Mkuu sidhan Kama umefanya tafiti sahihi kwasbb moyo wa plant wote utegemea mkemia. Mkemia fake si kuleta madhara kwa watu tu, Bali kuleta hasara kubwa kwa kutosababisha dhahabu ikamatwe kwenye cabon.
Kwa mmiliki wa plant au mtu aliyepeleka rundo kuozesha hawez kuwa na mkemia fake maana atajua yuko hatarin kupata hasara.
Jambo lingine zile kemikali ni hatari Sana kwa binadam na wanyana na hata mimea. Mfano sayanaidi ni sum mbaya, sidhan Kama kweli mtu anachezea maisha yake kijinga jinga.
Kama hiyo haitoshi sehem ya kujenga plant serikali kupitia watu wa mazingira NEMK, wako Makin Sana kutoa vibali haswa kwa kuangalia yale maji ya shimo la sumu.
So nakubaliana na wewe kwa kias kidogo, siyo plant zote Zina hatarisha maisha, uenda ni uko Kanda ya ziwa tu. Unaweza kwenda Kanda ya kati mfano pale dodoma kule NHOLI, plant zote ziko na wataalam na Serikali inasimamia usalama wa watu kwa ukaribu sana.