INASIKITISHA: Makaburi Kinondoni yanavunjwa makusudi ili ipatikane nafasi ya kuzikia

INASIKITISHA: Makaburi Kinondoni yanavunjwa makusudi ili ipatikane nafasi ya kuzikia

Hapo kinachofanyika ni uhuni wa daraja la juu. Tulinunua eneo la kuzikia sh millioni 2, tukaambiwa tulipe laki 3 ya wachimbaji. Aisee kwenye kaburi la ndugu yangu ilifukuliwa mifupa ya mtu aliyezikwa zamani. Tukiwa tunazika, wachimbaji wakaomba waifukie mifupa ya yule marehemu wa Kwanza mle kaburini
Hamna kwenu? Mfano labda Mnasafirisha kuzika kijijini kwenye makaburi ya ukoo
 
Hamna kwenu? Mfano labda Mnasafirisha kuzika kijijini kwenye makaburi ya ukoo
Mi nshasema nikifa waniweke kwemye mkonge wa Serikali waingize wanangu wawili,baba na mdogo wangu wanipeleke kijijini kwetu..kama watashindwa kukodi gari!hapa mjini Mimi hapana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku sifa za mjini kuzikwa Kinondoni kiwanja cha kaburi milion kumi

Mkuu, hivi jeneza linachukua muda gani kuharibika kule chini ya kaburi?
Na mifupa inachukua muda gani kuharibika kabisa?




NB:
Aulizaye ataka kujua.
Kuuliza sio ujinga
 
Kuna siku nilienda msibani, sa wakati wa kuzika tukiwa makaburini sheikh akatoa speech

Akiwataka wanaozika ndugu zao kwenye makaburi ya eneo hilo waache mara moja tabia ya kujenga makaburi kwa cement, concrete au tiles

Maana eneo hilo limekwisha jaa hivyo kufanya hivyo unakua unazuia wengine washindwe kuzika ndugu zao, utaratibu uliopendekezwa ni kuzika bila kujenga ili siku za mbeleni mwingine apate nafasi ya kuzika juu yako

Aisee ningekuwepo hapo now ningekuwa nina kesi ya kumpiga huyo sheikh wenu
 
Back
Top Bottom