KWELI Inashauriwa kumtahiri mtoto kati ya siku za mwanzoni hadi wiki ya 8 baada ya kuzaliwa

KWELI Inashauriwa kumtahiri mtoto kati ya siku za mwanzoni hadi wiki ya 8 baada ya kuzaliwa

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Wakuu

Nimeona hii mtu akiuliza huko nikawa curious pia kujua hili
photo_2026-05-19_09-59-35.jpg

1779178391419.png
 
Tunachokijua
Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani (WHO) wanaieleza Tohara (kutahiriwa) kwa mwanaume ni kitendo cha kutoa ama kukata sehemu au govi lote kutoka kwenye uume. Govi ni mwendelezo wa ngozi kutoka kwenye mlingoti wa uume ambao hufunika kichwa cha uume (glans penis) na tundu la mkojo (urethral meatus).

Ni muda gani sahihi wa kufanya Tohara

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia machapisho ya kisayansi yaliyoandikwa na wataalamu wa afya wanabainisha kuwa hakuna muda sahihi wa kufanya tohara ila inashauriwa ni vyema kufanya tohara mtu akiwa bado mtoto mchanga.

Tovuti ya medical point internationa l inaeleza kuwa Umri wa kutahiriwa ni moja ya mambo yanayoathiri hatari ya kupata matatizo yanayoweza kutokea wakati wa upasuaji. Ingawa hakuna umri maalum unaopendekezwa kimatibabu kwa ajili ya tohara, muda unaopendekezwa na madaktari ni ndani ya mwezi mmoja wa kwanza baada ya kuzaliwa.

Kituo cha tohara London, Uingereza wanaeleza kuwa mtoto mchanga ni kuanzia siku za mwanzoni baada ya mtoto kuzaliwa hadi kufikia wiki ya 8. Kwamba katikakipindi hiko mchakato unaweza kuwa rahisi zaidi, watoto wana asili ya kupona haraka zaidi na mara nyingi ganzi ya kienyeji kwenye eneo husika inaweza kutumika.

Kwanini kufanya tohara utotoni (uchanga) hupendekezwa zaidi kuliko hatua nyingine za utoto?

Kwa mujibu wa Kituo cha tohara London Sababu kuu ni pamoja na:
  • Govi na tishu zinazolizunguka kwa kawaida huwa laini na zinazovutika kwa urahisi zaidi.
  • Utaratibu wa tohara mara nyingi huchukua muda mfupi zaidi kwa watoto wachanga.
  • Ganzi ya eneo husika (local anaesthetic) kwa kawaida hufaa zaidi kutumika.
  • Kupona kwa kawaida huwa haraka zaidi kuliko kwa watoto wakubwa.
  • Watoto wachanga hawajishughulishi sana (hawajigeuzi au kutembea) wakati wa kipindi cha kupona.
  • Hatari ya kupata matatizo kwa ujumla huwa ndogo zaidi ikilinganishwa na watoto wakubwa.
  • Watoto wachanga hawana uelewa au kumbukumbu ya utaratibu huo kama walionayo watoto wakubwa.
Umuhimu wa wanaume kutahiriwa

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, miongozo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Kituo cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa (CDC), tohara huwa na faida nyingi kwa afya ya mwanamme mwenyewe, pamoja na mwanamke ambaye atashiriki naye tendo la ndoa.

  1. Tohara hupunguza nafasi ya kupata maambukizi ya mara kwa mara kwenye mfumo wa mkojo hasa kwa watoto wadogo.
  2. Hupunguza nafasi ya kuugua Saratani ya uume pamoja na magonjwa mengine ya zinaa hasa VVU/UKIMWI
  3. Hupunguza uwezekano wa kuugua saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake. Hii ni kutokana na ukweli kuwa mwanamme asiye tahiriwa huwa na uwezekano mkubwa wa kubeba Virusi vya Human papilloma kuliko yule aliyetahiriwa.
  4. Tohara husaidia pia kurahisisha suala la usafi kwa mwanamme.

Je, Tohara hupunguza ukubwa wa uume?

Tofauti na jinsi ambavyo watu wengi huamini, tohara haiwezi kudumaza afya ya sehemu za siri za mwanamme hata kama itafanyika kwa mtoto mchanga. Soma zaidi hapa ufuatiliaji wa JamiiCheck pia.

