Inashangaza: Watu wanamuomba ruhusa Rais Magufuli, badala ya kupewa wanatumbuliwa

Inashangaza: Watu wanamuomba ruhusa Rais Magufuli, badala ya kupewa wanatumbuliwa

Huyu ni dikteta, Watanzania wana haki ya kuomba ruhusa kwa waajiriwa wao ili wakagombee nafasi yoyote ile ya uongozi na kama watashindwa wanaruhusiwa kurudi kwenye ajira zao bila matatizo lakini kwa kuwa kuna dikteta magogoni basi ndiyo hivyo tena.
Haiko hivyo Chief
Unaruhusiwa kutia nia ya kugombea ukiwa mtumishi
Ukichaguliwa tu na chama chako unaacha utumishi
Ukipata ubunge unaenda ,ukiukosa na kazi ndo ushakosa hivoo u cant come back
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kama ni kwa wale wanafasi za kuteuliwa na mimi namuunga mkono Magufuli, kwenda kuomba nafasi ya ubunge wakati wewe unajua kuwa Rais alikuteua kuwa RC, DC, IGP na nafasi zingine za kuteuliwa ni kumkosoa na kumdharau Rais kuwa alifanya makosa kukuteua katika nafasi ulionayo.

Nafasi yako ulitakiwa uwe mbunge au nafasi nyingine, kama sivyo basi walitakiwa wakatae mapema nafasi za kuteuliwa wabaki kwenye nafasi zao za awali au wasubiri kazi wanazoona zinawafaa wao.
Kwa ufupi nafasi za kuteuliwa na rais siyo permanent and pensionable! Hivyo hazina kusema eti ruhusa, ni kufukuzwa kazi then jina linatupwa otherwise kama ulikuwa teacher rudi huko
 
IMO that’s not fair and the end results is stupid people like Msukuma in parliament.

Haiko hivyo Chief
Unaruhusiwa kutia nia ya kugombea ukiwa mtumishi
Ukichaguliwa tu na chama chako unaacha utumishi
Ukipata ubunge unaenda ,ukiukosa na kazi ndo ushakosa hivoo u cant come back
 
Mkuu izi nafasi za kuteuliwa aliyekuteua anaweza kukutengua kulingana na kasi anayoihitaji kwenye serikali yake . Ualimu ni ajira ya kudumu ya utumishi wa umma kwa utaratibu ukiomba ruhusa bila malipo kwa mwajiri wako atakupa utaratibu wa kufuata.
Hivi unajua ata hiyo ajira ya ualimu barua ya kukutamburisha inatamka kua umeteuliwa nasi kwajiriwa?
 
Mkuu izo nafasi tayari wanazo wazifanyie kazi tu ili walete maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.ubunge waache na wengine ambao hawana nafasi wakatumikie wananchi. me nakuelewa Sana mh. Rais kwenye hili
Ndoto za mtu hazitawaliwi na mtu mwingine hata kwa maagizo...kila binadamu na ndoto zake ndugu yangu ,mfano n mdogo leo Magufuli anateua baadhi ya maaskari wanajeshi na mapolisi kwenye nafasi ambazo ni za kiraia (zamani watumishi kama walikuwa wakiteuliwa wakiwa wamekwisha staafu) ila siku hizi anateua wakiwa kazini hatukatai ila kwa nini na wao wasitumikie nafas walizonazo waachie wengine nafasi.

Magufuli alikuwa mwalimu Leo ni Rais angenyimwa ruhusa kwa kuondolewa kazini Leo angekuwa wapi...Kwa vile DED Das dc RC aliwateua wao ngoja awapangie cha kufanya.
 
Hivi karibuni Mh. Rais aliwapa ruksa baadhi ya wakuu wa mikoa, wilaya ma DED, RAS na DAS kwenda kwenye kinyang'anyiro cha kugombea ubunge na pia aliahidi Kuwapa ruksa wale wote wenye nia ya kwenda kugombea ubunge, lakini cha kushangaza baada ya tamko hilo baadhi ya wakuu wa mikoa wame piga breki na kusitisha nia zao za kugombea ubunge mmoja wao aliye jitokeza hadharani ni mkuu wa mkoa Mbeya.

