Inasikitisha na kuhuzunisha sana jinsi 'plants' za madini zinavyohatarisha maisha ya watu

Hilo nalo ni tatizo, kuna baadhi ya watu wanafanya biashara ya madini igeuke ya umafia kwa mambo kama haya.
 
Hii nayo ngumu kumeza, pamoja na ugumu wa maisha tulionao watanzania wenzangu bado uhai ni kitu cha thamani sana

Unakubalije kuingia Plant area bila PPE?
Kama wanaweza kula maandazi, chapati , vitumbua vilivyolowana maandishi ya magazeti nini kushika kemikali
 
kama mnajadiri matajiri wakubwa na sie tulio ktk makarasha ya kawaida mnatusaidiaje me niko chunya ila maisha ya kuendesha mitambo mbona poa tu
 
Dunia imeamua hivyo acha tuangamie. Hata maabara za kisasa hatari ipo palepale. Cha msingi mshauri mtoto wako asiende kuganta kazi hayo maeneo basi. Kuwazuia hao wenye migodi ni kupiteza muda.
 
Si kwamba awajui madhara,sisi waswahili ni watu wa kuupuza Sana mambo
 
Dunia imeamua hivyo acha tuangamie. Hata maabara za kisasa hatari ipo palepale. Cha msingi mshauri mtoto wako asiende kuganta kazi hayo maeneo basi. Kuwazuia hao wenye migodi ni kupiteza muda.
Sumu hizo hazitumiki kwetu pekee,sema atupendi kuchukua taadhari.
Mfano watu wanaambiwa mzitumie vyombo vya plastic uleta Kansa,awasikii,magazeti kufungia Vyakula ni sumu, kuweka chai au Vyakula kwenye mifuko ya plastic sumu tupu.
Hapo utamlaumu vipi Mungu sasa
 
Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya wakemia wanafanya kazi ktk plant si professional pia NEMC hawajui yanayoendelea uko plant kiufupi plant karibu zote za Kanda ya ziwa ni vyanzo vya uchafuzi wa maji.
 
Bro wakemia wengine ni wa kufundishwa juu juu na hao wengi n ma cheap labour hawana gharama na wanapendwa na maboss.
Wataalam wa madini (Processing engineers na technicians) wapo wengi ila wengi wao utawakuta kwenye CIP/CIL plants maana nyingi zinakua monitored na NEMC/TUME YA MADINI,ila hizi VAT leachings wengi wanatumia hao wa kemia wa kuunga wasiojua hata namna bora ya kufanya chemical handling na kusimamia afya zao na wafanya kazi wazungukao maeneo yao ya kazi.
 
Kingine cha kuongezea maboss wapunguze ujuaji na kuajiri cheap labours,Tume ya madini,Nemc na GCLA wawe wakali kwenye haya kuepusha athari za kiafya kwa wafanyakazi wa sekta ya uchenjuaji madini
 
INASIKITISHAA SANAA ANII HADII MOYOO UMEUMIAAA DAAAAAAAAH😭😭😭😭😭😭😭😭😭🥺🥺🥺🥺🥺🥺🥺
 
Asante Artificial Intelligence, Kwa hii
Unaweza saidia inbox migodi ambayo umetembelea bukombe namba moja Geita na ukakutana na kadhia hii ili tuungane kulisemea.
Tukipata muathirika wa haya kwetu wanahabar inakua nzuri Zaid.

Changamoto yetu toka lwa wamiliki wa migodi na.maafisa madini ni kuwa hawako wazi kwetu wakiamini wakisema migodi utafungwa jambo ambalo sio kweli.

Naomba picture na contacts za yule mhanga wa Migodi ya No 1 bukombe aliye haribika macho kwa kemikali.

lubangoseni@gmail.com
 
Naomba jina la mgodi huo wa no1, jina la mhanga na contacts zake
Ili tuone tunamsaodiaje kwa haraka.
Tumeguswa sana sana na hilo.
Asante kutujuza.
Wakati nikiwa Bukombe, sehemu moja inaitwa namba moja, kuna plant moja kijana alikuwa anachanganya conc. Sulfuric acid kwa bahati mbaya sijuhi alikosea nini, kutokana na kuvuta hewa yake kwa sababu moshi ulitanda chumba kizima, alipiga kelele na kuomba msaada, wakati anatolewa kupelekwa kituo cha afya alisema hivi "siwezi kuona", kituoni aliambiwa sumu aliyovuta hawaiwezi ikabidi apelekwe hospitali ya wilaya Bukombe, kiukweli mpaka natoka kule kijana niliacha hajaweza kuona tena.
 
siku siyo nyingi nimeibiwa simu ambayo ilikuwa na picha, contacts , na vitu vyangu vingine ndiyo maana nina siku nyingi sijaingia JF,hivyo kwa kukuwa umejitokeza kusaidia ngoja nifatilie upya ntaktumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…