Inasikitisha, Nimelia sana: Hii picha ya Dr Bashiru ni usaliti mkubwa, sikutarajia

Inasikitisha, Nimelia sana: Hii picha ya Dr Bashiru ni usaliti mkubwa, sikutarajia

nzagambadume,
Hivi hayo mabarabara tunayojisifia kujenga hasa awamu hii yako kona zipi za nchi Hii.....!?

Anyway, yule Police aliyekuwa anaongea kwa uchungu mkubwa na kugonga Meza amepata pa kuanzia.
 
Nilivyoona title "NIMELIA SANA" nikaja kuangalia kama aliyepost ni mwanaume nilipokuta ni mwanaume sikusumbuka kuendelea kusoma.
 
Hawa watu, kama mleta mada, ndio viongozi wetu kwenye nchi hii tukufu sasa!

Kweli tuta-'survive' kwa mwendo huu? Jamaaa kalia sana kwa vile ni Dr Bashiru kakwama hapo. Kuonyesha tu tukio hilo, ni "kuhujumu uchumi"!


Kusikitika kwangu ni kupoteza mda wa kusoma vitu kama hivi.
 
Kwanza hueleweki unalilia nini

Nchi ina changamoto ya barabara serikali ijitahidi kutatua changamoto kuliko kujisifia, kwani barabara zikiwa bora itakuwa siri? Si kila mtu ataona barabara nzuri?

Kuna maeneo serikali imejitahidi barabara ni nzuri na watu hupiga picha na kupost mbona hukuja kulalamika juu ya hilo?

Lengo lake ni kwamba - RC Gambo alimwamuru RPC Shana awakamate na kuwachukulia hatua madereva wa watalii waliopst picha za barabara mbovu ndani ya hifadhi ya Ngorongoro akisema si wazalendo na wanahujumu nchi.

Sasa kuna huyo Sijui Jaji alipost picha hipi ya barabara mbuvu, na hii ya Bashiru aliyoipost.

Yeye anachukidai ni kuwa:
Kama kupost picha za Barabara mbuvu ni kuhujumu huchumi, kwa nini hawa wengine wasichukuliwe hatua kama hao waliochukuliwa hatua huko ngorongoro?
 
Bashiru yuko ziarani Kigoma, kumbe ndio maana Bwana Mkubwa haendi Kigoma, hakuna njia, manake zingekuwepo wangempitisha Bashiru...

Sasa hivi hizo njia za Kigoma zitatengenezwa...

Maendeleo ya Afrika yatakuja siku wakubwa wa hizi nchi wakiwa wanaishi na sisi, wanatumia hizi barabara tunazotumia sisi, shule, basi la mwendokasi, hospitali... Hivi unadhani Waziri wa Afya Ummy Mwalimu anapeleka mtoto wake hospitali Sinza Palestina?
 
Mimi bado nabaki palepale,tunapaswa kutangaza vivutio vyetu kwahabari chanya ili kupata izo fedha za kideni... Habari nyingine zisizohusu specific/targeted income areas tunaweza kuziongelea openly!!!
Huwezi post kitandachako kinapovunjika lkn kiti unaweza post...tusibishe alimradi,tujiongeze kifikra kunavitu ni nyeti na vingine ni vya kawaida ni swala la kuwa na fikra sahihi.
 
Waha Wa Kigoma Wanasema Igari!!!🤨😶😶😃😂😁😄😅
 
Sijawahi kuona uzwazwa kama huu...kupost ubovu wa miundo mbinu ni kuhujumu uchumi...mi nilihisi amerahisisha kazi kwa serikali ili ifanyie kazi sehemu korofi...tena hao wanao post wangepewa pongezi...nchi ni kubwa hii viongoz hawawez kujua kila mahali penye changamoto pasipo wananchi kupaza sauti kupitia social media
 
Barabara kuwa mbovu yaweza kuwa kivutio cha utalii pia. Itategemea huo ubovu ni hatarishi kiasi gani.
Tatizo hapa ni fikra fupi za kujidanganya kwa hisia kali.
Ni muhimu watu wawe na mawazo chanya. Kwa zama hizi za utandawazi unawazaje kuficha ubovu wa barabara?
 
Back
Top Bottom