Kwa maoni yangu kwa wale wote wenye nia ya kuuwania ubunge na wamesitisha kwa kuhofia kauli ya Rais ni bora Mh. Rais awaondoe wote wenye nia maana bila kufanya hivyo wakuu hao watakuwa kimwili katika nyadhifa hizo lakini kiroho watakuwa wanauwaza ubunge, ni vyema Rais akawarahisishia kazi ya kuwaondoa tu bila hata kusubiria maombi ya ruhusa zao, kwani kufuatia kauli yake wameamua kunyamaza ili yaishe lakini ukweli ni kwamba watakuwa wanafiki katika nafasi zao.

Maoni yangu ni bora kuwaondoa haraka ili wakawe huru, naamini wote wanafahamika. Ni bora kuwaondoa katika nafasi zao kuliko kuwaacha wakiwa kimwili wakati roho zao zinauwaza ubunge.
 
Afu ujue kabudi anapigiwa kampeni wazi wazi tena kwao kilosa, Baba wa kabudi alikaa Kilosa kama Mwinjilisti ndio jamaa kazaliwa kule lakini ni mgogo leo hii anaitwa mtu wa Kilosa na jimbo anapewa na hana hata kibanda pale anafikia hotel
Yani hawa wabunge wenye majimbo ya mawaziri wateule watulie tu wawe wapole wasubili teuzi zao mpya maisha yaendelee.

Ukijifanya mjuaji unaweza kosa bara na pwani [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Tujifunze kuona uzuri wa jambo katika kila hali.

Kwenye hili kuna uzuri wake mkubwa sana kwa pande zote!
 
Ameyafanya mengi yapi, mbona mie siyaoni? Hivi hujaona akina Kikwete walivyosambaza barabara nchi nzima?
Miaka mitano umeona barabara gani ya maana imejengwa
Hivi ni kweli hukumbuki wakti wa JK nambi yalivyokua hovyo?Tulikua na kila aina ya uchafu tangu EPA mpaka wenye ncho wkikua wanatutukana hata uliwa kituo cha polisi?Leo tunaheshimina,tulikua hatuna hata ndege,umeme ndio usiseme makampun yakilipwa mabilion hata bila kuzalisha umeme,makampuni ya kuchimba madini jinsi tulivyoingia mikataba ya ajabu ajabu inayofilisi nchi
Jaman kwan nyie wenzetu mwapofushwa na nini?
 


Nimejiuliza, Rais wetu mpendwa alipokuwa Mwalimu pale Sengerema Secondary School, alipoomba Ruhusa ya kwenda kugombea Ubunge kule Biharamulo. Je, aliachishwa kazi? Watu wanaomba ruhusa ili wakajaribu bahati zao, badala ya kupewa ruhusa wanatumbuliwa. Hii mnaionaje raia?

Binafsi naona sio sawa jamani au kwa vile ni nafasi za kuteuliwa? Najiuliza wale wa kwenye Sector zisizo za kuteuliwa i.e Watumishi wengine mfano walimu n.k wakiomba ruhusa nao wataachishwa kazi badala ya kupewa ruhusa. It means ukishindwa imekula kwako.

Hii ndo Tanzania ya Magufuli.

Ila wengine mumeumbwa muwepo tu kwa ajili ya kutoa lawama ,sasa hapo kosa lipo wapi?mnataka Mh raisi awafanye nini?
 
Nadhani miaka ya mwisho ya Mwinyi au mwanzoni mwa Mkapa lilitokea hilo pia, kipindi cha akina Mwanri wakiwa MaDC..
 
Ruhusa maana yake, ukirudi unarudi kwenye nafasi yako. Hapa naona wanatumbuliwa na wakishindwa kura za maoni maana yake imekula kwao.

Ni watashida au atawateua tena baadae. Ni kama watia nia wengi wanaofahamu hawatapata ubunge, ila wanataka Rais awe na info zao awateue mbeleni. Wamejua ameyatenda hayo tangu awe Rais.
 
Back
Top Bottom