Ukuaji wa viungo vyote vinavyounda mwili wa binadamu huongozwa na mifumo rasmi iliyoshikizwa kwenye vinasaba vya urithi pamoja homoni mbalimbali za mwili.

Msingi wa taarifa hizi hauwezi kuathiriwa kwa kukata ngozi ya mbele inayofunika sehemu hizo.

Kama ambavyo mtu huzaliwa akiwa na asili ya urefu, ufupi, macho makubwa au kipara na asiwe na uwezo wa kuibadili asili hii, vivyo hivyo kwa ukubwa au udogo wa maungo haya muhimu kabisa kwa afya ya uzazi wa mwanamme kwa sababu kinacho ondolewa ni ngozi tu, siyo kichwa wala nyama ya sehemu hizo.
Duhh kwahiyo miaka 2 pia ni sawa au ndio viba100 vijavyo!🫢
 
tunajua kwamba mtoto anaetahiriwa akiwa bado mchanga kama alivosema Ntakuzibua kwamba anakuwa ana kibamia kweli kinakuwa kadogo.kwa makabila/jamii nyingi zinatahiri watoto wakiwa na umri wa miaka 4 hadi 12
Next kibamia in town. Miaka 6 mpaka 9 hapo freesh
Duhh kwahiyo miaka 2 pia ni sawa au ndio viba100 vijavyo!🫢
Kuanzia 2005 Kurud nyuma hakujawai kua na vibamia
Mwanangu atafanyiwa tohara akiwa na miaka 6 akiwa anajitambua angalau na nyie wengine endeleeni kuunda vibamia kwa watoto wenu
Mnafanya baadae wawe na vibamia mnawah wapi kutahiri watoto
Hii hoja ishapingwa humu JamiiCheck sijui huwa mnatoa wapi hizi imani. Ni kama ile imani kuwa kitovu kikidondokea uume wa mtoto anakua hanithi.

Ushahidi wa kisayansi unaonyesha ni genetiki na puberty (balehe) ndio inaathiri size ya uume not otherwise.
 
Hii hoja ishapingwa humu JamiiCheck sijui huwa mnatoa wapi hizi imani. Ni kama ile imani kuwa kitovu kikidondokea uume wa mtoto anakua hanithi.

Ushahidi wa kisayansi unaonyesha ni genetiki na puberty (balehe) ndio inaathiri size ya uume not otherwise.
😮‍💨
 
Wakuu,msithubutu kumtahiri mtoto mchanga au yeyote aliyechini ya miaka 15, ni heri mtoto akue na govi angalau akijitambua ndipo ataamua yeye mwenyewe kuwa atahili ama asitahili,kwa upande wangu nawalaumu mno wazazi wangu kwa kunitahili nikiwa sijitambui na nilikuwa sitaki kabisa kufanyiwa kitu kinaitwa tohara,na huwa najuta sana. Hivyo tohara ni hiari ya mtu si matakwa ya wazazi. NAMALA.
 
Angalau mtu awe 'Govinda' hadi miaka 15 kisha atahiriwe baada ya hapo, hii inasaidia mtu kutokuwa na kibamia ama kipilipili kichaa.
 
Mnafanya baadae wawe na vibamia mnawah wapi kutahiri watoto
Je, kwa kuwa umeweka hoja ya vibamia:
Naomba kufahamu kwa nchi yetu ipo katika watu wenye uumie mrefu duniani?
Na je Kuna uhusiano wa kuwa na kibamia na kutahiriwa mapema?
 
Je, kwa kuwa umeweka hoja ya vibamia:
Naomba kufahamu kwa nchi yetu ipo katika watu wenye uumie mrefu duniani?
Na je Kuna uhusiano wa kuwa na kibamia na kutahiriwa mapema?
Ebu nikuache uamini unachoamini
 
Angalau mtu awe 'Govinda' hadi miaka 15 kisha atahiriwe baada ya hapo, hii inasaidia mtu kutokuwa na kibamia ama kipilipili kichaa.
Huu ni uongo na misinformation. Why mnadanganya watu? Ishapingwa hii hoja na wataalamu kwa ushahidi wa kisayansi
 
Back
Top Bottom