The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Ku-share data/taarifa binafsi imekuwa muhimu katika kufanya kazi zetu za kila siku na kushirikiana na watu wengine katika jamii.
Mwingiliano wetu na mashirika na taasisi mbalimbali unahusisha ubadilishanaji wa data/taarifa binafsi.
Hizi data/taarifa binafsi ni taarifa yoyote inayokuhusu, iwe inahusiana na maisha yako binafsi, kitaaluma, au ya umma (Mfano: majina, namba za simu, anwani n.k)
Sasa basi, ni mara ngapi unakutana na taarifa za watu wengine katika mazingira ambayo hukupaswa kukutana nazo? Kama ni mara nyingi, basi huenda hata taarifa zako zinazagaa mahali wakati huu bila wewe kujua.
Kwa mfano: Hapa chini ni vielelezo vinavyoonesha nyaraka zenye taarifa binafsi za watu. Yaani unanunua vitumbua, vinakuja na taarifa za watu. Si sahihi. Hizi taarifa zinapaswa kuwa ni siri miongoni mwa wahusika.
Si taasisi binafsi tu ambazo hazioni umuhimu wa kutunza taarifa za watu kwa usiri mkubwa, bali hata taasisi za umma/mamlaka za serikali.
So, nimepiga picha hizo karatasi kwa masikitiko makubwa. Zilitumika kama vifungashio vya chakula.
Kwakweli kunahitajika mwongozo wa jinsi data/taarifa za watu zinapaswa kukusanywa, kushughulikiwa na kuhifadhiwa kulingana na unyeti na umuhimu wake.