Inasikitisha sana: Simba day ishafelishwa na tulioaminishwa ni wa kisasa

Inasikitisha sana: Simba day ishafelishwa na tulioaminishwa ni wa kisasa

maatope

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2013
Posts
1,422
Reaction score
957
Nikiwa kama mshabiki wa simba nawapa pole wote mnaoshindwa kununua tiketi za Jumapili, msiwe na wasiwasi ikifika Jumatatu wahusika watarudisha system yao vizuri

Mwaka jana walifanikiwa ku frustrate wanunuzi wa tiketi na mwaka huu bado siku mbili jamaa wanaupiga mwingi sana hadi sasa huku kina Kamwaga wakiwa busy kuhamasisha watu wanuunue tiketi ambazo wenye kumiliki system wanahujumu klabu kwa sabotage ya kibabe kabisa.

Basi tena labda tusubiri mwakani kama kutakuwa na sytem nyingine ya kununua tiketi angalau wao UTOPWINYO mwananchi day yao huwa haikumbwi na hujuma hizi zenye kiwango cha kimafia
 
Simba ili kuondoa aibu ya kuto ujaza uwanja, wangetumia shamba la Bibi. Kutaka kushindana na Wananchi hawawezi, Wananchi hawaitaji promo wenyewe wanakwenda kwa mapenzi.
 
Kwamba Haji ni sawa na mzazi? Mbona umetumia mfano ambao hauhusiki kabisa hapa?
Isiwe nongwa Mfano mwingine ni huu..

Wachezaji hawajui kama ni jukumu lao kwenda kucheza vizuri uwanjani wapate matokeo? Kama wanajua mbona bado makocha na wamiliki wanawahamasisha na muda mwingine wanawatangazia hadi bonus wakipata matokeo mazuri?
 
Sijawahi kwenda uwanjani kwa kuhamasishwa na Manara,nakwenda kwa pesa yangu na mapenzi kwa Simba.Mimi na familia yangu kwa Mkapa Jumapili asubuhi tu.
Wapo wenzako waliowahi kwenda kwa kuhamasishwa nae. Sio kila mtu anaweza kula wali mkavu wengine mpaka mboga iwepo
 
Isiwe nongwa Mfano mwingine ni huu..

Wachezaji hawajui kama ni jukumu lao kwenda kucheza vizuri uwanjani wapate matokeo? Kama wanajua mbona bado makocha na wamiliki wanawahamasisha na muda mwingine wanawatangazia hadi bonus wakipata matokeo mazuri?
Kwamba Haji hakuwahamasisha wachezaji wa Yanga dhidi ya Rivers na Zesco?
 
Back
Top Bottom