya mara moja na waliridhia. Mimi naona kuliko kuwakamata wanaofanya

Iangaliwe system kwa wafanyiwaji pia. Sioni kijana wa miaka 18 au fundi pikipiki wana utoto wa kusema huyo jamaa akamatwe peke yake. Kama act ni mbaya. Kamateni wote wote
 
Nawaza hapa kivyangu vyangu

1. Inawezekana mlawiti ameshindwa kutimiza malipo kwa wahusika, wameamua kulipua bomu (inawezekana hao wote walikuwa wanapigwa kwa mkopo, shetani naye si mjomba wake kaamua kumuabisha kwa wakati huo)

2. Hao wafirwaji ni wazoefu, wasingekuwa wazoefu wangetoa taarifa haraka sana ili mfiraji akamatwe

3. Inawezekana ukawa mtego wa kumharibia huyo

4. Au ikawa ndagu ya kulinda kazi yake (waganga wana mambo na vijimabo sana)

EPUKA YAFUATAYO

1. ewe mtu mzima, hv vitoto vya msingi na sekondary vinawashwa washwa sana, viko tayari kwa kila jambo hata kufirwa ili vipate chochote, na ukizingua vinakuzingua
-ukiona ksichana hukijui kinaanza kukuita ankoo naomba buku nikale, we kimbia huo ni mtego.

2. wazazi tujitahd kukaa na kuwapa amahtaj watoto wetu

3. wanaume punguzeni mazoea na vitoto hv kisa vina matiti na vinawaka mapaja yaani jela inakuita

KUHUSU HUYU MKUBWA (fund pkpk) ACHA AFIRWE TU AKILI ZIMKAE SAWA,
Ijapo sina imani kama kuna mtumishi wa umma hapo.
 
Hata kama ni kweli zaidi ya miezi mitatu anawalawiti alafu anakuja kukamatwa mwezi huu!

=======
Watu Watatu wakazi wa Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora wanadaiwa kulawitiwa na mtumishi wa halmashauri ya wilayani humo kwa nyakati tofauti.

Akizungumza na Mwananchi leo Aprili 12, 2026 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema wanaodaiwa kulawitiwa, wawili ni wanafunzi wa Shule ya Sekondari (17) na (18) na mmoja ni fundi pikipiki wilayani humo.

"Inadaiwa mtumishi huyu amekua akiwafanyia vitendo hivyo mara kadhaa hao wanafunzi pamoja na huyu fundi pikipiki ambaye ni mkazi pia wa hapo hapo Igunga," amesema Kamanda Abwao.

Amesema mtumishi huyo ambaye anafanya kazi halmashauri ya Igunga upande wa utawala na mkazi wa mtaa wa Stoo Igunga mjini, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Tabora kwa ajili ya mahojiano zaidi ikiwa ni pamoja na uchukuaji wa sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa kisayansi kwa pande zote mbili.

Amebainisha kuwa mbinu aliyokua akiitumia mtuhumiwa ni kuwarubuni na vitu tofauti na kuwapa fedha anapowahitaji.

"Tumefanya mahojiano ya awali na uchunguzi wa awali pia umefanyika, kuna baadhi ya vitu tumebaini lakini tunaendelea na uchunguzi kubaini tatizo zaidi ili tuweze kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria," amesema.

Amesema matukio hayo yanadaiwa kutekelezwa katika kipindi cha Desemba 2025 hadi Aprili 6 2026, katika nyakati tofauti na maeneo tofauti wilayani humo.

Kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi wa Tabora kuchukua tahadhari na kuacha kurubuniwa na vitu ambapo inapelekea kuharibu utu na heshima yao.

"Haiwezekani unakubali kirahisi kufanyiwa vitu vya ajabu na hutoi taarifa, unakuwa umeridhika tu na hela ndogo ambazo pia hazileti matokeo yoyote kwenye maisha yenu."

Amewahimiza wazazi na walezi kuhakikisha wanafanya ufuatiliaji wa karibu kwa watoto wao ili kubaini vitendo hivi kwa haraka vinapojitokeza, hasa ikizingatiwa vijana hao wawili ni wanafunzi wa kidato cha nne ni nguvu kazi ambayo inapaswa kurudi kuleta matokeo kwenye jamii.

"Lindeni watoto na wafuatilieni na mkiona mambo ambayo hamuyaelewi tupeni taarifa mapema tuchukue hatua, msisubiri mpaka tatizo liwe kubwa lakini pia msipende kumaliza kesi nyumbani kwa matukio kama haya," amesema Kamanda Abwao.

Chanzo: Mwananchi
Aisee! Laana
 
Polisi nendeni na pale CHINA PLAZA KARIAKOO vijana wengi wenye viflemu maeneo yale hawana marinda hata tembea yao utawaona kabisa mwendo wa kutia shaka WAOKOENI HAWA VIJANA
 
Back
Top Bottom