Inasikitisha na kuhuzunisha sana jinsi 'plants' za madini zinavyohatarisha maisha ya watu

Inasikitisha na kuhuzunisha sana jinsi 'plants' za madini zinavyohatarisha maisha ya watu

Mkuu umeongea ukweli kabisa
Ni ukweli na nina uchungu sana pia kwa sababu hata mimi nimeishampoteza mtu wangu wa karibu[emoji24] kutokana na cancer na kwa maelezo yale tuliopewa nimegundua kabisa ni athari za hizo kemikali.
 
Kiujumlau hakuna sehemu salama kwenye huu ulimwengu na siwalaumu hao vijana maana wanajitafutia mkate wao kutokana na tatizo la ajira na ukosefu wa elimu juu ya kazi husika na hizo ni ajali tu.
Tukirudi kwenye hizo plants ni kwamba kazi hazifanywi kwa utaratibu unaoweza kumkinga mfanyakazi na madhara ya sumu na kemikali tofauti tofauti.
Kwa mamlaka zinazohusika huwa zinaenda kukagua tu kama kutimiza ratiba zao, na ikitokea kila plant ikaguliwe kama inafuata kanuni na sheria amini asilimia 95 zitafungwa, hivyo hata mamlaka inafanya fair tu ila hutokea mara chache plant flani kuwekewa vizuizi ili kuwa mfano na waonekane wamefanya kazi.
Kuhusu hiyo Conc Sulphuric acid kule plant huwa haina matumizi yeyote hapo umetupiga na kitu kizito, kule huwa wanatumia Hydrochloric acid na Nitric acid, hiyo Sulphuric inatumiwa Elution.
 
Mimi concern yangu kubwa ni usalama wao, vifaa hawapewi, kuhusu suala la degree hata kama mtu kakariri uelewa wake ni mkubwa kuhusu kitu anachokifanyia kazi kwa sababu tayari angalau ana basics, tofauti na mtu anayefundishwa tu kazi, hajuhi basics za kile anachokifanyia kazi.
Acha uongo. Basics ndio nini? Unajua aina za elimu? Una kitu kinaitwa on job training? Umekariri elimu hadi ukae darasani miaka minne? Pole sana.

Kuna mafundi wazuri wamejifunzia gereji tu na wanapiga kazi kuliko hata hao wa darasani.

Kwa taarifa yako kwa Tanzania mfumo wa darasani ni tofauti na mazingira halisi.

Karibu mtaani.
 
Kiujumlau hakuna sehemu salama kwenye huu ulimwengu na siwalaumu hao vijana maana wanajitafutia mkate wao na hizo ni ajali tu.
Tukirudi kwenye hizo plants ni kwamba kazi hazifanywi kwa utaratibu unaoweza kumkinga mfanyakazi na madhara ya sumu na kemikali tofauti tofauti.
Kwa mamlaka zinazohusika huwa zinaenda kukagua tu kama kutimiza ratiba zao, na ikitokea kila plant ikaguliwe kama inafuata kanuni na sheria amini asilimia 95 zitafungwa, hivyo hata mamlaka inafanya fair tu ila hutokea mara chache plant flani kuwekewa vizuizi ili kuwa mfano na waonekane wamefanya kazi.
Kuhusu hiyo Conc Sulphuric acid kule plant huwa haina matumizi yeyote hapo umetupiga na kitu kizito, kule huwa wanatumia Hydrochloric acid na Nitric acid, hiyo Sulphuric inatumiwa Elution.
Ni kweli zitafungwa, lakini bhasi waonyeshe jitihada watu wanapata shida Sana. Kuhusu conc. hcl nahisi umekariri, unaweza kutumia conc sulfuric acid au hcl itategemea na limiting reagent na racimics za unachotaka kupata. Na hili uitumie conc sulfuric acid in elution inabidi isiwe ni small molecules, ikiwa ni small molecules it will not work effectively.
 
Acha uongo. Basics ndio nini? Unajua aina za elimu? Una kitu kinaitwa on job training? Umekariri elimu hadi ukae darasani miaka minne? Pole sana.

Kuna mafundi wazuri wamejifunzia gereji tu na wanapiga kazi kuliko hata hao wa darasani.

Kwa taarifa yako kwa Tanzania mfumo wa darasani ni tofauti na mazingira halisi.

Karibu mtaani.
Naona unaleta mada nyingine kabisa tofouti na lengo la uzi. Sitaki tuendeleze huu mjadala wako, tufanye umeshinda. Alafu hata kama hujaenda shule usiwachukie waliosoma, mbona wasomi uwa hawawachukii ambao hawajasoma.
 
