Inasikitisha Mtumishi wa Umma anafanyiwa Eviction kwa kushindwa kulipa Deni la kuuziwa Nyumba na TBA

Inasikitisha Mtumishi wa Umma anafanyiwa Eviction kwa kushindwa kulipa Deni la kuuziwa Nyumba na TBA

Waatumishi wa umma ujanja wao ni kula rushwa na kupiga madili kazini ila kwenye mambo mengine hawana akili kabisa. Mtu unakopesheka hadi 50m kwanini usijenge nyumba yako badala ya kwenda kununua nyumba za TBA?
Wanapenda kuishi kotaz kwani wewe unasemaje
 
Watumishi hawa wamejikuta Wana mizigo mikubwa ya KuService deni la Nyumba la kufanyia Nyumba finishing ili iweze kukalika mikataba ukaisha deni bado kulipika. Wamejaribu kujieleza kuomba mikataba mingine TBA imekataa Kwa kupewa Nguvu na Waziri wa Ujenzi wafukuzwe.

Hivi mpaka itokee Aibu ya kufukuza Watumishi Kwa kushindwa kulipa ndani ya Mikataba Kwa nini Serikali isiwasikilize Watumishi hawa? Ni Huzuni Sana kumfanyia Mtumishi au Mstaafu aliepewa mafao ya Kikokotoo unyama huu. Serikali ni Sikivu iwasikilize Wadaiwa wake Kwa kuwa hakuna aliyefanya makusudi kutomaliza Deni.
Kwa nini mfanyakazi amekwenda kujitwisha mzigo asiyouweza?

Ulitakiwa upige mahesabu yako vizuri kabla ya kuchukuwa mkopio benki. Mfano hata mimi nilitaka kukopa semi finished house lakini baada ya kupiga mahesabu niliwaza hivi deni nitaweza kulilipa mimi? Nilimtafuta muhasibu anisaidie kukokotoa kiasi ambacho ningelipa (pamoja na riba) na nilishangaa kujikuta ningelipa deni labda mara mbili plus.... Nilijiondoa pole pole.
 
Kitu ambacho nimejifunza sector ya nyumba ni muhimu sana kama driving force ya uchumi.

Ukienda nchi za wenzetu (private debt) 90% ni mortgages. Sisi kwetu private debt sehemu kubwa ni mikopo ya wafanyakazi (consumption loan).

Very bad how kuekezea hadithi yake kwanini ‘vice versa’ ya consumer loans kuwa kubwa kushinda secured loans ni hadithi ndefu.

Fanya research yako ya private debt duniani uwezi kukuta ‘consumer loan’ ni kubwa kushinda secured loan.

Kuelezea sasa mpaka haya mapoyoyo ya serikali ya elewe ndio mtihani; Lakini sasa kuna watanzania wakurugenzi wa bank na financiers.

Unaweza wale walio kwenye banks kutojali hiyo tofauti mradi kwao kuna faida ya consumer loan (maana it’s very much secure) kwakuwa serikali inatoa guarantee ya mishahara ya wafanyakazi.

Why would they want to risk in actual secure loans for cheap at 5% interest, jumlisha na akili za TBA na NHC kwenye kupambana wananchi wamiliki nyumba.

Tanzania inaongozwa na watu wajinga sana wasio na uwezo.

Mtu pekee mwenye akili ni Dorothy Gwajima tu.
Nimeshangaa sana. Watumishi wa umma wana secure income. Walichotakiwa kukifanya ni kuongeza muda wa malipo. Kama wanavyofanya kwa wenzetu wangeweza kuongeza muda wa kulipa mkopo ( mortgage) uwe miaka 5, 10,15, 20,25. Muhimu kampuni zilizojenga
zinapata cash flow na kuzitumia kujenga nyumba zaidi.

Wengi wametumie pesa zao wenyewe kukamilisha ujenzi zilikuwa semi finished. Kimsingi nyumba zinaweza kuwa na thamani kubwa zaidi ya bei walizolipa kuzinunua. Kwahiyo wangeweza kutumia hata equity kupata mkopo mwingine.
 
Waatumishi wa umma ujanja wao ni kula rushwa na kupiga madili kazini ila kwenye mambo mengine hawana akili kabisa. Mtu unakopesheka hadi 50m kwanini usijenge nyumba yako badala ya kwenda kununua nyumba za TBA?
Na uzinzi...na mambo ya porini tu
 
Hakuna hata mmoja aliyekataa kulipa elewa hivyo. Walitaka Extension ya Mkataba waweze kumaliza Deni. Usitukane Watu hautapata Chochote kama Zawadi ya Matusi.
Wanataka "extension" na yeye TBA benki ampe "extension" kwa interest atakayolipa nani?

