Inasikitisha Mtumishi wa Umma anafanyiwa Eviction kwa kushindwa kulipa Deni la kuuziwa Nyumba na TBA

Waatumishi wa umma ujanja wao ni kula rushwa na kupiga madili kazini ila kwenye mambo mengine hawana akili kabisa. Mtu unakopesheka hadi 50m kwanini usijenge nyumba yako badala ya kwenda kununua nyumba za TBA?
Wanapenda kuishi kotaz kwani wewe unasemaje
 
Kwa nini mfanyakazi amekwenda kujitwisha mzigo asiyouweza?

Ulitakiwa upige mahesabu yako vizuri kabla ya kuchukuwa mkopio benki. Mfano hata mimi nilitaka kukopa semi finished house lakini baada ya kupiga mahesabu niliwaza hivi deni nitaweza kulilipa mimi? Nilimtafuta muhasibu anisaidie kukokotoa kiasi ambacho ningelipa (pamoja na riba) na nilishangaa kujikuta ningelipa deni labda mara mbili plus.... Nilijiondoa pole pole.
 
Nimeshangaa sana. Watumishi wa umma wana secure income. Walichotakiwa kukifanya ni kuongeza muda wa malipo. Kama wanavyofanya kwa wenzetu wangeweza kuongeza muda wa kulipa mkopo ( mortgage) uwe miaka 5, 10,15, 20,25. Muhimu kampuni zilizojenga
zinapata cash flow na kuzitumia kujenga nyumba zaidi.

Wengi wametumie pesa zao wenyewe kukamilisha ujenzi zilikuwa semi finished. Kimsingi nyumba zinaweza kuwa na thamani kubwa zaidi ya bei walizolipa kuzinunua. Kwahiyo wangeweza kutumia hata equity kupata mkopo mwingine.
 
Waatumishi wa umma ujanja wao ni kula rushwa na kupiga madili kazini ila kwenye mambo mengine hawana akili kabisa. Mtu unakopesheka hadi 50m kwanini usijenge nyumba yako badala ya kwenda kununua nyumba za TBA?
Na uzinzi...na mambo ya porini tu
 
Hakuna hata mmoja aliyekataa kulipa elewa hivyo. Walitaka Extension ya Mkataba waweze kumaliza Deni. Usitukane Watu hautapata Chochote kama Zawadi ya Matusi.
Wanataka "extension" na yeye TBA benki ampe "extension" kwa interest atakayolipa nani?

Eti "wanataka" extension,wanamtaka nani?

Mna vichaa nyie yaani mnajiangalia nyie tu na "maisha yenu"?

Yeye TBA nani amuangalie wakati kakopa hela zote hizo benki?

Eti "extension",halafu mpaka lini?Utaenda utarudi na ujinga ule ule!

Solution ni nzuri kabisa,TBA fanya repossession ya nyumba zote wakae bila nyumba uza kwa wengine!

Nyang'anya nguruwe hawa,hawana hela wanajitanua kuchukua nyumba wasizoziweza!

Takataka kabisa
 
Terms and conditions zilikuwa zinasemaje ?

Ndio hivyo mkuu the way of the world hakuna cha msalia mtume..., It's a Dog eat Dog World....
 
Mtu ukienda kukopa pesa benki kwa ajili ya kununulia gari watakupa masharti yao ya kukupa huo mkopo. Benki haitakusamehe deni kama ikitokea gari litapata ajali kabla haujamaliza deni. Aidha, wakopeshaji wanaangalia historia yako ya kulipa deni lao kabla hawajafikia uamuzi wa kukuevict kwenye nyumba. Mathlani ulikuwa mlipaji mzuri kwa miaka mitano ya miaka 6 ya deni halafu likakupata jambo wanakuwa tayari kukaa na wewe ili kuangalia namna gani utaweza kumaliza hilo deni. Ukiona mtu anakuwa evicted ujue huyo ni mdaiwa sugu na mdai uvumilivu umemuisha.

Watu wengi wanakosea wanapoangalia deni la nyumba. Wengi hawaangalii thamani ya nyumba ya sasa na ya hapo baadae. Nyumba za TBA zinajengwa katika maeneo ambayo yamepimwa na kupangwa na hivyo miaka inavyozidi kwenda thamani ya kiwanja peke yake inaongezeka. Maeneo kama Sinza yalilengwa kwa watu wa kipato cha chini. Msasani zilijaa nyumba za udongo na lilikuwa eneo la mamwinyi. Watu walionunua nyumba kwenye kijiji cha ujamaa cha Mwenge walishinda bingo.

Aidha, kwa kulipa pole pole kunakuachia pesa ambayo unaweza kutumia kuzalisha pesa zitakazokusaidia kulipia deni. Unaweza kupangisha chumba ili umalize deni. Wengine wamepangisha nyumba nzima na kutumia pesa wanayopata kulipia deni. Wote hawa kipaumbele chao kilikuwa ni kulipa deni na sio kutambia jamii. Kuna kitu cha kujifunza hapa.

Amandla...
 
Moja wapo ya mifano mingi katika nchi hii kufanyika bila uhalisia. Mkopo nyumba 50m mshahara laki 6-8, bado mtu hajaishi na familia, katika uhalisia ni kitu ambacho hakipo. Hiyo ela ya marejesho/makato si mtu angejenga kibanda chake, na una kuta mtumishi akishindwa kumalizia mkopo marejesho yake yanachukuliwa kirahisi tu, yaani huu ni wizi/ujambazi mchana kweupe
 
Sijaona kosa la TBA
Kama huna uwezo acha kuchukua ambavyo vipo juu ya uwezo wake

Haya mambo ya kutia huruma ni ujinga mkubwa
 
Kama kipato chako si kikubwa kwa nn uingie huo mkopo?
 
Huu ulimwengu wa kipebari...mwendo wa mikataba tu, huruma kwa mama yako..
Unakopa 50m unaenda fanya finishing...are you mad?
 
Hajakopa 50 milioni. Anadai ametumia 50 milioni kumalizia nyumba! Hapo ndio naona anatupiga mchanga wa uso maana hizo pesa bila shaka zingetosha kulipia deni.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…