Inasikitisha Mtumishi wa Umma anafanyiwa Eviction kwa kushindwa kulipa Deni la kuuziwa Nyumba na TBA

Waatumishi wa umma ujanja wao ni kula rushwa na kupiga madili kazini ila kwenye mambo mengine hawana akili kabisa. Mtu unakopesheka hadi 50m kwanini usijenge nyumba yako badala ya kwenda kununua nyumba za TBA?
 
Swali la kujiuliza: Je,hao watumishi walilazimishwa?
 
Anaenunua nyumba TBA, anae nunua nyumba NSSF, NHC au Watumishi housing. Ni wa kumpepea, akili hana kabisa.
 
Serikali iwaonee huruma. Lakini na wao wanakaujinga fulani hivi.

Hao walikosa kuwa na kipaumbele. Walitakiwa, waache kufanya finishing kwanza na walipe deni baada ya kumaliza ndio waendelee na finishing.

Naona wao walikuwa wanajisemea tu, serikali haiwezi kutufukuza.

Kama nyumba zilikuwa semi finished ina maana zilikuwa zinakalika. Ilikuwa ni kuvuta umeme + maji na kiendelea kuishi huku wakilipa deni la Watu, yaani Watanzania.

Wao walianzaje kufanya finishing ya mamilioni ya pesa wakijua wanadiwa?
 
Hawa vijana wajinga achana nao.
 
Eti "serikali sikivu" umerogwa wewe, hakuna cha usikivu, watakusaidia ama kukusaidieni haswa wakiona ina kiki kwa maslahi yao ya kisiasa.
 
Kwa kawaida unapokopa nyumba unaonyesha mapato yako na unaelezea jinsi utakavyolipa kwa awamu ( mara nyingi kila mwezi) ili umalize deni lako. Unakubaliwa kukopeshwa pale inapoonekana kuwa kipato chako kinatosha wewe kulipa kwa awamu. Tatizo la wengi ni kuwa wakishalipa tu awamu chache za mwanzo wanaacha kulipa. Na hata wakikumbushwa hawalipi. Utamuongezeaje mtu muda ambae hata robo ya deni lake hajalipa? Badala ya kulalamika angesema aliuziwa kwa kiasi gani na alikuwa anadaiwa kiasi gani.

Watanzania wengi wanahamia kwenye nyumba ambazo zina milango ya nje tu na nondo kwenye madirisha. Choo cha shimo nje, maji ya kununua na taa ni za chemli. Inawachukua muda lakini wanamaliza. Huyu halipi deni anakimbilia finishes za bei mbaya ( hata hii sidhani kama amefanya).

Kama kweli anaitaka nyumba akope sehemu nyingine amalizane na TBA, ama sivyo TBA wataiuza, watakata wanachodai pamoja na gharama za kumtoa na zilizobaki watamrudishia.

Amandla...
 
Wao si wanavaaga ma tshirt yenye picha ya Mama na kusema anatosha na atawatosha kisawasawa
 
Kutukanwa nayo ni ajabu?

Tatizo ulisaini mmekubaliana terms and conditions

Shida inakuja wewe kutokutimiza your end of the bargain

Unakuja na visababu vya your own failure eti uachiwe....who the fvck will pay?

Eti Finishing,thats your preferences not the seller

Nakudhihaki sana unaleta upumbavu wa kutaka kurusha watu hela yao upewe nyumba bure....Hiyo nyumba ilitoka hewani?

TBA nao walikopa benki,wanadaiwa interests za ajabu halafu unakuja kuleta upumbavu eti usamehewe,hivi are you insane?

Agian,kama thinking yako ni ya namna hii kuomba nyumba za bure,nakutukana kwa mara ya pili!
 
Kuna watumishi wengine wanakaa nyumba chakavu na vidogo za serikali na hawalipi pia, ila wana apartments wamepangisha.
Sijui hawa tunawaweka kundi gani?
 
Sawa wakilipa zitaenda Mfukoni kwako. Na TBA ni taasisi ya Ukoo wako. Hayo yatapita na wewe Hapo TBA unapita tuuu. Usifanye Misiba ya Wenzako Kicheko na dhihaka zako. Be nice to people because you don't know the battle they are Fighting. Matusi yatakurudia one day
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…