Eti "wanataka" extension,wanamtaka nani?

Mna vichaa nyie yaani mnajiangalia nyie tu na "maisha yenu"?

Yeye TBA nani amuangalie wakati kakopa hela zote hizo benki?

Eti "extension",halafu mpaka lini?Utaenda utarudi na ujinga ule ule!

Solution ni nzuri kabisa,TBA fanya repossession ya nyumba zote wakae bila nyumba uza kwa wengine!

Nyang'anya nguruwe hawa,hawana hela wanajitanua kuchukua nyumba wasizoziweza!

Takataka kabisa
 
Terms and conditions zilikuwa zinasemaje ?

Ndio hivyo mkuu the way of the world hakuna cha msalia mtume..., It's a Dog eat Dog World....
 
Mtu ukienda kukopa pesa benki kwa ajili ya kununulia gari watakupa masharti yao ya kukupa huo mkopo. Benki haitakusamehe deni kama ikitokea gari litapata ajali kabla haujamaliza deni. Aidha, wakopeshaji wanaangalia historia yako ya kulipa deni lao kabla hawajafikia uamuzi wa kukuevict kwenye nyumba. Mathlani ulikuwa mlipaji mzuri kwa miaka mitano ya miaka 6 ya deni halafu likakupata jambo wanakuwa tayari kukaa na wewe ili kuangalia namna gani utaweza kumaliza hilo deni. Ukiona mtu anakuwa evicted ujue huyo ni mdaiwa sugu na mdai uvumilivu umemuisha.

Watu wengi wanakosea wanapoangalia deni la nyumba. Wengi hawaangalii thamani ya nyumba ya sasa na ya hapo baadae. Nyumba za TBA zinajengwa katika maeneo ambayo yamepimwa na kupangwa na hivyo miaka inavyozidi kwenda thamani ya kiwanja peke yake inaongezeka. Maeneo kama Sinza yalilengwa kwa watu wa kipato cha chini. Msasani zilijaa nyumba za udongo na lilikuwa eneo la mamwinyi. Watu walionunua nyumba kwenye kijiji cha ujamaa cha Mwenge walishinda bingo.

Aidha, kwa kulipa pole pole kunakuachia pesa ambayo unaweza kutumia kuzalisha pesa zitakazokusaidia kulipia deni. Unaweza kupangisha chumba ili umalize deni. Wengine wamepangisha nyumba nzima na kutumia pesa wanayopata kulipia deni. Wote hawa kipaumbele chao kilikuwa ni kulipa deni na sio kutambia jamii. Kuna kitu cha kujifunza hapa.

Amandla...
 
Moja wapo ya mifano mingi katika nchi hii kufanyika bila uhalisia. Mkopo nyumba 50m mshahara laki 6-8, bado mtu hajaishi na familia, katika uhalisia ni kitu ambacho hakipo. Hiyo ela ya marejesho/makato si mtu angejenga kibanda chake, na una kuta mtumishi akishindwa kumalizia mkopo marejesho yake yanachukuliwa kirahisi tu, yaani huu ni wizi/ujambazi mchana kweupe
 
Sijaona kosa la TBA
Kama huna uwezo acha kuchukua ambavyo vipo juu ya uwezo wake

Haya mambo ya kutia huruma ni ujinga mkubwa
 
Hiki ni cha Serikali. Watumishi ni wa Serikali. Vipato vya Watumishi wao wanavijua. Unamfukuzaje badala ya kumsikiliza?? Serikali Sikivu ni ipi ikiwa hata kuongeza Mkataba hawasililizi? Unamfukuzaje Mtu ilihali ana nia ya kulipa? Haya yalitokea Ubungo Plaza Blue Pearl 2016 Hadi Leo jengo halina matumizi na Kodi hailipwi.
Kama kipato chako si kikubwa kwa nn uingie huo mkopo?
 
Huu ulimwengu wa kipebari...mwendo wa mikataba tu, huruma kwa mama yako..
Unakopa 50m unaenda fanya finishing...are you mad?
 
Moja wapo ya mifano mingi katika nchi hii kufanyika bila uhalisia. Mkopo nyumba 50m mshahara laki 6-8, bado mtu hajaishi na familia, katika uhalisia ni kitu ambacho hakipo. Hiyo ela ya marejesho/makato si mtu angejenga kibanda chake, na una kuta mtumishi akishindwa kumalizia mkopo marejesho yake yanachukuliwa kirahisi tu, yaani huu ni wizi/ujambazi mchana kweupe
Hajakopa 50 milioni. Anadai ametumia 50 milioni kumalizia nyumba! Hapo ndio naona anatupiga mchanga wa uso maana hizo pesa bila shaka zingetosha kulipia deni.

Amandla...
 
Back
Top Bottom