Kiukweli nilibahatika kutembelea jumla ya plants za madini 9, tatu kahama Shinyanga na 6 wiliya ya Bukombe Geita. Nilichokiona na kukishuhudia kwenye plants hizo ni cha kuhuzunisha na kusitikisha Sana haswa kuhusu afya za watu walioajiriwa kwenye hizo plants na wanaoishi kuzunguka hizo plants.

Plants hizo ambazo zinajihusisha na uchenjuaji wa dhahabu kutoka kwenye mchanga au mawe ni za watu wenye kipato cha Kati na cha juu, ili kuendesha plants hizo, wataalamu mbalimbali wa kusimamia na kuendesha shughuli hiyo uhitajika.

Jinsi gani zinahatarisha afya za watu, niligundua baadhi ya mambo kama ifuatavyo

Kwanza
Wataalamu walioajiriwa ni unprofessional, hawana taaluma ya kile wanachokifanyia kazi. Hapa nitatolea mfano wakemia wanaotumika kupima na kuandaa kemikali zinazohitajika Kwa ajili ya uchenjuaji, cha kwanza kabisa katika plants zote hizo ni plant moja tu iliyokuwa na mkemia ambaye ni professional(na huyo anasema ndiye anaye wafundisha vijana) , zilizobaki ni vijana wanachukuliwa mtaani na kufundishwa jinsi ya kupima na kuandaa hizo kemikali, vijana hawa kwa sababu hawana ujuzi zaidi kuhusu hiyo taaluma wanajikuta wakifanya kazi katika mazingira magumu sana.

Vijana wanaingia maabara bila vifaa maalumu vya kujikinga na kumwagikiwa au kudondokewa na sumu hizo za kemikali, katika hali ya kustahajabisha vijana hawa ushika kemikali kwa mikono na vifaa vya kemikali bila kujali, hapa ndipo wanajikuta katika matatizo ya kiafya kwani nilishuhudia baadhi yao wakikohoa damu, kucha kuchomoka, nywele kuungua, ngozi kubabuka n.k, baada ya kuwauliza Kwa nini jibu lilikuwa ni sisi "tumeshazoea haya ndiyo maisha yetu, tunajua tutakufa"[emoji24]. Hii ni kwa sababu maabara hazikizi viwanga na ukosefu wa maarifa kuhusu good laboratory practices na laboratory safety.

Wakati nikiwa Bukombe, sehemu moja inaitwa namba moja, kuna plant moja kijana alikuwa anachanganya conc. Sulfuric acid kwa bahati mbaya sijuhi alikosea nini, kutokana na kuvuta hewa yake kwa sababu moshi ulitanda chumba kizima, alipiga kelele na kuomba msaada, wakati anatolewa kupelekwa kituo cha afya alisema hivi "siwezi kuona", kituoni aliambiwa sumu aliyovuta hawaiwezi ikabidi apelekwe hospitali ya wilaya Bukombe, kiukweli mpaka natoka kule kijana niliacha hajaweza kuona tena.

Pili
Uchafuzi wa vyanzo vya maji vinavyozunguka plants hizo, hapa ndipo kuna hatari kubwa sana ya watu wa kanda ya ziwa kupata cancer, kwani plants hizo hazina wataalamu wenye utaalamu wowote kuhusu "chemical speciation" na "waste management", hivyo hawajuhi chochote kuhusu bioconcentration, bioaccumulation concepts , hivyo kemikali hizo baada ya kuzifanyia treatment uzitoa kwenye mantenki na kwenda kuzitupa bila utaratibu, kwahiyo kemikali hizo utiririka hadi kwenye vyanzo vya maji kama mito na visima ,hali hii inapelekea maji wanayotumia kutoka kwenye visima na samaki kutoka kwenye mabwawa na hiyo mito kuwa na kiasi kikubwa cha kemikali hizo zenye sumu.
.
Pamoja na kwamba ni uchimbaji mdogo, lakini unahitaji utaalamu na usimamizi pia, wamiliki wa plants wanapata pesa nyingi, lakini hawajali kabisa kuhusu afya za watu, NEMC pamoja na ofisi ya mkemia mkuu mkuu wa serikali (GCLA) kwa kushirikiana na wizara ya madini chini ya serikali mnao wajibu wa kusimamia hili ili kuwanusuru watu kutokana na hizo sumu za kemikali.

Najua kuna rushwa kubwa sana kule, Ila wekeni nguvu, vijana mikono, miguu inatoboka tu[emoji24], huku wenye plants wakivuna pesa.
Mkuu yaani hili ni janga kubwa sana kitaifa. Nadhani watu wa NEMC wanakula rushwa kubwa mno. Mi kuishi mikoa inayochimba madini ni no kubwa.
 
Kuna mda nilikua mwz
Kuna mda unaoga maji ya bomba unashangaa ngozi inababuka au gafla unakua mweupe nilishangaa inawezekana hata maji ya hilo ziwa yako concetrated😦😦😦😦
 
Mkuu sidhan Kama umefanya tafiti sahihi kwasbb moyo wa plant wote utegemea mkemia. Mkemia fake si kuleta madhara kwa watu tu, Bali kuleta hasara kubwa kwa kutosababisha dhahabu ikamatwe kwenye cabon.

Kwa mmiliki wa plant au mtu aliyepeleka rundo kuozesha hawez kuwa na mkemia fake maana atajua yuko hatarin kupata hasara.

Jambo lingine zile kemikali ni hatari Sana kwa binadam na wanyana na hata mimea. Mfano sayanaidi ni sum mbaya, sidhan Kama kweli mtu anachezea maisha yake kijinga jinga.

Kama hiyo haitoshi sehem ya kujenga plant serikali kupitia watu wa mazingira NEMK, wako Makin Sana kutoa vibali haswa kwa kuangalia yale maji ya shimo la sumu.

So nakubaliana na wewe kwa kias kidogo, siyo plant zote Zina hatarisha maisha, uenda ni uko Kanda ya ziwa tu. Unaweza kwenda Kanda ya kati mfano pale dodoma kule NHOLI, plant zote ziko na wataalam na Serikali inasimamia usalama wa watu kwa ukaribu sana.
 
Mkuu unachosema ni kweli watu wenye plant na elution wengi wao wanajali hela tu na hawana muda wa kufuatilia afya za wafanyakazi wao, kweny field ya mining industry unaweza kujifunza vitu vingi je tujiulize hata baada ya kujifunza na kuwa skilled suala la usalama na afya za wafanyakazi zinazingatiwa? Jibu ni hapana lakini pamoja na hizi plant na elution kutoa pesa nyingi kwa serikali lakini ni kama serikali hawana muda wao wanacho jari ni kodi tu hii ni tofauti na nchi nyingine kama South Africa na Botswana
 
Mkuu yaani hili ni janga kubwa sana kitaifa. Nadhani watu wa NEMC wanakula rushwa kubwa mno. Mi kuishi mikoa inayochimba madini ni no kubwa.
Na kitu kingine baadhi ya maeneo yapo remote areas, kwahiyo serikali mara nyingi haina muda na hizo sehemu, tofauti na kama ingekuwa ni maeneo ya mijini.
 
Mkuu sidhan Kama umefanya tafiti sahihi kwasbb moyo wa plant wote utegemea mkemia. Mkemia fake si kuleta madhara kwa watu tu, Bali kuleta hasara kubwa kwa kutosababisha dhahabu ikamatwe kwenye cabon.

Kwa mmiliki wa plant au mtu aliyepeleka rundo kuozesha hawez kuwa na mkemia fake maana atajua yuko hatarin kupata hasara.

Jambo lingine zile kemikali ni hatari Sana kwa binadam na wanyana na hata mimea. Mfano sayanaidi ni sum mbaya, sidhan Kama kweli mtu anachezea maisha yake kijinga jinga.

Kama hiyo haitoshi sehem ya kujenga plant serikali kupitia watu wa mazingira NEMK, wako Makin Sana kutoa vibali haswa kwa kuangalia yale maji ya shimo la sumu.

So nakubaliana na wewe kwa kias kidogo, siyo plant zote Zina hatarisha maisha, uenda ni uko Kanda ya ziwa tu. Unaweza kwenda Kanda ya kati mfano pale dodoma kule NHOLI, plant zote ziko na wataalam na Serikali inasimamia usalama wa watu kwa ukaribu sana.
Kaka kanda ya ziwa kuna shida sana kwenye issue za plant na elution suala la usalama na hata utunzaji wa chemical zinazotumika kuna shida kidgo japo siyo sehemu zote, kweny suala la mkemia hapa tukubaliane kwamba tanzania wakemia wa masuala ya madini wapo ila lazima tupate wakemia bora ili kupata faida nzuri tatzo ni kwamba hao pia wapo ila ni wachache sana, na ni kama serikali haijawekeza sana kwao na kwa watu wenye plant na elution hasa kwenye suala la elimu ya afya za watu, utunzaji wa mazingira na kuwa updated kila mara
 
Mkuu sidhan Kama umefanya tafiti sahihi kwasbb moyo wa plant wote utegemea mkemia. Mkemia fake si kuleta madhara kwa watu tu, Bali kuleta hasara kubwa kwa kutosababisha dhahabu ikamatwe kwenye cabon.

Kwa mmiliki wa plant au mtu aliyepeleka rundo kuozesha hawez kuwa na mkemia fake maana atajua yuko hatarin kupata hasara.

Jambo lingine zile kemikali ni hatari Sana kwa binadam na wanyana na hata mimea. Mfano sayanaidi ni sum mbaya, sidhan Kama kweli mtu anachezea maisha yake kijinga jinga.

Kama hiyo haitoshi sehem ya kujenga plant serikali kupitia watu wa mazingira NEMK, wako Makin Sana kutoa vibali haswa kwa kuangalia yale maji ya shimo la sumu.

So nakubaliana na wewe kwa kias kidogo, siyo plant zote Zina hatarisha maisha, uenda ni uko Kanda ya ziwa tu. Unaweza kwenda Kanda ya kati mfano pale dodoma kule NHOLI, plant zote ziko na wataalam na Serikali inasimamia usalama wa watu kwa ukaribu sana.
Mimi hayo maeneo niliyoyataja nimefika kabisa, vijana wanapewa training, then wanakabidhiwa mzigo na wanashika dhahabu vizuri tu, Ila shida ni kwenye usalama hapo ndipo penye shughuli kwelikweli. Na plants nyingi zinatumia wakemia feki, na dhahabu wanapata, lakini usalama ni hatari tupu.
 
Kwa suala kama hili kuna haja OSHA kwenda katika hizo plants ili watoe ripoti ifanyiwe kazi, maisha ya mfanyakazi ni muhimu sana kwake, familia yake na taifa kwa ujumla
 
Mkuu unachosema ni kweli watu wenye plant na elution wengi wao wanajali hela tu na hawana muda wa kufuatilia afya za wafanyakazi wao, kweny field ya mining industry unaweza kujifunza vitu vingi je tujiulize hata baada ya kujifunza na kuwa skilled suala la usalama na afya za wafanyakazi zinazingatiwa? Jibu ni hapana lakini pamoja na hizi plant na elution kutoa pesa nyingi kwa serikali lakini ni kama serikali hawana muda wao wanacho jari ni kodi tu hii ni tofauti na nchi nyingine kama South Africa na Botswana
Ni kweli na kiukweli pesa ni tamu kwa kila mtu, lakini hata wafanyakazi wa hizo plants ni kama hawana habari na afya zao na wameshakubali matokeo.
 
Ni ukweli na nina uchungu sana pia kwa sababu hata mimi nimeishampoteza mtu wangu wa karibu[emoji24] kutokana na cancer na kwa maelezo yale tuliopewa nimegundua kabisa ni athari za hizo kemikali.
Nishawahi kutembelea hizo plants mpaka ellusion ambapo ndio final stage ya process ya kupata dhahabu

Kwanza siku niliyofika nikiwa geti la kwanza kabisa huku karibia na barabara nikaribishwa na harufu kali ya cyanide.

Kufika ndani nikakutana na vijana wanacheza draf wengine wanakula nguna hawana habari na ile harufu wakati huo mimi nimevaa mask na bado nimeshikila pua at the same time

Kuingia geti la pili nikakutana na kesi, ng'ombe za wasukuma zilikunywa maji ya mto ambayo yalikua contaminated na sumu za plant. Ng'ombe kama 15 zimedanja wasukuma wamekuja kuweka bunge wanataka walipwe

Mmiliki wa plant alikua na mkwanja, akawanyamazisha wale wasukuma wakasepa.

Tulizunguka maeneo ya mle ndani tukagundua kuna vijana wengi sana ambao wameajiriwa kwa ajili ya kuopoa mchanga kwenye tanks ambazo wanachanganyia hizo sumu hii kazi imebatizwa kwa jina la chepe

Mazingira ya kiusalama kiukweli ni mabovu sana, wale vijana hawapewi vizuizi vya kujikinga na sumu na wao wanaona freshi tu as long as wanalipwa on time

Kwenye yale matank ya michanga nilishuhudia kuona vitu vingi vyenye kuashiria hatari ya ile kazi na kufikiria kwamba ilikua ni kazi iliyopaswa ifanywe na maroboti na sio watu.

Ile harufu ya ile sumu kwenye zile tanks ilikua ikivutia sana wadudu na ndege, kuna zile ndege ambazo zinaruka juu na kushuka chini ya maji kisha kunywa maji bila kutua zikiwa zina hang angani, hizi nimeshuhudia kwa macho yangu zikishuka na kudonoa yale maji na kuanguka hapo hapo yani hata kufurukuta hakupo
 
Back
Top Bottom